Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Kongamano la Kiuchumi Mjini Diyarbakir Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi

Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa kongamano la kiuchumi katika Ukumbi wa Mikutano wa Mir Yildiz huko Diyarbakir kwa anwani "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi!" Sambamba na mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 wa Hijria ya kuvunjwa Dola ya Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu 1342 H.

Kwa neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, watu wa mji wa Diyarbakir walionyesha hamu sana na mfululizo wa makongamano yaliyofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Masuluhisho ya Kiislamu kwa Migogoro ya Kiuchumi"ambapo walimiminika kwenye ukumbi wa mkutano hadi pomoni.

Kongamano lilianza kazi yake chini ya uenyekiti wa Saadallah Tukinmiz, kwa usomaji mzuri wa aya za Quran Tukufu ikifuatiwa na hotuba ya ufunguzi kwa Kikurdi na mwandishi wa jarida la Kokludegisim, Burhan Erkan, ikifuatiwa na hotuba ya Dkt Abdul Rahim Shin yenye kichwa "masuluhisho ya Kiislamu ya migogoro ya kiuchumi", ambapo alijadili kupitia mifano halisi aliyoitoa akilini kutoka karne 13 za Historia ya Kiislamu kwamba nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu ndio nidhamu sahihi zaidi na yenye mafanikio makubwa kabisa, na akadhihirisha, kwa kutaja mifano ya kitakwimu na mifano ya rai jumla, kwamba mhusika pekee wa mgogoro wa kiuchumi unaoisibu dunia hii leo na unaoisumbua Uturuki kwa sasa ni mfumo wa uchumi wa kibepari, na khiyana ya viongozi wa serikali kwa hazina ya serikali. Shin alisema kwamba hata kama matajiri wangetoa zakat kwa idadi pekee, wangeokoa watu kutoka kwa taabu, na hili ndilo jukumu la dola yenyewe. Alisimulia jinsi Dola ya Kiislamu ilivyotangaza vita dhidi ya wale waliokataa kutoa zaka katika zama za Khilafah ya Abu Bakr, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi.

Baada ya hotuba ya Dkt. Abdul Rahim Shin, Ustadh Abdullah Imamoglu, mwandishi wa kitabu “Sunnah ni Chimbuko la Maisha katika Uislamu na Elimu ya Siasa ya Muislamu,” aliwasilisha hotuba yenye kichwa “Kutabikishwa kwa Nidhamu ya Kiuchumi ya Kiislamu” ambapo alitaja riwaya fupi kutoka katika historia ya Uislamu uliotawala kwa muda wa karne 13, zikionyesha kwamba Uislamu una nidhamu yake ya kiuchumi na ilitabikishwa chini ya utawala wa Khilafah, na kwamba maadili na uaminifu ndivyo vilivyotawala katika jamii ya Kiislamu, hivyo wakajiepusha kutokana na kugusa hata uzi wa hazina. Baada ya mifano hiyo, Imamoglu aliregea hadi siku za leo na kueleza jinsi watawala waliotabikisha mfumo wa kisekula wa kirasilimali walivyopora hazina ya serikali bila ya kumuogopa Mwenyezi Mungu, alidhihirisha wazi tofauti kati ya ubepari wa kisekula na mfumo wa Uislamu.

Katika makongamano na mazungumzo yetu tuliyoyaandaa ndani ya wigo wa kampeni yetu kwa anwani "Masuluhisho ya Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi," ambayo yalidumu takriban miezi miwili, tumejaribu kufafanua tofauti kati ya haki na batili kwenye kila jukwaa, na kwamba chanzo kikuu cha tatizo ni mfumo wa kisekula wa kirasilimali, na suluhisho msingi ni Uislamu na nidhamu yake ya kiuchumi.

Kongamano hili lilihitimishwa kwa kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) aharakishe kusimama kwa Dola ya Khilafah Rashida, itakayotabikisha mfumo huu upya.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Jumapili, 26 Rajab Tukufu 1443 H – 27 Februari 2022 M

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu