Jumamosi, 30 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 [وَكَانَ حَقّاً عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ]

“...Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.” [Ar-Rum: 47]
(Imetafsiriwa)

Hali chungu ya Waislamu na maisha yao duni katika sehemu zote za ardhi haifichiki kwa mtu yeyote. Popote unapogeuza macho yako, utaona mataifa yanayopigana dhidi yao na nchi zao na uwezo wao, na watawala wao wahalifu wanawatawala, na utaona vita, umaskini, njaa, ukosefu wa usalama na vikwazo juu yao katika kutekeleza ibada zao na kushikamana na ibada za dini yao. Waislamu wengi, kwa kuzingatia uhalisia huu mchungu, wamekata tamaa na kufadhaika, na wamepoteza matumaini kwamba hali itabadilika, kwamba giza la usiku litapita, na kwamba alfajiri itapambazuka. Hakika wengine wamekata tamaa na watu na wakakanusha kheri na uadilifu kutoka kwao, kwa hivyo walivunjika moyo na wakaacha kufanya kazi ili kubadilisha uhalisia huu mchungu, na hata wakaanza kuwakejeli wafanyikazi wa mabadiliko na juhudi zao.

Kanuni msingi kwa Muislamu, pamoja na uhalisia huu chungu, ni kwamba asipoteze matumaini yake na kukata tamaa na rehma ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha kukata tamaa na kukosa matumaini; Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّهُ لاَ يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللّهِ إِلاَّ الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ]

“Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri.” [Yusuf: 87]. Kukata tamaa ni tabia mbaya kwa Mwenyezi Mungu (swt):

[وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنْسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَى بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ كَانَ يَؤُوساً]

“Na mwanaadamu tunapo mneemesha hugeuka na kujitenga kando. Na inapo mgusa shari hukata tamaa.” [Al-Isra: 83]. Na kama ambavyo Muislamu hapaswi kukata tamaa na rehma na msaada wa Mwenyezi Mungu, hapaswi kukata tamaa na watu na kufikiri kwamba anawaaga, kwani Umma wa Uislamu ni Umma wa kheri; kheri na matumaini havikosekani kwa watoto wake, kama (saw) alivyosema «إِذَا قَالَ الرَّجُلُ هَلَكَ النَّاسُ فَهُوَ أَهْلَكُهُمْ»Pindi mtu anaposema: Watu wameangamia, basi yeye ndiye aliye angamia kuliko wote.” Ina maanisha ameangamia zaidi miongoni mwao, na ikapokewa kwamba “amewaangamiza” kwa tuhma, na maana yake ni kuwafanya waangamie, sio kwamba wameangamia kwa hakika.

Muislamu hana budi kuzingatia kwamba nguvu na uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt) unazidi nguvu za madhalimu na wakandamizaji wote, na kwamba tunaloliona kuwa ni gumu au haliwezekani ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu. Ujasiri huu ndio msingi wa itikadi yake, ambayo inamlazimu kuamini hilo kwa imani thabiti isiyo na shaka na isiyochanganywa na shaka. Waislamu katika vita vya Al-Ahzab, licha ya makafiri kuungana na kupigana dhidi yao na uhaba wao wa nguvu, walikuwa na imani na ushindi wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَذَا مَا وَعَدَنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَاناً وَتَسْلِيماً]

“Na Waumini walipo yaona makundi, walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na ut'iifu.” [Al-Ahzab: 22]. Kinyume na msimamo wa wanafiki na wazushi, ambao Mwenyezi Mungu (swt) aliubainisha kwa kauli yake:

[وَإِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ مَا وَعَدَنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ إِلَّا غُرُوراً]

“Na walipo sema wanaafiki na wale wenye maradhi katika nyoyo zao: Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu,” [Al-Ahzab: 12]. Nakumbuka hapa kile kilichosimuliwa kuhusu Umar al-Mukhtar, kwamba aliambiwa: “Italia inamiliki ndege, lakini sisi hatumiliki.” Akasema: “Je! Wanaruka juu ya Arshi au chini ya Arshi?” Wakasema: “Chini yake, ewe Umar.” Akasema: “Yule aliye juu ya Arshi yuko pamoja nasi, basi yasituogopeshe yaliyo chini yake.”

Mtihani na uchunguzi ni miongoni mwa Ahkaam (sheria) za Mwenyezi Mungu Ulimwenguni ili kutofautisha wabaya na wema, na kuwanusuru wale wanaomnusuru Yeye (Dini Yake). Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[أَمْ حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُمْ مَثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلِكُمْ مَسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّى يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ ءَامَنُوا مَعَهُ مَتَى نَصْرُ اللَّهِ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِيبٌ]

“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.” [Al-Baqara: 214]. Katikati ya mitihani na misukosuko, imani ya Muumini kwa Mola wake na nusra yake kwa waja wake huonekana; Bwana wetu Musa, alipotoka yeye na waliokuwa pamoja naye na Firauni akawafuata mpaka akaishia baharini, hakuwa na pa kukimbilia, lakini alikuwa na yakini na nusra ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[فَلَمَّا تَرَاءَى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَى إِنَّا لَمُدْرَكُونَ قَالَ كَلَّا إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ]

“Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana! * (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa!” [Ash-Shu’ara: 61-62].

Wakati bwana wetu Muhammad (saw) alipokuwa anafuatwa na Maquraishi, alimuahidi Suraqa vikuku vya Kisra, na akamhakikishia Abu Bakr walipokuwa ndani ya pango kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja nao na kwamba atawanusuru. Kutoka kwa Abu Bakr As-Siddiq (ra) amesema: “Nilitazama miguu ya washirikina tukiwa ndani ya pango, nayo ilikuwa juu ya vichwa vyetu. Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, lau mmoja wao angetazama chini ya miguu yake, angetuona. Akasema (saw): «يَا أَبَا بَكْرٍ، مَا ظَنُّكَ بِاثْنَيْنِ اللَّهُ ثَالِثُهُمَا» “Ewe Abu Bakr! Unadhani vipi kwa wawili ambao wa tatu wao ni Mwenyezi Mungu?

Katika historia yao yote, Waislamu wamepitia nyakati za shida na uhalisia mchungu, kama sisi, hadi ikafikiriwa kwamba Uislamu na Waislamu hautakuwepo tena, kama vile uvamizi wa Makruseda wa Jerusalem na uvamizi wa Mamongolia na Matatari katika nchi za Kiislamu, lakini Mwenyezi Mungu akauwepesishia Ummah huu watu waliokuwa wakweli kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakailinda mipaka yake, na akawapa ushindi na akawapa mamlaka juu ya adui zao. Mwenyezi Mungu (swt) asema: ﴾وَكَانَ حَقّاً عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ﴿ “...Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.” [Ar-Rum: 47].

Mwanadamu kimaumbile anapenda habari njema, na nafsi yake hutulia kwayo, na humpa ari yenye nguvu ya kutenda, na bishara njema za ushindi kwa Uislamu na Waislamu na kutawala kwao juu ya dunia ni nyingi, ikiwemo kauli yake Mwenyezi Mungu:

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur :55].

Na bishara njema ya Mtume (saw), ya kurudi Khilafah baada ya utawala wa kutenza nguvu: «تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً عَاضّاً فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Utume utakuwepo kwenu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha Atauondoa atakapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume na itakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha Ataiondoa Atakapo kuiondoa, kisha utakuwepo utawala wa Ufalme wenye kung’ata, utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, kisha Atauondoa atakapo kuundoa, kisha utakuwepo na utawala wa kidhalimu utakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa atakapo kuuodoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” kisha akanyamaza.” Na tunazo bishara zake njema za kupanuka kwa Uislamu na kuingia kwake katika kila nyumba «لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ، وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ، بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ؛ عِزّاً يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ، وَذُلّاً يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ» “Jambo hili kwa hakika litafika kila mahali panapofikiwa na usiku na mchana. Mwenyezi Mungu hataacha nyumba wala makaazi isipokuwa Mwenyezi Mungu ataiingiza dini hii ndani yake, ima kwa kupewa izza wenye izza au kwa kudhalilishwa madhalili. Izza ambayo Mwenyezi Mungu atautukuza kwayo Uislamu na udhalilifu ambayo Mwenyezi Mungu ataudhalilisha ukafiri.” Mwenyezi Mungu na Mtume wake kamwe hawavunji yale waliyoahidi, na twamuomba (swt) kwamba hili liwe hivi karibuni, na kwamba tuwe miongoni mwa mashahidi wa siku hizo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bara’ah Manasrah

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu