- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Maafa Yanayowakumba Ummah ni Mabaya Mara Nyingi Zaidi kwa Wanaadamu Wengine
Mwanaadamu ni kiumbe, cha kibinafsi na pia ni kiumbe cha kijamii, kiasi cha kuwa balaa la kibinafsi na la kijamii humuathiri. Quran inaeleza kuwa mwanaadamu atatahiniwa na majanga kama uzee, maumivu, kiu, njaa, machofu, hofu, kupotea kwa mali, maisha na vitu. Kuna kuwepo pia maafa katika Dini, nayo ni kuwacha njia ya Dini na kuvunja amri za Mwenyezi Mungu na mipaka. Kwa mfano, kuyumba katika masuala ya imani ni balaa kubwa katika Dini. Kutotekeleza swala, kutokufunga, riba, kusengenya na kudanganya yote ni balaa katika Dini. Hadi hapa, yote hiyo ni mifano ya maafa katika kiwango cha kibinafsi. Pamoja na haya, kuna maafa katika kiwango cha kijamii, ambayo humuathiri kila mtu katika jamii, wale waliofeli na wale wasio na hatia, kwa namna ile ile. Fikra yoyote inayodhuru kiini cha Uislamu, ambayo inawavuta watu nje ya Uislamu ni maafa. Wanazuoni, wanaoshindwa kuzungumza haki; watawala, wasiotawala kwa Uislamu, ni maafa. Kutotekeleza Uislamu kimfumo, makafiri kuwa na nguvu na satwa juu ya Waislamu, huku wakipiga marufuku mfumo wa Kiislamu na kuufanya historia, yote ni katika maafa. Kutofahamu maafa haya, au kufahamu bila kuyakanusha, ni aina ya
[وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ]
“Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu.” (Ash-Shuraa: 30)
Maafa katika kiwango cha kijamii daima yamepelekwa kwa mataifa kutokana na madhambi yao, uasi wao; kwa kukanusha, na kuwadhulumu Mitume wao na wale wanaowaunga mkono Mitume. Aina hii ya maafa muda wote imepelekea katika maangamizi ya taifa hilo. Mataifa ya Nuh, Thamud, Lut, ikiwa ni onyo na somo kwa wanaadamu.
Virusi vya Korona vya leo huweza kuonekana kama ni onyo, mtihani au hata adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt). Hivyo, kirusi, ambacho kinaleta magonjwa au kifo kwa mtu binafsi, ni maafa kwa mtu binafsi. Kwa upande mwengine, hatua zisizofaa na maamuzi mabaya kama kuwafungia watu yanayo chukuliwa na serikali kutokana na virusi hivi, ambayo yanawasukuma watu na jamii katika ugumu wa maisha na kuvuruga akili za watu na jamii pamoja, ni maafa ya kiwango cha kijamii. Swala za pamoja (katika kila dini), kuhudhuria mazishi, kuzuru wagonjwa, kukusanyika kwa ajili ya uzawa wa mtoto na harusi ni mahitaji yenye umuhimu, ni ya lazima kwa kila jamii. Kuwanyima watu haya ni maafa ya upande wa kijamii, ambayo yanawakumba sio tu Ummah lakini pia wanaadamu wote.
Tunashuhudia kuwa madhara yaliotarajiwa ya COVID-19 kwa kiasi kikubwa hayajafikia madhara yaletwayo na serikali zisizo na huruma na za kipumbavu, zinazotumia virusi kwa mipango yao wenyewe. Kiwango cha vifo hakijawa kikubwa kama walivyokadiria, na hospitali hazikuzidi uwezo wake. Idadi ya walio athiriwa na virusi ni kubwa zaidi kwa mamia ya idadi ya waliopata ugonjwa. Idadi ya vifo ni fungu la elfu tu ya idadi iliotarajiwa. Hivyo, maafa halisi yameongezwa na kukuzwa kwa kasi ya kikatili kwa wanaadamu na nguvu za wakoloni mabepari kote duniani. Kwa usahihi zaidi, maafa ya kikweli ni wanaadamu kunyimwa mfumo wa uadilifu, huruma na baraka wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Japokuwa Waislamu wanaihisi misiba hii zaidi ya wanaadamu wengine, kwao ni mitihani tu, ambayo hupelekea mafanikio katika dunia hii na Akhera. Hata hivyo, athari ya maafa haya itabaki juu ya makafiri hapa duniani na Akhera. Hivyo maafa yanayo wakumba Waislamu, kwa wanaadamu wengine ni mabaya kwa mara nyingi zaidi. Mwanachuoni mkubwa Ibn Qayyim Al-Jawziyya amesema, “Msiba juu ya Muumini, ni mwepesi zaidi kuliko msiba juu ya kafiri”.
Kwa zaidi ya karne moja sasa, Waislamu na wanaadamu wote, wanahangaika wakiwa chini ya unyonyaji, vita, uvamizi na aina zote za dhulma na mabalaa yanayo wakumba kutoka kwa dola za kikafiri za kikoloni, kwa sababu tu Ummah wa Kiislamu umepoteza ngao ya kujihifadhi wenyewe na walimwengu dhidi ya aina zote za maafa. Kuvunjwa kwa Khilafah katika mgongo wa sayari hii ni maafa makubwa zaidi kwa wote, Ummah na wanaadamu wengine. Ni kutokana na haya, Ummah wa Kiislamu, (ambao ni) mwenge wa walimwengu, hauwezi kujihifadhi wenyewe na wanaadamu kutokana na kiza. Kwa hakika, Mtume (saw) ametujulisha sisi kuhusu kuja kwa masiku haya:
«لَيُنْقَضَنَّ عُرَى الْإِسْلَامِ عُرْوَةً عُرْوَةً فَكُلَّمَا انْتَقَضَتْ عُرْوَةٌ تَشَبَّثَ النَّاسُ بِالَّتِي تَلِيهَا وَأَوَّلُهُنَّ نَقْضًا الْحُكْمُ وَآخِرُهُنَّ الصَّلَاةُ»
“Mafundo ya Uislamu yatafumuliwa moja baada ya moja, kila linapofunguliwa fundo moja watu watashikilia lile linalofuatia, la mwanzo kufumuliwa ni utawala na la mwisho wao ni swala.” (Hakim, Ahmad)
Kwa hiyo fundo la mwanzo, nidhamu yetu ya kisiasa limeshafumuliwa, likiiacha Dini yetu na sisi, wanajumuiya wake, bila ya ulinzi, ikitupora Khalifah wetu, ngao yetu. Zaidi ya hayo, muda wote katika miezi michache iliopita, tumeporwa swala zetu kwa kisingizio cha kirusi kidogo… Bila shaka, tunaendeleza swala zetu za mtu mmoja mmoja, lakini tumekosa swala za jamaa, swala zetu katika muundo wa mujtamaa mzima wa Waislamu! Wametupora swala zetu Ijumaa, swala za Taraweh na swala za Idd!!!
Imam Ghazali (rh) amesema katika kitabu chake, Al-Iqtisad Fi’l-Itiqad: “Dini na Dola ni mapacha. Hivyo dini ni msingi na mtawala ni mlinzi: kile ambacho hakina msingi huvunjika na kile ambacho hakina mlinzi hupotea.” Hii inamaana kuwa wakati wowote pindi dini ya Uislamu na utawala wa Uislamu vinapotenganishwa, Ummah wa Kiislamu na wanaadamu wote, wanabaki bila ulinzi na kuwa katika mazingira magumu. Kwa hakika, ni wazi kwa kila Muislamu mwenye akili timamu na wasio Waislamu hivi leo kuwa kipote cha watandawazi hutaka kupunguza idadi ya watu duniani. Kote katika ulimwengu wa nchi tajiri za kirasilimali zikiwemo Amerika, Uingereza, Ujerumani na nchi nyingi nyengine za Ulaya watu wanalalamika dhidi ya kunyimwa uhuru wao, demokrasia na hata katiba, ambavyo walifanywa waviamini hadi leo. Hata hivyo, malalamiko yao yananyamazishwa na polisi. Machafuko haya, ambayo yanaongezeka kote duniani, hayaonyeshwi au yanaonyeshwa kwa namna ya kupotoshwa na vyombo vikuu vya habari, ambavyo ni ala za serikali zinazotawala.
Kitendo na mwitiko wa mtu binafsi kwa maafa ni katika namna ya kumuomba Mola wake kwa dua na swala, na kuonyesha subira, kwa kuwa hivi ndivyo Mola wetu anatutaka tufanye:
[يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَعِينُوا۟ بِٱلصَّبْرِ وَٱلصَّلَوٰةِ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ]
“Enyi mlio amini! takeni msaada kwa subira na swala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.” (Al-Baqara: 153)
Lakini hili sio tendo la kijamii na mwitiko kwa maafa! Subira, dua na kuomba kwa jamii viko katika muundo wa “kuamrisha mema na kukataza maovu” kwa watawala. Subira (kwa upande wa) jamii ni kuwalingania watawala kukataa mifumo ya kikafiri na badala yake kutawala kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu! Mwitiko wa jamii kwa maafa ni kupitia kufanya bidii kubadilisha kile ambacho kina madhara na kinacho sababisha dosari ndani yake chenyewe. Mapambano haya ni faradhi juu ya mujtamaa wa Waislamu na ndio taji la faradhi zote! Pindi Mwenyezi Mungu (swt) anaposema katika Sura Ar-Ra’d 11,
[إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ]
“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.”
Yeye (swt) ameitaka jamii ya Waislamu kujibadilisha yenyewe. Hivyo, maadamu mujtamaa wa Waislamu haujaondoa sababu za machafuko ndani yake yenyewe, Mwenyezi Mungu (swt) hatoondoa maafa kwake, na hautoweza kuwa muokozi wa wanaadamu.
Enyi Waislamu! Ni Uislamu, ambao utafukuza aina zote za maafa! Ni Uislamu, ambao unatibu aina zote za maradhi, na kumaliza mauwaji, uvamizi, ufukara, kutojiweza, uoga, upweke, ulegevu, uhaini nk.! Ummah huu unabeba maagizo pamoja na dawa dhidi ya uchoyo na watawala wasio na huruma ambao wanatumikia maslahi ya kipote cha mabepari! Uislamu ndio nguvu pekee, ndio mkono pekee, ndio ngumi pekee iwezayo kuwaokoa wanaadamu kutokana na fumbato la ujinga na ukafiri!
[ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُمْتَرِينَ]
“Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanaofanya shaka” (Al-Baqara: 147)
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zehra Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
#FromAffliction2Success #MihnettenKurtuluşa محن_ومنح#
#Covid19 #Korona كورونا#