- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kuhitimu kwa Maelfu ya Waliohifadhi Qur'an hakutabadilisha hali ya Umma wa Kiislamu isipokuwa wawe miongoni mwa wale wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah
(Imestafsiriwa)
Katika miaka ya hivi karibuni, hamu ya Waislamu katika kuhifadhi Qur'an Tukufu imeongezeka sana, na kundi la watoto wakiume na mabinti watiifu wa Umma wa Kiislamu limejipanga kuanzisha jumuiya zaidi za Qur'an na kujishughulisha na kuwafundisha wanafunzi Tajweed ya Qur’an, ikijumuisha kisomo, usomaji, kuchora, adabu na tafsiri, kwa matumaini ya mabadiliko na kuushika mkono Ummah kuelekeza kwenye uongofu wake na kubadilisha hali yake. Jumuiya zimeanzishwa na kuzidishwa, na shule za mtandaoni, makundi ya Facebook, makundi ya WhatsApp, n.k. pia yameongezeka, na kauli mbiu ni moja: kuitumikia Quran Tukufu.
Ingawa inafurahisha kushuhudia sherehe za mahafala za maelfu ya wabebaji Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika sehemu mbalimbali za nchi za Kiislamu, na shauku ya vijana na wazee kuhifadhi maneno ya Mwenyezi Mungu na kuyasoma usiku mzima na jioni kwa Lugha fasaha ya Kiarabu kwa sauti nzuri zisizo fichika, ni muhimu kukumbusha mambo makubwa kwa wale ambao lengo lao ni kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt):
1- Kuyafanyia kazi yaliyoteremshwa na Qur’an ni faradhi na ndio msingi, na ndio maana Maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, walikuwa wakiipokea Qur’an ili kutekeleza na kutii maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake, na wakamwomba Mwenyezi Mungu wasiwe miongoni mwa wanaozichunguza herufi zake na kutumia mipaka yake vibaya. Kwa hivyo, hasara yote ni pale Muislamu anapotumia maisha yake kuhifadhi Qur’an au kuwafundisha wengine huku akiwa mbali na kuzifahamu hukmu zake na kuzitekeleza. Inajulikana kutokana na dini kwa ulazima kwamba kushikamana na hukmu za Uislamu ni faradhi kwa kila Muislamu, mwanamume na mwanamke. Na jambo hili japokuwa tunakumbushwa nalo, lakini mawaidha yetu si suala la kudunisha ujira mkubwa wa mwenye kuhifadhi, na pia linajulikana kutokana na yaliyokuja katika Hadith, bali ni suala la kuweka mambo mahali pake na kuyaweka mambo mahali pake na kuweka nukta kwenye herufi.
Kuzifahamu hukmu za Uislamu na wajibu wa kuzipokea kwa ajili ya kuzitekeleza kunamlazimu Hafidh kutafuta neno la Mwenyezi Mungu ili kuregesha uwepo wa Dola ya Kiislamu, na awe kwenye moja ya mianya ya Uislamu, aamrishe mema na akataze maovu. kujali mambo ya Waislamu wote, kufuatilia habari zao, kutafuta kuwanusuru waliodhulumiwa, na kutojitenga na uhalisia kwa kujifungia kwenye kinu chembamba, kana kwamba yuko kwenye bonde moja na umma wake uko kwenye bonde jengine!!
2- Kuzingatia kazi ya ushirika pekee na kuwahitimisha maelfu ya wenye kuhifadhi haitoshi kuuokoa Ummah wa Kiislamu na yale uliyoyafikia, kwa sababu maradhi yake yanajulikana vyema, ambayo ni kukosekana kwa dola inayotawala kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu (Shariah), na licha ya jinsi idadi inavyoongezeka na kujiunga na safu za wale wanaoifuata Qur’an, robo tatu ya hukmu za Uislamu zitabaki kuwa hazipo na kusimamishwa, na tutaulizwa kuzihusu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Hizi ni pamoja na hukmu za kisiasa na kiuchumi, mfumo wa adhabu, mipaka ya ndani na nje, na mengineyo.
Tunajua kwamba wengi wa wale walioanza kazi ya ushirika wana kheri nyingi na shauku kubwa ya kuitumikia dini, lakini ni lazima lengo liwe wazi na njia ya mabadiliko ijulikane kwao ili kufanikiwa katika lengo lao.
Mtume wetu Mtukufu (saw) alikuwa amejishughulisha na kazi ya kisiasa, na si siri kwa watu wawili kwamba alifanya kazi ya kusimamisha dola na hata kuisimamisha Madina baada ya wenye kunusuru - Ansari - kumkumbatia (saw) na kukiamini alichotmilizwa kwacho, na kila mtu pia anajua jinsi dola iliweza wakati huo kuunganisha mujtamaa wa kwanza kwa fahamu za Uislamu, na jinsi ilivyouinua na kujumuisha ndani yao sadaka na wema. Na waliishi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), wakibeba bendera ya Uislamu kwa ulimwengu mzima.
Je, hadi lini waliozembea hawatachukua hatua yoyote katika kazi kubwa ya kisiasa inayoendelea kama matokeo ya upotoshaji na udanganyifu ambao maadui waliunadi?! Je mpaka lini Juhudi za ukarimu zitatumika kutibu dalili pasi na kuugundua ugonjwa na kuutumilia dawa?!
Inafaa kwa wenye kuhifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu leo wawe katika safu ya kwanza ya wale wanaofanya kazi ya kuleta mabadiliko na kuhuisha Umma wa Kiislamu, na inafaa kwao kufuata nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Da ́wah na kupigana na Makafiri, katika mapambano ya kifikra, wanaokandamiza haki na kuisukumana kwa mikono ya madhalimu. Hili ndilo pengo lao ambalo wanapaswa kulijaza, na haitoshi kwao kujishughulisha tu na elimu, kazi ya hisani, au kitu chengine chochote.
Kurekebisha watu binafsi hakubadilishi jamii kwa sababu jamii zimejengwa juu ya fikra, hisia, na mifumo inayowadhibiti na kutawala katika mazingira yao ya kijamii. Inahitajika kuondoa mkanganyiko huu kutoka kwa akili ili kufafanua kile kinachohitajika na njia ambayo lazima ifuatwe. Ukiwalingania watu kuwa wema wao binafsi, hili huzalisha watu wema tu, na hili aghlabu halipelekei wema wa jamii, kwani wengi wa watu huathiriwa na mazingira jumla na sheria zinazotekelezwa juu yao, na kwa hiyo ni lazima zikusudiwe na kubadilishwa ikiwa kiu ni kali ya kufanya mabadiliko.
Kuuawa shahidi kwa wengi katika muktadha huu kunatokana na kauli ya Mwenyezi Mungu:
[إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ]
“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Ar-Ra’d 13:11] kudai kwamba mageuzi huanza na kujibadilisha kibinafsi tu ni shahada ya kimakosa. Mabadiliko katika jamii yanawezekana tu kwa kuwepo watu wema na warekebishaji, kwa mujibu wa yale yaliyokuja katika Hadith:
«لَتَأْمُرُنَّ بالْمعْرُوفِ، وَلَتَنْهوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ، ولَتَأْخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ، ولَتَأْطِرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ أَطْراً، ولَتقْصُرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ قَصْراً، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللَّه بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ، ثُمَّ لَيَلْعَنكُمْ كَمَا لَعَنَهُمْ»
“Hamutaacha kuamrisha mema na hamutaacha kukataza maovu na hamutaacha kuukamata mkono wa dhalimu na hamutaacha kumshawishi atende uadilifu na kushikamana na haki, isipokuwa Mwenyezi Mungu atazigonganisha nyoyo zenu nyinyi kwa nyinyi, kisha atawalaani kama alivyowalaani wao.” Hadith hii inaashiria dalili ya wazi ya ufaradhi wa Muislamu kujitahidi kubadilisha batili inayomzunguka, ambayo inajumuisha dhulma ya watawala na kuikamata mikono ya dhalimu, lakini ikaiita Hadith hii kuwa ni muundo wa haki na akaonya matokeo ya kutofanya hivyo. Na akaulizwa (saw) katika tukio jengine: “Je, tuangamie, na wamo miongoni mwetu wema? Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema:
«نَعَمْ، إِذَا كَثُرَ الْخَبَثُ» “Ndiyo, pindi unapokithiri uovu.” Je! ni uovu gani mkubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko haya yanayotokea leo katika suala la kuvuruga Shariah Yake, kupora mamlaka ya Ummah, kuwagawanya Waislamu, na kuwafanyia uadui?! Na kuna manufaa gani kwa wema miongoni mwetu kuongezeka ikiwa wao sio watengenezaji?!
Mwenye kuchunguza yale aliyoyafanya Mjumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) mjini Madina kabla ya kuasisiwa dola ya kwanza ya Kiislamu, atatambua kwamba Mus’ab al-Khair hakujiweka katika kuwafanya watu wa Madina kuhifadhi peke yake pindi walipoikubali Qur'an ili wapate kuongoka kwayo. Bali, kazi yake, na wale waliosilimu pamoja naye, ilikuwa ni kuandaa rai jumla kwa ajili ya kuunusuru Uislamu kupitia kutafuta watu mashuhuri, kuyalingania makundi, kufichua batili (al-batil), kupiga vita ufisadi, na kulenga fikra na hisia za jamii na mfumo unaotekelezwa kwao. Kwa hiyo, wale ambao hamu yao ni mwamko wa Ummah lazima wasitumie juhudi zao katika mambo ambayo hayafikii lengo lile lile.
Enyi wabebaji Kitabu cha Mwenyezi Mungu: Kuweni wastahiki wa kile mnachokibeba vifuani mwenu, na kuweni watu wema na watengenezaji, wanaoamrisha mema na kukataza maovu, wenye kusema haki hata mbele ya mtawala dhalimu, wala msizinunue Aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo. Kuweni wanasiasa kama vile Mtume wenu (saw) alivyokuwa akichunga mambo ya watu na kuuwasilisha Uislamu kama badali ya tawala za kilazima, na songeni mbele kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu:
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur 24:55]. Na yeye (saw) amesema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”.
Haya ndiyo mapengo ambayo ni lazima muyazibe, kwani Wallahi hii ndiyo njia sahihi kwa wale wanaotaka kuutumikia Uislamu na kuitumikia Qur’an. Mwenyezi Mungu (swt) atuongoze sisi na nyinyi kwa yale anayoyapenda na kuyaridhia.
Imeandikwa kwa Ajili ya Upeperushaji wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Mennah Tahir
Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:
#Time4Khilafah |
#EstablishKhilafah |
#ReturnTheKhilafah |
#TurudisheniKhilafah |
#KhilafahBringsRealChange |
#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي |
أقيموا_الخلافة# |
كيف_تقام_الخلافة# |
#YenidenHilafet |
#HakikiDeğişimHilafetle |