Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tatizo la Wakimbizi

(Imetafsiriwa)

Tatizo la wakimbizi ni mojawapo ya majanga ya kibinadamu yanayotokana na ukoloni uliozaliwa na mfumo wa kibepari, na ufumbuzi wa tatizo hili unawezekana kwa kuangamizwa ukoloni.

Mapinduzi yaliyotokea Ulaya baada ya Zama za Kati, yalifichua mfumo ya kibepari. Kwa Mapinduzi ya Viwanda yaliyofuata mara moja baada ya hapo, nchi za Magharibi zilipata maendeleo na nguvu kubwa ambayo nchi nyingine hazingeweza kushindana nazo zenyewe. Ili kupata utajiri na raslimali zinazohitajika kwa ajili ya tasnia na ustawi wao, wakiwa na uwezo huu mkubwa mikononi mwao, walivamia na kuziteka nchi zilizoko sehemu kubwa ya Asia, Afrika na Mashariki ya Kati, ambako utajiri na rasilimali hizo zinapatikana, na kugundua ukoloni. Uingereza, Ufaransa, Uholanzi, Uhispania na Ureno zikawa nchi kuu katika ukoloni huu.

Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Marekani ilijiunga na nchi hizi za kikoloni. Pamoja na nyongeza ya Marekani miongoni mwao, ukoloni umekuwa ni njia inayotumiwa na nchi zilizoendelea kiviwanda na zilizoendelea katika unyonyaji wa mali na rasilimali katika nchi zilizo nyuma ambazo hazina uwezo wa kuzipinga, na katika kuenea kwa Mfumo wa Kibepari.

Ilitumia mitindo ya kijeshi, kisiasa na kiuchumi ili kuanzisha ushawishi wake barani Amerika, Asia, Afrika na Mashariki ya Kati, haswa katika makoloni ya Uingereza na Ufaransa yaliyoko katika maeneo haya. Ililingania haki ya mataifa kuamua uhuru wao, huria, usawa, uadilifu na haki za binadamu. Kutokana na hali hii mpya, nchi za kikoloni zililazimika kuyapa makoloni yao kile kinachoitwa uhuru wao.

Walipoondoka, waliwaleta mameneja wasimamizi waliowaajiri kutoka kwa wenyeji wa nchi hizi kufanya kazi mahali pao. Na kisha mameneja hawa vibaraka waliendelea kunyonya mali na rasilimali za nchi hizi kwa mikono yao. Walizuia maendeleo ya nchi hizi, walizuia kufikia hali ya kushindana na wao wenyewe, walizishutumu kwa kubaki nyuma kuwa wazi kwa unyonyaji, waliwaacha watu wa nchi hiai na njaa na taabu, kwa asili ya kibinadamu waliwanyima haki, wakawaacha chini ya shinikizo na mateso ambayo ilikuwa vigumu kuyahimili.

Matokeo ya haya yote, watu ambao hawakuweza kufikia mahitaji katika nchi yao wenyewe na kunyimwa haki zao za asili za kibinadamu walianza kutafuta hifadhi katika nchi zilizoendelea ambapo wangeweza kupata mahitaji yao kwa urahisi na bila kushinikizwa, na waliikabili dunia kwa tatizo kubwa linaloitwa wakimbizi/watafutaji hifadhi na janga jipya la kibinadamu la kusikitisha.

Kinaya na hali ya kutapatapa ya kujaribu kujiepusha na njaa, taabu na ukandamizaji unaosababishwa na ukoloni wa dola za Marekani na Ulaya, mtekelezaji wa mfumo wa kibepari, na hatua zinazochukuliwa na Dola za Magharibi dhidi ya watafutaji hifadhi hawa, pamoja na kasumba ya kikatili, pia ni suala linalohitaji kutathminiwa.

Tatizo hili, ambalo limekuwepo mbele ya dunia kwa muda mrefu, linaumiza dhamiri ya wanadamu karibu kila siku, kujikumbusha na kujiweka kwenye ajenda, halijatatuliwa, bali haliwezi kutatuliwa. Suluhisho la tatizo halipaswi kutarajiwa kutoka kwa wale ambao tayari wameliunda tatizo hili.

Kama ilivyoelezwa mwanzoni mwa makala haya, tatizo la wakimbizi litatoweka tu kwa kuangamizwa ukoloni uliojidhihirisha wenyewe. Ukoloni unaweza kuzuiliwa na dola kubwa na zenye nguvu za Marekani na Ulaya zilizousababisha, na pia kwa pigo kali ambalo dola nyengine kubwa na yenye nguvu ambayo ina ukubwa na nguvu ya aina yake na inaweza kupigana na ukoloni itawapiga wakoloni.

Leo hii, sio tu katika bara la Asia, Afrika na Mashariki ya Kati, hakuna fikra au dola duniani inayoweza kupambana na ukoloni na dola za kikoloni.

Hivi sasa, Uislamu ndio badali na chaguo pekee mbele ya mfumo wa kibepari wa kikoloni duniani, sio tu kwa wakimbizi au wanaokandamizwa, bali kwa Waislamu wote na wanadamu wote wanaoteseka katika mfumo fisadi wa ubepari. Kwa sababu hautekelezwi, uko mbali na uwanja wa maisha na mapambano dhidi ya ukoloni.

Iwapo Khilafah ya Kiislamu yenye nguvu itasimamishwa tena itakayouwezesha Uislamu kurudi kwenye uwanja wa maisha, kuutekeleza Uislamu, kuwaunganisha Waislamu wote chini ya uongozi wa kifikra na kisiasa wa Uislamu, na katika ardhi za Kiislamu na wakimbizi kuupiga vita ukoloni na dola za kikoloni katika nchi zao wenyewe, ukoloni unaweza kumalizwa, na watu wanaoishi hapa hapo watapata fursa ya kutumia mali na rasilimali zao.

Ufunguzi mkubwa umefanywa na Makhalifa ambao wameutekeleza Uislamu kwa karne nyingi, na watu ambao wameteswa na kudhulumiwa kwa njaa na taabu wameokolewa kutoka kwa dola na tawala ambazo zimewafanyia mambo haya. Dola ya Khilafah haikuwanyonya watu wa nchi walizozifungua kama dola za kikoloni za kibepari za leo, lakini kinyume chake, walileta uadilifu na ustawi. Hawakuwanyang'anya mali na rasilimali zao na waliondoa vikwazo vya matumizi yake kwa watu hawa.

Kwa sababu hii, watu wa nchi zilizofunguliwa na Dola ya Khilafah hawakulazimika kuhama kwenda nchi nyingine na kupata hifadhi, walipendelea kuishi kama raia wanaoheshimika wa Dola ya Khilafah. Historia ni shahidi wa hili.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Remzi Özer – Wilayah Uturuki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu