Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Katuni ya Kejeli ya Ufaransa Inadhihaki Waislamu Wanaokufa baada ya Matetemeko ya Ardhi ya Uturuki na Syria

(Imetafsiriwa)

Uhuru wa kuwatukana na kuwaonyesha chuki Waislamu ni jambo ambalo sheria ya kimataifa inaruhusu na kamwe haitoadhibu kwani inaunga mkono mateso ya Umma.

Jarida la Charlie Hebdo, ambalo linajulikana kwa katuni za kumtukana Mtume (saw), lilianza tena matamshi yake ya chuki kwa kuchapisha katuni ya jengo lililoporomoka kutokana na tetemeko la ardhi likiwa na maandishi yanayosema, "hakuna haja ya kutuma vifaru (kuwaua Waislamu)". Kejeli hizi za kinyama za mateso ya Umma hazijalaaniwa rasmi na kiongozi yeyote, Muislamu au asiye Muislamu, kwani uhuru wa kujieleza siku zote ni kisingizio kinachotolewa pale kipengele chochote cha thaqafa ya Kiislamu kinapochafuliwa.

Idadi ya vifo vya sasa ni zaidi ya 22,000 kufikia wakati wa kuchapisha toleo hili, na bado inaongezeka. Maelfu ya wanawake na watoto wamekufa, na mamia ya watoto mayatima wamepoteza familia zao na majina katika janga hilo.

Kuna taarifa za watu ambao wameona picha za vijana wakiokolewa kutoka kwenye maafa hayo, lakini wametoweka katika sokomoko na kuvurugika kwa mchakato wa baada ya tetemeko la ardhi. Wahalifu wa kimpangilio na vikundi vya mafia wameripotiwa katika maeneo hatari bila nia ya kusaidia, bali wakipora tu vitu vya thamani wanavyoweza kupata.

Uturuki na Syria tayari zina tatizo la ulanguzi wa binadamu, na hakuna njia ya kuhakikisha kuwa watoto walio katika mazingira magumu hawatekwi nyara au kuchukuliwa na wale wenye nia za kikatili.

Muda unaochukuliwa kuwatusi wale wanaokabiliwa na janga hili ni akisi ya mifumo ya kikatili inayoendesha ulimwengu leo chini ya mwelekeo wa utaifa na ubaguzi wa rangi. Watawala wetu wanaruhusu kura ya turufu ya Umoja wa Mataifa kuzuia misaada kuingia Syria, huku Urusi na China zikiongoza juhudi za kuongeza vifo vya wale wanaohitaji zaidi. Hivi sasa, kuna kituo kimoja tu cha ukaguzi nchini Syria ambacho Umoja wa Mataifa umeidhinisha kwa ajili ya msaada kuingia katika eneo la maafa. Vyengine vitatu vimefanywa kuwa haramu.

LA HAWLA WALLA QAWITTA ILLAH BILLAH!

Mwenyezi Mungu (swt) ametoa amri ya kutuma msaada na kuwasaidia kaka na dada zenu katika nyakati zao za shida na majanga ya kimaumbile. Umar Ibn Al-Khattab (ra) alikusanya msafara wa ngamia ulioanzia kutoka ncha moja ya Bara Arabia hadi nyengine ili kuwasaidia wale wanaokabiliwa na njaa nchini Misri.

Ni kukosekana kwa Khilafah ndiko ambako kunawapa idhini maadui wa Uislamu kufikia haki zao za kibinadamu katika ulimwengu wa Kiislamu.

Majanga ya kimaumbile yanatoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) lakini njia ya kukabiliana nayo haitekelezwi. Hii ni Haramu kubwa inayohitaji kukomeshwa mara moja kabla ya mitihani mengine kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuusibu Ummah.

Mwenyezi Mungu (swt) anazungumza kuhusu wale wanaokejeli amali hiyo kuwa na adhabu kali, lakini wale wanaozuia kabisa kukabiliana na mateso na udhalilifu wa sasa wa Ummah pia watakuwa na gharama kubwa ya kulipa katika maisha ya akhera. Dunia inapaswa kuondokana hivi karibuni na wale wanaofurahia maneno maovu na kejeli kwa Waislamu.

Imepokewa na Abu Qatada bin Rib'i Al-Ansari: Bukhari na Muslim

مُرَّ عَلَيْهِ بِجِنَازَةٍ فَقَالَ: «مُسْتَرِيحٌ، وَمُسْتَرَاحٌ مِنْهُ». قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا الْمُسْتَرِيحُ وَالْمُسْتَرَاحُ مِنْهُ؟ قَالَ: «الْعَبْدُ الْمُؤْمِنُ يَسْتَرِيحُ مِنْ نَصَبِ الدُّنْيَا وَأَذَاهَا إِلَى رَحْمَةِ اللَّهِ، وَالْعَبْدُ الْفَاجِرُ يَسْتَرِيحُ مِنْهُ الْعِبَادُ وَالْبِلاَدُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ»

Msafara wa mazishi ulipita kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye alisema: “Amepumzishwa au anapumzisha?” Watu wakauliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)! Ni nini maana ya kupumzishwa au kupumzisha?” Akasema: “Muumini hupumzishwa (kwa mauti) kutokana na shida na dhiki za dunia na anaondoka kwenda kwa Rehema ya Mwenyezi Mungu, huku (kifo cha) mtu muovu huwapumzisha watu, ardhi, miti, (na) wanyama kutokana naye.”

Kamwe hatupaswi kuogopa matokeo ya kusimama dhidi ya makosa ya wakati huu wa mtihani. Tunajua kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amewaahidi Waumini ushindi na kufeli hakuna umuhimu wakati kutochukua hatua dhidi ya Munkar (uovu) ni kushindwa kukubwa zaidi. Msimamo wetu Siku ya Kiyama mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) ndio jambo pekee tunalopaswa kuwa nalo juu ya pato au cheo chochote cha dunia.

[مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِنْ ذَكَرٍ أَوْ أُنْثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُمْ بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ]

“Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” [Al-Nahl 16:97].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu