Msimamo Unaokinzana wa Indonesia juu ya umbile la Kiyahudi: Maneno Makali Lakini Ingali Inadumisha Mahusiano Mazuri
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Indonesia imeyataka mataifa ya Kiislamu na Kiarabu kukata uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na ‘Israel’ ili kukomesha ghasia mjini Gaza. Katika kikao cha Riyadh cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na OIC, Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje Anis Matta alisisitiza ulazima wa kukata vitega uchumi vinavyohusiana na taasisi za Kizayuni na kuimarisha biashara ndani ya uchumi wa nchi za Kiislamu. Licha ya wito huu, biashara ya Indonesia na ‘Israel’ ilifikia dolari milioni 173 kuanzia Januari hadi Septemba 2024, ongezeko la 24.6% kutoka mwaka uliopita.