- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Lini Janga la Virusi vya Korona Litakwisha?
Wanaadamu kupitia historia yao ndefu, wamekumbana na maambukizi mengi ambayo yameathiri afya zao na maendeleo yao, kitarakimu au kivitendo, kutokana na kuenea kwa haraka kwa maambukizi haya na udharura wake kwa namna ya ghafla na ya kasi, kiasi kuwa watu hawapati fursa ya kuyazuia na kuyaondoa isipokuwa baada ya kupotea kwa maelfu ya roho, na baada ya kusababisha zahama na usumbufu katika jamii. Kama tutaichunguza historia ya maambukizi kwa upande wa muda na mahala, tungeweza kuona kuwa mataifa hayakuwa huru kutokana na udharura na kuenea, kama tauni, ikiwemo tauni nyeusi na homa ya mafua ya aina zote, hasa mafua ya Uhispania (Spanish flu), ambayo yaligharimu maisha ya watu milioni 75 kote duniani, kipindupindu, Ebola, SARS, nk. hadi kwenye virusi vya Korona…
Huenda kuendelea kwa virusi vya Korona kuvamia nchi za ulimwengu, na kushindwa kukabiliana navyo au kugundua chanjo ya kuvizuia, licha ya jitihada za kasi kuvipunguza, na licha ya hatua kali za serikali kudhibiti ueneaji wake, pamoja na kushindwa kwa nchi nyingi kama Italia, Uhispania, Ufaransa na Amerika mbele ya maambukizi haya yasiyoonekana kwa macho, na kusalim amri kwa nchi nyengine kuwa ni tamko la kuonyesha kushindwa kuvikabili, pamoja na udhaifu wa mifumo ya tiba uliofichuka hata kwa kiwango cha nchi zilizoendelea, yote haya yamezusha masuali mengi kwenye akili za watu: Lini janga la virusi vya Korona litaisha? Na ni lini watu watarejea katika maisha yao ya kawaida?
Kwa sababu maambukizi haya bado yanatibuka kwa mujibu wa taarifa rasmi za mambo ya tiba, na yanaendelea kuenea na yanagharimu zaidi wahanga wake, na inawatesa Waislamu na Makafiri mashariki na magharibi ya dunia, lakini tofauti ni katika namna inavyo angaliwa kama ni mateso, ambayo Muislamu huamini, katika aqida yake, ambaye huamini kuwa Mola wake atakuwa mwema kwake (kuwa Mola wake atamlipa na kumkubalia matendo yake), na huwa anaongozwa kwa uoni huu kwa tabia nzuri, kwa utambuzi na kwa matendo ili kulishinda janga hili kwa njia nzuri, isio na kuchanganyikiwa, kuvunjika moyo, wasi wasi na hofu ambayo Wamagharibi inawapata, wanaohesabu kila mshindo kuwa uko juu yao.
Kabla hatujauliza ni lini janga la virusi vya Korona litaisha? Ni lazima kwanza; tusite katika nukta muhimu; nayo ni kuwa maambukizi kawaida humalizika, huwa hayabakii na hayadumu, na janga hili litakwisha kama yalivyo kwisha majanga mengine mengi, kwa idhini ya Mola wao, kwa sababu hakuna cha kudumu katika ulimwengu, na kila kitu kina mwanzo na mwisho ambao Mwenyezi Mungu ameupangia kwa kitu hicho. Historia ni ushahidi bora wa hilo kama tulivyo taja mwanzoni kuwa maambukizi yameyakumba mataifa mengi kabla yetu, lakini yalimalizika.
Akili ya Muislamu anaye amini ukomo wa ulimwengu huu, maisha haya, na mambo yote yanayompata, yanamfanya kuwa na uhakika ya kuwa kila kitu kina mwisho na kuwa maambukizi ni kudura ya Mwenyezi Mungu (swt) itampata yule anayemtaka Yeye katika waja wake.
Kwa upande mwengine, mwisho wa janga la virusi vya Korona hutegemea juu ya kugunduliwa kwa kinga ya virusi. Kama ilivyo kwa maambukizi mengine, inaweza kuchukua muda, lakini siku itafika itatangazwa, na haya yamehakikishwa na Hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Katika Sahih Bukhari, kutoka katika Hadith kwa njia ya Abu Huraira kuwa Mtume (saw) amesema:
« مَا أَنْزَلَ اللَّهُ دَاءً إِلَّا أَنْزَلَ لَهُ شِفَاءً »
“Mwenyezi Mungu hajateremsha maradhi isipokuwa ameteremsha na ponyo yake.”
Katika Sahih Muslim kutoka kwa Hadith ya Jabir ibn Abd Allah, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
« لِكُلِّ دَاءٍ دَوَاءٌ فَإِذَا أَصَابَ دَوَاءُ الدَّاءِ بَرَأَ بِإِذْنِ اللَّهِ »
“Kuna dawa kwa kila maradhi, na dawa ikisibu maradhi, hutibu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”.
Na katika Musnad ya Imam Ahmad kutoka kwa Hadithi ya Usama bin Sharik kutoka kwa Mtume (saw) kuwa amesema:
« إِنَّ اللَّهَ لَمْ يُنْزِلْ دَاءً إِلَّا أَنْزَلَ لَهُ شِفَاءً، عَلِمَهُ مَنْ عَلِمَهُ وَجَهِلَهُ مَنْ جَهِلَهُ »
“Hakika Mwenyezi Mungu hajateremsha maradhi yoyote isipokuwa ameteremsha ponyo, hutambuliwa na mwenye kuitambua na hukosa kutambuliwa asiyeitambua”.
Pili, imani ya kuwa mema na mabaya ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) huongeza utulivu wa mja muumini na pozo wakati wa dhiki na majanga, kwa sababu fikra ya Qadhaa na Qadar huondosha hofu na huzuni kwa watu. Na tukumbuke vyema nasaha za Mtume wetu (saw) kwa Ibn Abbas ikiwa ni nasaha kwa Ummah wote:
« أَنَّ مَا أَصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَأَنَّ مَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبَكَ »
“Na tambua kuwa lile lililokufika, halikuwa ni lenye kukukosa, na lile lililokukosa, halikuwa ni lenye kukufika”.
Ikiwa Mwenyezi Mungu ameamua tuathirike na maambukizi haya, hakuna ngome au minara itakayotuzuia kutokana nayo, na kile kilichotokea leo duniani kinatufanya tutambue udhaifu wa mwanaadamu mbele ya Qadari ya Mwenyezi Mungu (swt), na kuwa pesa zao, silaha, maarifa, au mamlaka hayakuwalinda kutokana nayo! Hili pekee linatosha kufanya tutambue ukubwa wa Mwenyezi Mungu na udhaifu wa wanaadamu, hivyo tunamthamini Yeye kwa thamani Yake ya kweli, na kuamini ahadi Zake na kumtukuza Yeye (swt).
Tatu, namna ya kushughulikia maambukizi haya:
Moja ya mambo muhimu zaidi ya kufanya kwa mja muumini katika hali hii ni kuchukua hadhari za kutosha, kushikamana na maelekezo na miongozo, na kujielimisha mwenyewe na watu waliomzunguka kuhusu namna ya vipi kushughulikia maambukizi kama haya kwa uelewa na kwa matendo. Zaidi ya tahadhari za kimatendo kwa vifaa, hatutoachana na dua; ni moja ya tiba bora kabisa; ni adui wa maafa; inayafukuza, kuyatibu, inalinda, inaondosha au kupunguza maafa, na ni silaha ya muumini.
Al-Hakim amepokea katika Sahih yake Hadith ya Aisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) amesema:
«لَا يُغْنِي حَذَرٌ مِنْ قَدَرٍ، وَالدُّعَاءُ يَنْفَعُ مِمَّا نَزَلَ وَمِمَّا لَمْ يَنْزِلْ، وَإِنَّ الْبَلَاءَ لَيَنْزِلُ فَيَلْقَاهُ الدُّعَاءُ فَيَعْتَلِجَانِ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ»
“Hadhari hainufaishi kutokana na Qadar, na dua inanufaisha kutokana na kile kilichoteremshwa na kile kisichoteremshwa, na balaa huteremka na ikakutana na dua na kupambana hadi Siku ya Kiyama”
Moja ya matendo muhimu ambayo Muislamu hutenda wakati yanapotokea maambukizi na magonjwa ni uwajibikaji!
Kwa hili nakusudia kuziwajibisha serikali zenye kuwadhikisha watu katika nchi za Waislamu; zile zenye kuongeza kuwadhalilisha watu wake katika hali nzito. Hawazifanyi bora huduma za afya, sio kwa vifaa wala si kwa kujenga uelewa, na kuwaburuza katika kufuata sera za nchi za Wamagharibi, kwa kuweka karantini kamili na kutenga kikamilifu licha ya hali na mazingira tofauti. Hivyo maamuzi yasio imara ya serikali yamekuwa ni sababu ya kulitanua janga kwa watu, kwa kusitisha maisha ya kiuchumi na kuwafungia watu majumbani, na juu ya hayo, kutoweza kushughulikia maslahi na riziki na kuwapatia mahitaji muhimu ya msingi ya maisha yao! Kwa upande mwengine, tunakuta serikali hizi zinakimbilia kuvuruga sheria za Uislamu, kama kuswali misikitini, Hajj na Umrah, juu ya muktadha wa kuepusha mikusanyiko, hadi kunakoweza kupelekea kutolewa Fatwa ya kuvunja saumu kwa sababu ya virusi vya Korona, au kushindwa kuangaliwa muandamo wa mwezi kwa kujifunga na sheria za karantini!
Kumekuwa na jitihada katika kuzuia hukumu za Sheria na kuzielekeza moja kwa moja kwa baadhi ya serikali za Kiarabu ambazo zimehodhi suala hili la maambukizi katika kuzidi kuwabana Waislamu kutokana na majukumu yao ya Kisharia, na baadaye, tunashuhudia bidii yao katika kuchelewa kuwapatia wananchi huduma za afya na mahitaji yao ya kimaisha.
Jukumu la mja Muislamu katika hali hii, na hasa mbebaji Dawah, ni kuwawajibisha watawala hawa kwa kudharau maisha ya watu, maslahi na mahitaji yao muhimu ya maisha, hasa kwa kuwa virusi vya Korona vimefichua sera zao fisidifu, na vimefichua wazi ulegevu wa mifumo ya afya na taasisi zinazoitegemea, licha ya madaktari na wauguzi, wahandisi na wengineo kibinafsi kutia juhudi bila kuchoka. Lakini hivi sasa tunahisi zaidi ya wakati mwengine hitajio letu kwa serikali halisi ambayo itahifadhi maisha ya watu na kulinda maslahi yao na mahitaji yao na kuchunga mambo yao na kufanya kila juhudi katika kushughulikia maafa kama haya, na kushughulikia kikweli majanga ya kiuchumi na kiafya na kuwa wa kwanza katika kutoa tiba na kinga, na sio kusubiri Wamagharibi kuitoa na kudhalilisha (kama alivyo shauri daktari wa Kifaransa, kujaribu kinga ya virusi vya Korona kwa Waafrika, kama walivyo fanya uchunguzi kwa maradhi ya AIDS).
Hitajio letu katika mazingira kama haya ni kuregea kwenye sheria za Mola wetu kwa kusimamisha serikali imara na yenye heshima, ambapo mtawala atakuwa ni mtumishi wa Dini yake na Ummah, atauhifadhi Uislamu na Waislamu, na atamuhofia Mwenyezi Mungu na kuwa na huruma juu yetu. Haya ni matendo yanayo inua hadhi ya mja na kumfanya awe karibu na Mola wake, hivyo muumini atapata heshima ya dunia hii na rehema za Akhera.
Ama kuhusu lini virusi vya Korona vitaisha? Muislamu ajiweke sawa katika ufahamu kwa maambukizi haya kuwa ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kukubali Qadhaa ya Mwenyezi Mungu kwa kuridhia na kuwa na tulizo bila kunun’gunika au kuwa na wasi wasi, na kuwa mtulivu, kukinai na kusubiri malipo. Kujiweka sawa kwa uelewa juu ya maambukizi huupunguza mzigo wake na watu watasita kuuliza suali hili, kwa sababu maafa ni uhalisia ambao umeshikana na uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
Na tulenge juu ya kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) ametukabidhi sisi kazi ya kufukuza maambukizi haya; ya watu binafsi, matendo ya kiroho au kisiasa, hasa kwa kuwa sisi tuko katika mwezi mtukufu, mwezi wa rehema na wema. Na tuitumie fursa hii katika mwezi wa Taqwa kwa kufanya matendo ya kutuinua na yalio bora, ambayo ni kusimamisha Sharia za Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu katika dunia Yake, ili tuweze kupata mazuri ya dunia hii na Akhera.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Nisreen Buzhafiri
#Covid19 #Korona كورونا#