Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Maoni ya Habari 24/07/2024
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.
Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi saba, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya elfu 130, wanaume na wanawake hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki inaandaa amali kubwa za halaiki kote nchini Uturuki kuwataka Waislamu waungane chini ya bendera ya Khalifa mmoja ambaye atakusanya mara moja majeshi ya kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina).
Matembezi ya 41 mfululizo tangu kuanza kwa Vita vya Kingunga cha Al-Aqsa yalifanyika mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu Tunis, ambayo yaliitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, watu wa Zaytouna na kichwa chake kilikuwa “Njia ya kuikomboa wa Palestina... maandamano ya Umma na kupinduliwa kwa Mafirauni wa zama hizi!”
Ushiriki wa Hizb ut Tahrir/Austria katika amali za kampeni ya kilimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yenye kichwa “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”
Licha ya mateso tunayoyapata kutokana na yale yanayowapata ndugu zetu wa Gaza na madhehebu ya Mayahudi ambao wamekuwa wabaya kwa muda mrefu, dhalimu wa Uzbekistan anajitokeza dhidi yetu kwa kuwakamata mashababu wa Hizb ut Tahrir na kuwatishia kwa vitendo vya ukandamizaji ni yale yale waliyoshtakiwa kwayo na Karimov aliyekufa, na ambayo walifungwa kwa karibu miaka ishirini, mashtaka ya kubuni ambayo hayana ushahidi.
Ushiriki wa Hizb ut Tahrir/Uswidi katika amali za kampeni ya kilimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yenye kichwa “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”
Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 mwaka huu kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov, ambayo kwayo walitumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 - 2000 M.
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 99 ya kuuawa shahidi Sheikh Said Biran al-Kurdi, Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa kongamano lililopewa kichwa la “Urithi wa Sheikh Said” katika ukumbi wa mikutano wa Msikiti wa Salah al-Din al-Ayyubi mjini Diyarbakir.
Katika siku ya nane ya Dhu al-Hijjah (Siku ya Tarwiyah), Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Tunisia iliadhimisha Sunnah ya Takbira katika mji mkuu, Tunis, kwa kuandaa matembezi makubwa yenye kichwa “Matembezi ya Takbira kutoka Tunisia hadi Palestina.”
Hizb ut Tahrir / Tanzania ilifanya visimamo baada ya swala ya Ijumaa (7 Juni 2024) katika sehemu mbalimbali kukemea ukatili wa umbile la Kiyahudi na kuwasilisha suluhisho la Kiislamu juu yake.