Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kwa Mujibu wa Uislamu, Hairuhusiwi Kugombea, au Kupiga Kura kwenye Chaguzi za Kidemokrasia

(Imetafsiriwa)

Gazeti la ‘The Guardian’ limeripoti mnamo Julai 2, 2024, kuhusu Australia, “Vuguvugu jipya “mashinani” la kisiasa liitwalo Kura ya Muislamu linasema litaunga mkono angalau wagombea watatu binafsi wakidhamiria kuwaondoa mawaziri wa chama cha Labor na washurutishaji serikalini jijini Sydney ya magharibi katika uchaguzi ujao wa serikali ya shirikisho. Kura ya Muislamu - iliyoanzishwa kama jibu la hasira za jamii kwa ushughulikiaji wa chama cha Labor kwa vita vya Gaza – inalenga kuwaunga mkono wagombea katika Watson, Blaxland na Werriwa, msemaji alisema siku ya Jumanne.” https://www.theguardian.com/australia-news/article/2024/jul/02/muslim-vote-political-movement-candidates-labor-federal-election

Ni hakika, kuwa ushiriki wa Muislamu katika Demokrasia ni jambo lenye kuwashughulisha watawala, wanasiasa, wasomi na watungaji sera. Hii ni ima Waislamu wakiwa katika Ulimwengu wa Kiislamu, au wakiishi ughaibuni katika nchi za Magharibi. Hivyo kuna mjadala kuhusu ushiriki wa Muislamu katika Demokrasia nchini Australia, Uingereza na Amerika, kama ulivyo mjadala kuhusu ushiriki wa Waislamu katika uchaguzi nchini Uturuki, Pakistan na Misri. Suala la Muislamu kushiriki uchaguzi limekuwa jambo la kushughulisha zaidi katika miezi ya karibuni, kwa mwanga wa mwitikio wa Waislamu kuelekea Gaza. Waislamu wana hasira na serikali zilizopo na mifumo ya utawala, kwa sababu ya dhulma yao kuhusiana na suala la Gaza.

Kama lilivyo suala jengine lolote maishani, Muislamu hugeukia Dini ya Uislamu anapoamua kusimama kama mwakilishi, au kuchagua mwakilishi. Ili kutoa hukmu ya Kisharia, mwanzo lazima kufahamu uhakika unaohitaji hukmu inayotaka kuvuliwa. Hii hujulikana kama Tahqiq Al-Manat. Uhakika hapa, au Manat, ni bunge au baraza la kutunga sheria katika serikali ya kidemokrasia, ikiwa ni pamoja na maumbile, kazi na nguvu za wanachama wake, ambao ni wawakilishi.

Uhakika wa nchi ya kisekula ni kuwa imeegemea juu ya demokrasia. Imejengwa juu ya fikra ya ubwana kwa watu, kupitia wawakilishi wao. Watu wanaamua kipi kinaruhusiwa, na kipi kinachokatazwa. Kama watu wataruhusu ndoa baina ya wanaume wawili, basi itaruhusiwa na sheria. Kama watu wataharamisha vazi la hijabu, basi sheria itaharamisha. Uhalisia juu ya bunge ni kuwa lina mamlaka ya utungaji sheria. Iinaidhinisha katiba inayotumika katika nchi. Linatunga sheria ambazo ni wajibu juu ya mamlaka za serikali na mamlaka za mahakama. Hii ni pamoja na nguvu nyengine ikiwemo haki ya kutoa, au kuzuia, imani kwa serikali, na haki ya kuchunguza mamlaka ya serikali, na kuiwajibisha kwa jambo lolote inalolitekeleza.

Uhalisia wa Demokrasia ni kuwa unagongana na Uislamu. Katika Uislamu, Mwenyezi Mungu Pekee ndiye Bwana. Yeye (swt) hana ushirika na wanadamu. Ni Yeye pekee anaeamua kipi ni halali au haramu. Pindi Yeye (swt) Alipoharamisha ndoa baina ya wanaume wawili, watu hawawezi kuifanya halali. Pindi Yeye (swt) alipoamrisha uvaaji wa Hijab, watu hawawezi kuikataza. Dalili ya kuhukumu kwa yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) ni kutoka nususi za kisharia, kwa dalili ya kukata na maana ya wazi, kama kwa mfano, Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَـفِرُونَ]

“Na wasiohukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri”. [Surah Al-Ma’idah 5:44]. Abdullah Ibn Abbas (ra) ameelezea, من جحد ما أنزل الله فقد كفر ومن أقر به ولم يحكم فهو ظالم فاسق  “Yeyote anayekataa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu atakuwa amekufuru, na yeyote anayeyakubali yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu lakini hahukumi nayo, huyo ni dhalimu na fasiki [Imepokewa na Ibn Jarir]

Kuna dalili nyingi ambazo ni za kukata na zenye maana ya wazi, zikiwemo,

[وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Ma’ida 5: 49].

[إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ]

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu.” [Surah Yusuf: 40]

[فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجًا مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا]

“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utakayotoa, na wanyenyekee kabisa.” [Surah An-Nisa’ 4:65]

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْمًا لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

“Je! Wao wanataka hukumu za kijahiliya? Na nani aliye mbora zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Surah Al-Ma’ida: 50].

Ama kutoka kwa Sunna Tukufu, tunaona kuwa Mtume (saw) hakushiriki katika nidhamu hiyo, ambapo Mwenyezi Mungu (swt) hakufanywa kuwa Bwana. Makafiri wa Kikureshi walimpatia Mtume (saw) fursa ya kuwatawala kwa mujibu wa sheria zao, na sio Uislamu. Yeye (saw) alikataa. Kutoka kwa Sera ya Ibn Is-haq, “السير والمغازي  As-Siyar Wal Maghazi,” imepokewa kutoka kwa Ikrimah kutoka kwa Ibn Abbas kuwa Utbah na Shaybah mtoto wa Rabia na Abu Sufyan ibn Harb, na Nadr bin al-Harith ndugu wa Bani Abd Ad-Dar, na Aba Al-Bukhturi, ndugu wa Bani Asad, na wengineo… Walikutana, au waliokutana miongoni mwao baada ya kuchwa jua nyuma ya Kaaba, baadhi walisemezana: Muite Muhammad na zungumza naye, na jadiliana naye na fanya naye… Walimwita na kumwambia: Ewe Muhammad, Tumekwita kufanya nawe … Kama utafikia katika mazungumzo haya kutaka fedha, basi tutakukusanyia, ili uwe tajiri zaidi yetu, kama unahitaji utukufu tutakupatia uwe juu yetu, kama unahitaji uongozi tutakufanya uwe kiongozi wetu… Mtume (saw) akasema,

, «ما أدري ما تقولون، ما جئتكم بما جئتكم به لطلب أموالكم، ولا الشرف فيكم، ولا الملك عليكم، ولكن الله بعثني إليكم رسولاً وأنزل علي كتابا، وأمرني أن أكون لكم بشيراً ونذيراً فبلغتكم رسالة ربي، ونصحت لكم فإن تقبلوا مني ما جئتكم به فهو حظكم في الدنيا والآخرة، وإن تردوا علي أصبر لأمر الله حتى يحكم الله بيني وبينكم» “Sikubaliani na kile mnachokisema. Kile nilichokuleteeni sio kwa ajili ya kutaka mali zenu, wala utukufu kwenu, wala uongozi juu yenu. Isipokuwa Mwenyezi Mungu amenileta mimi kuwa ni mjumbe kwenu. Na ameniteremshia kitabu, na ameniamrisha kuwa mwenye kubashiria na muonyaji, na hivyo nimekufikishieni ujumbe wa Mola wangu, na kukupeni nasaha, kama mtayakubali yale niliyokuleteeni, basi itakuwa kwenu vizuri duniani na akhera. Kama mtakataa basi mimi nitasubiri maamuzi ya Mwenyezi Mungu hadi ahukumu baina yangu na nyinyi.” Sawa sawa na kilichosemwa katika “دلائل النبوة لأبي نعيم الأصبهاني   Dala’il An-Nubuwa” ya Abu Na’im Al-Asbahani” na katika “السيرة النبوية لابن كثير  As-Seera An-Nabawiya ya Ibn Kathir” na katika vitabu vyengine vya Sera.

Maquresh pia walimpatia Mtume (saw) ofa ya kugawanya madaraka, baadhi ya muda yawe upande wao na baadhi yawe kwa Mtume (saw). Wakapendekeza kumuabudu Mola wake kwa mwaka mmoja na Yeye Mtume aabudu miungu yao mwaka mmoja. Mtume (saw) akakataa na kutaka Uislamu pekee utawale. Katika Tafsiri ya Al-Qurtubi ya Surat Al-Kafirun:

[قُلْ يَا أَيُّهَا الْكافِرُونَ]

“Sema, Enyi makafiri”, amesema, ذَكَرَ ابْنُ إِسْحَاقَ وَغَيْرُهُ عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّ سَبَبَ نُزُولِهَا أَنَّ الْوَلِيدَ بْنَ الْمُغِيرَةِ، وَالْعَاصَ ابن وَائِلٍ، وَالْأَسْوَدَ بْنَ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأُمَيَّةَ بْنَ خَلَفٍ، لَقُوا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالُوا: يَا مُحَمَّدُ، هَلُمَّ فَلْنَعْبُدْ مَا تَعْبُدُ، وَتَعْبُدُ مَا نَعْبُدُ، وَنَشْتَرِكُ نَحْنُ وَأَنْتَ فِي أَمْرِنَا كُلِّهِ، فَإِنْ كَانَ الَّذِي جِئْتَ بِهِ خَيْرًا مِمَّا بِأَيْدِينَا، كُنَّا قَدْ شَارَكْنَاكَ فِيهِ، وَأَخَذْنَا بِحَظِّنَا مِنْهُ. وَإِنْ كَانَ الَّذِي بِأَيْدِينَا خَيْرًا مِمَّا بِيَدِكَ، كُنْتَ قَدْ شَرِكْتَنَا فِي أَمْرِنَا، وَأَخَذْتَ بِحَظِّكَ مِنْهُ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ قُلْ يَا أَيُّهَا الْكافِرُونَ...“Ibn Ishaq na wengineo kutoka kwa Ibn Abbas amesema: kuwa sababu ya kuteremshwa (Asbab An-Nuzuul) Sura hii, kwamba Al-Walid bin Mughira na Al-Aas ibn Wa’il, na Al-Aswad bin Abdul Muttalib, na Umayyah bin Khalaf walikutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na wakasema: Ewe Muhammad, acha tuabudu kile unachoabudu na uabudu kile tunachoabudu, na tushirikiane baina yetu katika mambo yetu yote. Kama ulichokuja nacho kina kheri kuliko tulichokuja nacho sisi, basi tutashirikiana na wewe katika hilo, na tutachukua sehemu yetu humo. Kama ikiwa kile tulichonacho kina kheri kuliko ulichonacho wewe, basi utashirikiana nasi katika mambo yetu, na utachukua sehemu yako humo. Mwenyezi Mungu (swt) akateremsha [قُلْ يَا أَيُّهَا الْكافِرُونَ] “Sema Enyi makafiri.” [Surah Al-Kafirun: 1].

Kukataa kwa Mtume (saw) kushiriki katika nidhamu zilizo kinyume na Uislamu imeelezwa wazi na Muffassir At-Tabari. Kwa mujibu wa Tafsiri ya At-Tabari, جامع البيان “Jami’ Al-Bayan” ya Surah, [قُلْ يَا أَيُّهَا الْكافِرُونَ] “Sema, Enyi Makafiri.” [Al-Kafiruun: 1], حدثني محمد بن موسى الحَرشي، قال: ثنا أبو خلف، قال: ثنا داود، عن عكرِمة، عن ابن عباس: أن قريشا وعدوا رسول الله صلى الله عليه وسلم... فإنا نعرض عليك خصلة واحدة، فهي لك ولنا فيها صلاح. قال: "ما هي؟" قالوا: تعبد آلهتنا سنة: اللات والعزي، ونعبد إلهك سنة، قال: "حتى أنْظُرَ ما يأْتي مِنْ عِنْدِ رَبّي"، فجاء الوحي من اللوح المحفوظ: [قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ] “Amenihadithia Muhammad Ibn Musa al-Harashi, amesema: Abu Khalaf amesema, Daud amesema, kutoka kwa Ikrimah, kutoka kwa Ibn Abbas: kuwa Maquraysh walimuahidi Mtume (saw) … tunakupatia jambo moja, litakuwa la kwako na itakua bora kwetu. Akasema: ما هي؟  ni lipi hilo?’ Wakasema, Abudu miungu yetu kwa mwaka mmoja: Lat na ‘Uzza, na tutaabudu Mola wako mwaka mmoja. akasema: «حتى أنْظُرَ ما يأْتي مِنْ عِنْدِ رَبّي» “Nitasubiri hadi kije kile atachonishushia Mola wangu,” Wahyi ukashuka kutoka Al-Lawh Al-Mahfudh, [قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ] “Sema, Enyi makafiri” [Al-Kafiruun: 1].

Mwanachuoni maarufu, Ash-Shawkani, pia alitia nguvu juu ya kukataa kwa Mtume (saw) kushiriki katika nidhamu zisizofuata sheria za Uislamu katika tafsiri ya [قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ] “Sema, Enyi makafiri” katika “فتح القدير Fat’h Al-Qadiir” ya Shawkani, أَخْرَجَ ابْنُ جَرِيرٍ وَابْنُ أَبِي حَاتِمٍ وَالطَّبَرَانِيُّ عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: «أَنَّ قُرَيْشًا دَعَتْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ... فَإِنْ لَمْ تَفْعَلْ فَإِنَّا نَعْرِضُ عَلَيْكَ خَصْلَةً وَاحِدَةً وَلَكَ فِيهَا صَلَاحٌ، قَالَ: مَا هِيَ؟ قَالُوا: تَعْبُدُ آلِهَتَنَا سَنَةً وَنَعْبُدُ إِلَهَكَ سَنَةً، قَالَ: حَتَّى أَنْظُرَ مَا يَأْتِينِي مِنْ رَبِّي، فَجَاءَ الْوَحْيُ مِنْ عند الله قُلْ يَا أَيُّهَا الْكافِرُونَ * لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ إِلَى آخِرِ السُّورَةِ، وَأَنْزَلَ اللَّهُ: قُلْ أَفَغَيْرَ اللَّهِ تَأْمُرُونِّي أَعْبُدُ أَيُّهَا الْجاهِلُونَ إِلَى قَوْلِهِ: بَلِ اللَّهَ فَاعْبُدْ وَكُنْ مِنَ الشَّاكِرِينَ...) “Kutoka kwa Ibn Jarir, Ibn Abi Hatim, na At-Tabarani kutoka kwa Ibn Abbas: “kuwa Maqureshi walimwita Mtume (saw)… kama hutotaka, basi tutakupatia jambo moja zuri kwako. Mtume (saw) akasema: «مَا هِيَ؟»  ‘Lipi hilo?’ Wakasema: abudu miungu yetu kwa mwaka mmoja na sisi tutaabudu Mungu wako kwa mwaka mmoja. akasema (saw), «حَتَّى أَنْظُرَ مَا يَأْتِينِي مِنْ رَبِّي» ‘Hadi nione nini kitanijia kutoka kwa Mola wangu.” Wahyi ukashuka kutoka kwa Mwenyezi Mungu:

[قُلْ يَا أَيُّهَا الْكافِرُونَ * لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ]

“Sema: Enyi Makafiri. Siabudu mnachokiabudu” [Surah Al-Kafiruun: 1-2] hadi mwisho wa Sura. Mwenyezi Mungu (swt) ameteremsha:

[قُلْ أَفَغَيْرَ اللَّهِ تَأْمُرُونِّي أَعْبُدُ أَيُّهَا الْجاهِلُونَ]

“Sema, [Ewe Muhammad], “Je, Mnaniamrisha nimuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu, enyi majahili?”. [Surah Az-Zumar: 64] Hadi aya:

[بَلِ اللَّهَ فَاعْبُدْ وَكُنْ مِنَ الشَّاكِرِينَ]

“Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.” [Surah Az-Zumar: 66].”

Dalili za wazi kutoka kwenye Quran Tukufu na Sunna za Mtume (saw) zinakataza moja kwa moja kutohukumu kwa yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Zimekataza ushiriki wote katika hukmu namna hizo. Hakuna anayesimama dhidi ya dalili hizo za wazi isipokuwa wale wasiomtii Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) wazi wazi. Hoja yoyote wanayoileta ni yenye kukataliwa. Kutotii kwao kutawafunika kwa fedheha katika dunia hii, japokuwa adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali zaidi.

Uwakilishi wa kuchaguliwa ni sehemu ya mchakato wa kutunga sheria na hivyo ni kufanya kitendo kilichoharamishwa. Wawakilishi wanawakilisha watu katika kuelezea maoni yao kuhusu utungaji sheria. Katika suala hili, yeye ni mwakilishi wao (mjumbe). Wakati Muislamu anapoingia kwenye bunge anakiri nidhamu hii isiyo ya Kiislamu, inayoweka mamlaka ya ubwana kwa watu, na sio kwa Sharia ya Mwenyezi Mungu (swt), hapo bila shaka huwa ni mtenda dhambi. Hakuna mwenye haki ya kugawanya mamlaka ya utungaji sheria na Mwenyezi Mungu (swt). Hata kama mwakilishi ni mwenye kuchunga ibada za funga na swala, haifanyi hiyo kuwa halali.

Mtu anayeonekana mwema kwa mfano anaposafirisha pombe, hakupunguzi uharamu wa kuisafirisha, kwa kuwa kila anayeisafirisha hufungika na hukmu za Uislamu. Pia, dhambi za yule anayejua kuwa hilo ni haramu ni kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwani (swt) Anasema,

[كَبُرَ مَقْتاً عِندَ اللَّهِ أَن تَقُولُوامَا لَا تَفْعَلُونَ]

“Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyoyatenda” [Surah As-Saff: 3].

Kupiga kura kwa ajili ya kumchagua mwakilishi pia ni tendo la haramu. Mpiga kura atamkabidhi mtu kwa ajili yake kushughulikia mambo ya haramu. Tunapoangalia matendo haya, tunayakuta yote ni haramu kwa sababu yameegemea juu ya uongo, ambao ni kuwapa watu mamlaka ya kutunga sheria badala ya Mwenyezi Mungu (swt). Kama Muislamu anayepiga kura anaelewa kuwa mwakilishi wake atachagua utungaji wa sheria au sheria za kibinadamu, au kupiga kura kwa maslahi yake, basi atakuwa anatenda dhambi. Hii ni mbali ya ukweli kuwa hilo halikubaliki, kiasili, kuwakilisha kwenye jambo lililoharamishwa na Sharia. Kama ilivyo mtu anayeonekana mchamungu akichagua au kuwakilisha mwengine kusafirisha pombe kwa ajili yake, hiyo haitofanya usafirishaji huo kuwa halali, achilia mbali uwakilishi wa jambo hilo la dhambi. Kazi ya wanachama wa baraza la wawakilishi ni haramu kabisa. Hakuna shaka kuwa kupiga kura kwa ajili ya wawakilishi katika chaguzi hizi pia ni haramu. Inawapatia wawakilishi nguvu kwa ajili ya watu na vyama kutenda haramu.

Enyi Waislamu kwa jumla, na Maulamaa na Makhatibu hasa:

Kulingana na dalili za wazi kutoka kwenye Quran Tukufu na Sunna Iliobarikiwa, Waislamu hawaruhusiki kushiriki katika Demokrasia, ima kusimama kama wawakilishi, au kupiga kura kwa ajili ya wawakilishi. Kupinga hili ni kuwa na kiburi dhidi ya haki. Wale wenye kiburi watakaa mbali zaidi na Mtume (saw) Siku ya Kiyama, kutokana na kile Al-Tirmidhi alichokipokea katika Hadith Hassan, kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«وإِنَّ أَبْغَضَكُم إِليَّ وَأَبْعَدَكُم مِنِّي يومَ الْقِيامةِ: الثَّرْثَارُونَ، والمُتَشَدِّقُونَ، وَالمُتَفَيْهِقُونَ»، قالوا: يَا رسول اللَّه، قَدْ عَلِمْنَا الثَّرْثَارُونَ، وَالمُتَشَدِّقُونَ، فَمَا المُتَفَيْهِقُونَ؟ قال: «المُتَكَبِّرونَ» “Hakika, ninayemchukia zaidi miongoni mwenu na atayekuwa mbali nami Siku ya Kiyama ni Thartharun (mwenye majivuno), na Mutashaddiqun (mwenye kubwabwaja sana) na Mutafayhiqun.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tunajua Thartharun, na Mutashaddiqun, lakini nani Mutafayhiqun? Akasema (saw): “Mwenye kiburi”

Lazima tutangaze kukataa kwetu chaguzi za kidemokrasia zinazokwenda kinyume na Sheria za Mola wetu, zinazokataa Utukufu Wake juu ya wanadamu wote. Lazima tuwatake wagombea kutangaza kukataa kwao nidhamu hii ya kidemokrasia, na sheria zake zinazopingana na Uislamu. Kupungua kwa wapiga kura kuna matokeo muhimu ya kisiasa yalio chanya, lililo muhimu zaidi ni kuonyesha uwakilishi dhaifu wa wale wanaochukua madaraka. Kupungua kwa wapigaji kura kunadhoofisha Demorasia fisidifu na kipote cha watawala fisadi. Kupungua kutahakikisha dunia kuwa Waislamu wanakuwa na msimamo dhidi ya ufisadi na dhambi ya sheria za mwanadamu.

Uthabiti wa Waislamu hauji kutokana na ujio wa mwakilishi bungeni, au kwa kutekeleza sheria zilizo haramu. Uthabiti ni kwa kuregea Waislamu kwenye njia ya haki, kwa kujifunga na Uislamu, na kwa kuregesha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume kulingana na njia ya Kisharia iliyoelekezwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Hivyo tusiendelee kuchuma dhambi na kuutupa muda wetu kwa kushiriki katika Demokrasia. Na tushirikiane katika kazi iliyo bora ya kuregesha tena hukmu kwa yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu