Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Ombi kutoka Al-Aqsa kwa Ummah na Majeshi Yake katika Kumbukumbu ya Miaka 101 ya Kuvunjwa kwa Khilafah

Baada ya Swala ya Ijumaa mnamo tarehe 4/3/2022, katika halaiki ya waumini, na katika kuhitimisha amali zake za kukumbuka miaka 101 ya kuvunjwa Khilafah, Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina ilitoa ombi kutoka kwa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa kwa Ummah na majeshi yake, ikiwalingania kuharakisha kusimamisha Khilafah na kuwanusuru wabebaji dawah yake.

Katika kalima iliyotolewa na Dkt. Musab Abu Arqoub, Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb katika Ardhi Iliyobarikiwa, Hizb inaona kwamba Umma leo, bali wanadamu, wana hitaji pakubwa pambazuko la Dola ya Khilafah.

Hizb imesisitiza kuwa, Umma ungali unapitia maafa ya kuvunjwa kwa Khilafah nchini Palestina, ash-Sham, Iraq, Afghanistan, India, Myanmar na maeneo yote duniani.

Hizb ilisisitiza kuwa ulimwengu leo unahitaji nguvu mpya ya kimataifa ili kuung'oa mfumo huu wa kihalifu. Unahitaji Uislamu na Dola ya Khilafah ili kuuokoa na uhalifu wa nchi kubwa - Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na China - kwani jinai zao dhidi ya wanadamu ni za aibu, na dola ya Khilafah ndio mkombozi wa wanadamu na itabadilisha mahusiano kimataifa na kuyaregesha tena, na ndio kimbilio la wanyonge ulimwengu mzima.

Umati ulinadi Khilafah, ukiotoa wito kwa majeshi ya Ummah kutoa nusra, kuhamasika, na kuzing'oa tawala.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Sehemu ya Amali

#أقيموا_الخلافة

#الخلافة_101

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

#TurudisheniKhilafah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu