Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amerika inaweza kuwa na kesi milioni 1 za Covid-19 ndani ya wiki 2!

Amerika inakabiliwa na janga na imeipiku Ujerumani na Ufaransa ndani ya siku mbili zilizopita kwa kesi za Covid-19, na licha ya Italia kuwa na idadi maradufu ya kesi kama Amerika, mjumuiko wa idadi ya kesi inazidi mara mbili ndani ya kila siku 4 nchini Italia, ilhali inazidi mara mbili ndani ya kila siku nchini Amerika.

Trump aliahidi kwamba ataifanya Amerika kuwa kubwa tena, lakini ndani ya siku kadhaa Amerika itakuwa kubwa kutokana na kesi zaidi zitakazo ripotiwa za Covid-19 kuliko nchi yoyote duniani, na ndani ya wiki mbili kuna uwezekano wa kuwepo kesi takribani milioni 1 nchini Amerika.

Dunia hivi karibuni inaweza ikaviita virusi vya Amerika, lakini Trump aliviita “virusi vya Uchina” kwa sababu “vilikuja kutoka Uchina,” na alizuia usafiri wa anga kutoka Uchina na kuwaambia watu wake walikuwa salama sasa. Kisha vikaanza kuenea zaidi na kusababisha hofu nchini Iran, Italia na nchi nyingine za Ulaya, na kisha Trump akaviita “virusi vya kigeni” na kuwaambia watu wake kwamba wamshukuru kwa kuifunga nchini dhidi ya Uchina. Kisha ikambidi kufunga mipaka ya Amerika kwa Ulaya na kuviita “virusi vya Ulaya.” Alifanya makongamano na wanahabari akiisifu akili yake na kujibu kwake kwa haraka, lakini virusi tayari vilikuwa vinasambaa nchini Amerika. Kulikuwepo na kesi 62 mnamo Machi 1, kisha mamia kisha maelfu. Trump ameviteka na kuvishangaza vyombo vya habari kutokana na kiburi chake na kujitia hamnazo kiasi kwamba hawakufahamu kiuhakika ni kwa kiwango gani janga lilivyo na ni kwa muda gani litawaandama.  Trump aliwaahidi watu wake madawa mnamo Alhamisi na Ijumaa, ilhali wajuzi wake mwenyewe wa matibabu walisema kwamba dawa hizi bado hazijathibitishwa kuwa zafanyakazi, na kunahitajika miezi kadhaa ya kuzijaribu. Madaktari wanalalamikia kwamba hawana glovu na barakoa ndani ya nchi tajiri duniani licha ya tahadhari za kila siku kutoka kwa vitengo vya ujasusi vya Amerika tokea Januari.

Italia, hivi sasa inachukua sehemu ya pili baada ya Uchina, iliiweka nchi yake chini ya udhibiti mkali kuchelewa mno, lakini Amerika imekuwa polepole zaidi. Nchini UK, Waziri Mkuu Boris Johnson alizungumza kavukavu kuhusu kinga ya chini na kuiandaa nchi kwa vifo vya wengi wa “wapendwa wao” huku akichukua hatua za kudhibiti polepole ili asiweze kuwaudhi watu na hivyo UK nayo pia italipa gharama kubwa mno. Ilhali Uchina imevidhibiti virusi kupitia udhibiti wa ukandamizaji wa dola, Korea Kusini ilichapuka na kulithibiti janga mara moja, lakini ukaribu wake na mahusiano yake ya kithaqafa na Uchina inawezekana iliifanya kuwa rahisi kwa Korea kupata uungwaji mkono na watu wake katika matumizi makubwa na uvamizi wa faragha ili kupambana na virusi. Ama kwa viongozi wa mataifa ya kidemokrasia, wamefeli. Ubinafsi na ugumu wa Urasilimali wa Amerika ulifunga milango yake kwa dunia na kuiawachilia mbali wakati wa hitajio, na haikujaribu kuchokoza hasira ya watu wake kwa kuwawekea vikwazo katika uhuru wao ili kupambana na virusi na hivi sasa imepoteza.

Wabunge wa Amerika walijua hatari iliyokuwa inakuja lakini wakauza mamilioni ya dola ya hifadhi na hisa zao binafsi kabla soko la hisa la Amerika kuanguka chini kabisa kihistoria. Walipokea ushauri kutoka kwa Kamati ya Seneti kuhusiana na hatari ya Covid-19 lakini wakaiambia nchi kwamba kila kitu kiko chini ya udhibiti ilhali sio hivyo. The New York Times ilisema kuhusiana na wabunge waoga jana, “Wangelileta mabadiliko, lakini walitia faida!” Urasilimali na demokrasia zinawafelisha watu wa Amerika ambao wanaviziwa na tishio la umasikini na ukosefu wa makaazi na kuchezewa shere kwa ahadi za utajiri ambao ni wachache tu wanaoweza kuupata. Urasilimali unawapatiliza nayo demokrasia inawalaza katika matamanio yao pasi na kuzingatia gharama yake, na ni kwa uchache kilicho andaliwa mapema ili kuwalinda kutokamana na kile kinachoitwa virusi vya Uchina.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 26 Machi 2020 06:29

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu