Jumatano, 07 Jumada al-awwal 1444 | 2022/11/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kitengo cha Wanawake: Kampeni ya Ramadhan "Ramadhan na Ihsan"

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Kitabu chake kitukufu:

﴿لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴾.

"Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu." [Yunus: 26]

Katika Ayah hii nzuri ya Qur'an, Mwenyezi Mungu (swt) anaahidi mambo ya ajabu zaidi ambayo yatalipwa kwa wale wanaofanya mema, na ushindi wake, msaada, utunzaji na tawfiq yake. Malaika Jibril, amani iwe juu yake, wakati mmoja alimuuliza Mtume (saw):

"...فأخبرني عن الإحسان؟"

"Nipe habari kuhusu ihsan" Mtume akamwambia:

«الْإِحْسَانُ أَنْ تَعْبُدَ اللَّهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ»

"Ihsan ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba wamuona, basi ikiwa humuoni hakika Yeye yuakuona" (Bukhari na Muslim). Wanachuoni wameifafanua ihsan kuwa ni kujitahidi kwa ukamilifu, ikhlasi na ubora katika kumtii Mwenyezi Mungu.

Mwezi wa Ramadhan ni wakati mwafaka kwetu kuelewa na kufikiria juu ya mada hii muhimu. Katika mwezi huu uliobarikiwa, tunajaribu kujadidisha uhusiano wetu na Mwenyezi Mungu na kuleta mabadiliko bora kwa maisha yetu na kwa ajili ya maisha yetu ya duniani na Akhera yetu. Kwa hivyo, kipindi hiki cha siku hizi zenye baraka, sisi katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tunataraji kuangazia maswala haya kwa upana katika maudhui yetu ya: "Ramadhan na Ihsan."

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Jumanne, 01 Ramadhan Al-Mubarak 1442 H sawia na 13 Aprili 1442 H

- Ili kufuatilia kwa lugha nyenginezo -

عربي

English

Türkçe

Deutsch

Urdu

Kalima ya Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kwa mnasaba wa kuzinduliwa kwa kampeni "Ramadhan na Ihsan"

Jumanne, 01 Ramadhan Al-Mubarak 1442 H sawia na 13 Aprili 1442 H

- Alama Ishara za Kampeni -

#رمضان_والإحسان

#Ramadan_And_Ihsan

#Ramazan_ve_İhsan

MAKALA


“Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe.”

Muslimah Ash-Shami (Um Suhaib)

9 Ramadhan 1442 H - 21 Aprili 2021 M

KUAMILIANA NA ULIMWENGU HUKU NYOYO ZETU ZIKIMUONA MWENYEZI MUNGU

Yasmin Malik

6 Ramadhan 1442 H - 18 Aprili 2021 M

Kwa Kila Mwanamke wa Kiislamu:

Je Kuna Ujira Wowote wa Wema Isipokuwa Wema?

Bayan Jamal

3 Ramadhan 1442 H - 15 Aprili 2021 M

 

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu