- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Uholanzi:
Matembezi Jijini Amsterdam “Harakati kwa ajili ya Gaza!”
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 17, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa wanaume na wanawake wa Kiislamu zaidi ya 170,000 hadi sasa. Kufuatia umbile halifu la Kiyahudi kukiuka makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano alfajiri ya Jumanne, Machi 18, 2025, na kuanza tena mauaji ya kimpangilio ya Waislamu wasio na ulinzi, ambao wengi wao ni wanawake, watoto, na wazee, Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa matembezi na kisimamo cha halaiki katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kwa kichwa:
“Harakati kwa ajili ya Gaza!”
Nukta za matembezi na kisimamo zitakuwa:
Kuwajibisha wanazuoni, wenye ushawishi na taasisi kuchukua hatua za pamoja za kuyashinikiza majeshi katika nchi za Kiislamu na kuyataka yachukue hatua ili kuikomboa ardhi iliyobarikiwa (Palestina), ambayo ni wajibu wao wa kidini na wala haipaswi kupuuzwa.
Kuvunja mipaka ya kitaifa, kwani suala la ardhi iliyobarikiwa (Palestina) ni suala la Kiislamu, si la kitaifa, na kudhihirisha uhalisia wa mipaka bandia tuliyowekewa na mkoloni kafiri ili kutubakisha wanyonge.
Hakuna udhuru kwa watawala na viongozi katika nchi za Kiislamu. Hakuna utetezi kwao. Badala yake, lazima wawe na wajibu wa kukata uhusiano wao na Marekani na umbile la Kiyahudi, iwe uhusiano huo ni wa kisiasa, kiuchumi, au kijeshi.
Suluhisho liko kwetu sisi kama Umma mmoja la Kiislamu. Hatuwezi kutarajia haki na usawa kutoka kwa taasisi za kimataifa zilizounda umbile hili hapo awali. Hatupaswi kudanganywa na masuluhisho ya uwongo.
Umma lazima ufahamishwe nukta hizi, na kwamba hakuna suluhisho kwa masuala ya Umma isipokuwa suluhisho lililofaradhishwa na Uislamu.
Basi kuweni pamoja nasi...
Jumapili, 07 Shawwal 1446 H sawia na 06 Aprili 2025 M
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#ArmiesToAqsa
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#Aqsa_calls_armies
#AqsaCallsArmies
Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi
Facebook: Hizb ut Tahrir / Uholanzi
Twitter: Hizb ut Tahrir / Uholanzi
Instagram: Hizb ut Tahrir / Uholanzi