- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Zama za Mitandao ya Kijamii: Ufichuaji wa Uongo
(Imetafsiriwa)
Kwa miaka yote, ulimwengu wa Kimagharibi umeweza kufanya ukatili dhidi ya nchi, kwa kuhadaa kuwa wao wanasaidia nchi wahitaji, katika magazeti kama ‘New York times’, na programu mpya kama ‘Fox news’.
Mifano ya hili inajumuisha vita vya Iraq, vilivyouwa zaidi ya watu 650,000, vimefanywa kuwa ni lazima kwa sababu Washington iliamini kuwa kuna “Ushahidi muhimu kuwa Iraq ina silaha za maangamizi makubwa, na hivyo kuwa ni tishio halisi”.
Ilipokuja suala la ‘uingiliaji’ nchini Yemen, ilidai kutaka kusaidia kuishinda serikali ya Houthi. Kila Marekani inapotaka kuivamia nchi nyengine hutumia vyombo vya habari, inajifanya yenyewe kuwa ni shujaa kwa watu wake.
Hata hivyo, kuibuka kwa mitandao ya kijamii, watu wamejikuta wakiweza kuunganika na walioko maeneo mengine ya dunia. Hili liliyapa faida makampuni na serikali hadi ilipotumika dhidi yao. Wakati mauwaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina yalipoanza, watu wa Gaza waliweza kuunganika kwenye majukwaa kama ya TikTok na kuchapisha picha na video juu ya hali ya sasa.
Pia, muunganiko huu uliwawezesha kusoma uongo wa umbile la Kiyahudi na Marekani ilipojaribu kuutoa, na ukawapinga kwa kuchapisha video na picha zinazowasuta.
Wakati dola za Magharibi zilipodai kupeleka misaada kwa watu wa Palestina, watu walionyesha kwa haraka ushahidi kuwa kile walichokipokea ilikuwa ni mifuko ya kuwekea maiti.
Wakati umbile la Kiyahudi lilipojaribu kudai kuwa watu wake wanateseka kwa sababu ya mashambulizi ya Hamas, watu wanaona video za askari wa IDF wakichukua filamu za TikTok wakicheza dansi katika majengo yaliovunjwa ya watu wa Palestina.
Wakati Marekani ilipodai kupeleka misaada wakati wa Ramadhan, watu wa Palestina walionyesha kuwa misaada imewezesha kuwauwa watu na ilikuwa na nyama za nguruwe na vyakula vilivyomaliza muda wake.
Machapisho ya hivi karibuni mitandaoni yalionyesha maandamano ya wanafunzi katika vyuo vikuu vya Marekani kama USC na Havard yakiitwa “upigaji kambi.” Maandamano haya yamekumbana na usitishwaji na uingiliaji wa polisi na vikosi vya jeshi.
Maandamano haya yamerikodiwa na yanaenea katika majukwa ya mitandao ya kijamii kama TikTok. Video zinaonyesha wanafunzi wakijiwekea vizuizi katika majengo kuwazuia polisi na wanajeshi kuingia, zimesambazwa kwa maelfu, huku video moja ikionyesha mwanafunzi akimgonga askari kwa chupa tupu ya maji ikiwa ndio nembo ya upinzani dhidi ya “serikali ya kifashisti”.
Yote haya yamepelekea serikali ya Marekani kupitisha mswada wa kuzuia TikTok nchini. Seneta Pete Ricketts amefichua kuwa uzuiaji huu umetokana na ukweli kuwa “video za uungaji mkono Wapalestina na Hamas katika TikTok zimesambaa zaidi kuliko mitandao 10 ya habari ya Marekani ikijumuishwa pamoja”.
Marekani imeona kuwa haiwezi tena kuficha kuhusika kwake katika mauaji ya halaiki kwa watu wasio na hatia kwa ajili ya faida. Hii imewaacha katika hali ya kutokuwa na uhakika wa namna ya kuregesha tena huruma ya watu wake wenyewe, kwa vile kila jaribio la kudanganya limeweza kufichuliwa mara moja na hata kusababisha chuki zaidi na kutoaminiwa kwa serikali. Hii imewasukuma kupiga marufuku majukwaa, ikithibitisha kwa umma kuwa fahamu ya ‘uhuru wa kusema’ unatumika tu pindi unapomiliki pesa na kuwa na fikra zinazowiana na mahitaji ya serikali.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Isra Tarchoun