Ijumaa, 17 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari: Angazo Maalum "Naveed Butt... Je, Haijatosha Miaka Kumi ya Utekaji Nyara?!"

 

Mnamo tarehe 11 Mei 2021 M, utaanza mwaka wa kumi tangu Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, alipotekwa nyara mnamo 11 Mei 2012 M na kufungwa katika seli za vyombo vya siri vya ukandamizaji. Mpaka sasa serikali hii ingali inaendelea kumnyima Naveed Butt mawasiliano ya aina yoyote na familia yake. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 ﴿مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ

"Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao." [Fathi: 29] Je! Hali ya watawala hao ambao ni vibaraka wa Amerika ikoje? Wao ni wapole kwa maadui makafiri na hubadilishana nao hisia za upendo, huruma na upole, huku wanaamiliana na Waislamu kwa mkono wa chuma, mpaka wanatumia lugha ya moto na mabomu pamoja nao. Hii ni licha ya maneno yake (swt) katika Hadith Al-Qudsi ambayo ameizungumza Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

 «إِنَّ اللَّهَ قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِياً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ»

"Anaye fanya uadui na kipenzi changu (walii) basi nimekwisha tangaza vita na yeye," Imepokewa na Al-Bukhari. Naveed Butt, mwenye umri wa miaka hamsini na mbili, baba wa watoto wanne, ni mtoto wa Umma wa Kiislamu, na anasifiwa, kwani ni mwanasiasa wa kimfumo na miongoni mwa wenye uwezo kudura ya kutimiza jukumu la kutawala katika nafasi yoyote, baada ya kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume, na yeye anatoka katika familia mashuhuri ya Kashmir anayeishi jijini Islamabad. Alikubaliwa katika Chuo Kikuu mashuhuri cha Uhandisi na Teknolojia (UET) jijini Lahore. Kwa ubora wake, alipelekwa Chuo Kikuu cha Illinois nchini Amerika, ambapo alimaliza kuhitimu kwake. Alifanya kazi katika sekta ya kibinafsi nchini Amerika, kabla ya kuamua kurudi Pakistan kuwa sehemu ya mapambano ya kiulimwengu ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume katika nchi za Kiislamu, akiacha nyuma maisha ya kifahari kukabiliana na ghadhabu za madhalimu. Ameendelea bila kuchoka kufichua khiyana ya watawala wanaofanya kazi dhidi ya Uislamu na Waislamu na kufichua ubaraka wao kwa Amerika, kwa kuandika mamia ya taarifa za vyombo vya habari, kuandika safu kadhaa za magazeti, akihutubia mikutano kadhaa ya waandishi wa habari, akizungumza kwenye semina na makongamano, na kufanya mahojiano na maelfu ya watu wenye ushawishi wakati wa mapambano yake. Amesafiri kote nchini Pakistan ili kueneza ufahamu kati ya watu juu ya wajibu wa kusimamisha Khilafah na kufafanua vyombo vyake, na wakati wa mapambano yake ya kisiasa na mvutano wa kifikra, alikamatwa mara kwa mara na kufungwa na alikuwa maarufu katika kupambana kwake na ujasiri wake. Ni wazi kwamba licha ya ukandamizaji mkali wa serikali ya Pakistan, Hizb ut Tahrir haijaachana na mapambano yake na hajapunguza kasi. Badala yake, ushawishi wa Hizb ut Tahrir kwa ujumla umeongezeka baina ya Waislamu na haswa katika jeshi. Kwa hivyo, Waislamu wanaovumilia shida katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw), wana ikhlasi na wanastahili uongozi. Na katika mwezi huu uliobarikiwa wa Ramadhan, tunamwomba Mwenyezi Mungu (swt), kwamba kama vile Nabii Yusuf (as), alivyo achiliwa kutoka gerezani kwake, kwamba Naveed Butt pia atoke kwenye korokoro za watawala wa kiimla, na amkirimu kwa kuhukumu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt), na wakati huo

﴿وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ﴾.

"Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka." [Ash-Shu'ara: 227]

Ijumaa, 18 Ramadhan Al-Mubarak 1442 H sawia na 30 Aprili 2021 M

Mwacheni Huru Naveed Butt

https://www.change.org/p/free-naveed-butt-603fc16b-15ab-454d-b09c-53a8b5afa89c?redirect=false

Tia Saini Rufaa

Mnamo siku ya Ijumaa, 11 Mei 2012, Naveed Butt alitekwa nyara na maafisa wa kijasusi wa dola ya Pakistan, alipokuwa akiwachukua watoto wake wadogo shuleni.

Kama Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Pakistan, Naveed Butt alifanya harakati za amani za kisiasa, akitetea Khilafah.

Naveed anaamini kwa dhati kwamba maendeleo ya Pakistan yananyimwa kutokana na utiifu wake kwa Amerika na utabikishaji wa mfumo wa kikafiri wa Demokrasia nchini Pakistan.

Kwa hakika, Naveed Butt alitekwa nyara baada ya kuwakosoa vikali watawala wa Pakistan kwa kumwachilia jasusi wa Kimarekani Raymond Davis na kushindwa kuilinda Pakistan dhidi ya shambulizi la Marekani dhidi ya Abottabad.

Naveed Butt kitaaluma ni mhandisi wa umeme na baba wa watoto watatu wa kiume na binti mmoja, ambao wanasubiri kwa hamu kurudi kwake.

Tunalaani utawala wa Pakistan kwa kumtendea ukatili Naveed Butt na tunataka aachiliwe mara moja na aregeshwe salama kwa familia yake.

#FreeNaveedButt

- Ili Kufuatilia Angazo Hili kwa Lugha Nyenginezo -

Ar

En

Tr

Ur

Gr

Kalima ya Video ya Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Muhammad)

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kuhusu Kuendelea Kutekwa Nyara kwa Ndugu Naveed Butt Mwenyezi Mungu Amfariji Shida Yake

Kalima ya Video ya Dkt Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kuhusu Kuendelea Kutekwa Nyara kwa Ndugu Naveed Butt Mwenyezi Mungu Amfariji Shida Yake

Kudai kuachiliwa huru kwa Naveed Butt, ambaye alitekwa nyara tangu mwaka wa 2012 M kwa mujarad tu wa kutaka kwake kukombolewa kwa Pakistan kutokana na kutawaliwa na Marekani!

Tafadhali sambaza video hii kwa Waislamu katika nchi zote kwa jumla na Waislamu nchini Pakistan hasa, na itumwe kwa wanahabari, mawakili, mashirika ya haki za binadamu na misheni za kidiplomasia za Pakistan ndani ya nchi na ng’ambo kwa upana iwezekanavyo. Mwenyezi Mungu yuko katika msaada wa mja maadamu mja yuko katika msaada wa nduguye.

https://twitter.com/FreeNaveedButt_

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan 

Dua na Unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Ajili ya Naveed Butt Mwenyezi Mungu Afariji Kutekwa Nyara Kwake 

  Ijumaa, 14 Ramadhan 1443 H - 15 Aprili 2022 M

Katika mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan, wito wa kutolewa kwa Naveed Butt, mlinganizi wa dhati wa kusimamisha Khilafah!

Katika mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan, wito wa kutolewa kwa Naveed Butt, mlinganizi wa dhati wa kusimamisha Khilafah ambaye alitekwa nyara tangu 11 Mei 2012!

Enyi Watu wa Nguvu na Ulinzi!

Tunakulinganieni mtumie nguvu na ushawishi wenu kuhakikisha kuachiliwa kwa kaka yenu mheshimiwa Naveed Butt!

Naveed Butt anajulikana kwetu sote kama mshauri mwaminifu, aliyebeba ulinganizi wa Khilafah kwa njia ya Utume, na ndiye msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan.

Ndugu yetu mheshimiwa Naveed alitekwa nyara mnamo 11 Mei 2012 na magenge ya watawala wa wakati huo, utawala wa Kayani-Zardari.

Na katika mwezi huu uliobarikiwa wa Ramadhan, ujira ndani yake ni maradufu, tunakulinganieni kutabanni kadhia yake na kudai aachiliwe, ili mwaka wa kumi usipite ilhali angali katika maonevu.

Mtume (saw) asema: ((مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ اَلدُّنْيَا، نَفَّسَ اَللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ اَلْقِيَامَةِ))

"Yeyote mwenye kumuondolea muumini tatizo miongoni mwa matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamuondolea tatizo miongoni mwa matatizo ya Siku ya Kiyama".

Ijumaa ya nne ya mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan, 25 Ramadhan Al-Mubarak 1442 H sawia na 07 Mei 2021 M

#FreeNaveedButt

- Alama Ishara ya Angazo -

#FreeNaveedButt Face Insta Twitter

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tanzania

Hizb ut Tahrir Tanzania Yazuru Ubalozi wa Pakistan Kuitaka Kukomesha Utekaji wa Kimabavu wa Naveed Butt

 19 Dhul Qa'adah 1442 H - 30 Juni 2021 M

Kenya

Hizb ut-Tahrir Kenya Yatuma Ujumbe Wake kwa Ubalozi wa Pakistan Ukibeba Mwito wa Kusitisha Utowekaji wa Naveed Butt

 18 Dhul Qa'adah 1442 H - 29 Juni 2021 M

Wilayah Sudan

Kaimu wa Kazi za Ubalozi wa Pakistan Jijini Khartoum Akataa Kukutana na Ujumbe wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

3 Dhul Qiddah 1442 AH - 14 June 2021 CE

Afisi Kuu ya Habari

Wito wa Kutaka Kumalizwa kwa Kupotezwa kwa Nguvu kwa Naveed Butt Nchini Pakistan

29 Shawwal 1442 H - 10 Juni 2021 M

Makala

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan 

Dua na Unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Ajili ya Naveed Butt Mwenyezi Mungu Afariji Kutekwa Nyara Kwake 

  Ijumaa, 14 Ramadhan 1443 H - 15 Aprili 2022 M

 Barua ya Wazi kwa Naveed Butt, Mashahidi na Wakandamizaji Wake

Mohamed Asif

24 Muharram 1442 H - 01 Septemba 2021 M

Ushuhuda wa Abdullah Haider Kuhusu Naveed Butt

Abdullah Haider

24 Jumada II 1442 H - 06 Februari 2021 M

Faini ya Mamilioni ya Rupia Imetozwa kwa Maafisa wa Serikali Kutokana na Kesi za Watu Waliopotea

Asim Ali Rana

22 Jumada I 1442 H - 06 Januari 2021 M

 Hizb ut Tahrir Kenya:

Kampeni na Amali za Kutaka Kuachiliwa Huru kwa Naveed Butt!

Zaidi ya miaka tisa imepita tangu serikali nchini Pakistan imteke nyara mhandisi Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan, na tangu alipotekwa nyara haijulikani alipo!

Katika suala hili, mnamo Jumanne 29 Juni 2021, Hizb ut Tahrir / Kenya ilituma ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan jijini Nairobi na ujumbe huo ulioongozwa na mwakilishi kwa vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir nchini Kenya Shabani Mwalimu aliandamana na Ustadh Yassin Kiwayo, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Kenya na Bwana Yusuf Gasana mwanachama wa Hizb ut-Tahrir nchini Kenya. Ujumbe ulikutana na kuzungumza na Bwana Charles, mmoja wa wafanyikazi wa ubalozi huo, ambaye aliahidi kuziwasilisha nakala tatu za taarifa kwa vyombo vya habari kwa lugha tatu; Kiurdu, Kiarabu na Kiingereza, kwa Balozi.

Baada ya swala ya Ijumaa mnamo 02 Julai 2021, Hizb ut Tahrir nchini Kenya aliandaa msururu wa amali za kuonyesha kadhia ya Ndugu Naveed Butt kwa kumnusuru na kumuombea nusra, ikitaka aachiliwe mara moja, na imam wa Msikiti wa Taqwa, Sheikh Muhammad Ali, alisoma taarifa iliyotolewa na Afisi Kuu ya Habari kwa anwani "Wito wa Kutaka Kumalizwa kwa Kupotezwa kwa Nguvu kwa Naveed Butt Nchini Pakistan" kwa walio swali baada ya swala ya Ijumaa. Mwenyezi Mungu (swt) anawatunza waja wema.

Ijumaa, 21 Dhu al-Qa'adah 1442 H sawia na 02 Julai 2021 M

Bonyeza Hapa kwa Malezo Kamili

Hizb ut Tahrir/ Wilayah Tunisia:

Kisimamo cha Hali ya Juu Mbele ya Ubalozi wa Pakistan

Jumatatu asubuhi, Juni 21, 2021 ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilaya Tunisia ulizuru ubalozi wa Pakistan jijini Tunis ambapo ulimkabidhi kaimu wa shughuli za ubalozi huo nakala mbili za taarifa kwa vyombo vya habari ya Kiarabu na Kiurdu iliyotolewa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inayoihutubia serikali ya Pakistan chini ya anwani, "Wito wa Kutaka Kumalizwa kwa Kupotezwa kwa Nguvu kwa Naveed Butt Nchini Pakistan" Ujumbe huo uliongozwa na Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Ustadh Yassin bin Yahya, Mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano Ustadh Habib Al-Hajjaji, pamoja na Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika wilaya ya Tunisia Dkt. Al Assad Al-Ajili.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilitaja jinsi Ndugu Naveed alivyokuwa miongoni mwa Mashababu maarufu kutokana na kujitolea kwake katika Uislamu, tabia njema, mwanafikra mkweli, na aliye weza kutoa ruwaza ya "Ramani ya Barabara" ya kufikia Khilafah Rashida.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Bonyeza Hapa kwa Malezo Kamili

Hizb ut Tahrir Denmark:

Ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan Kutaka Kuachiliwa Huru kwa Naveed Butt!

Imepita zaidi ya miaka tisa tangu serikali ya Pakistan ilipomteka nyara Mhandisi Naveed Butt Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, na tangu alipotekwa nyara hajulikani aliko!

Kuhusiana na hili, Hizb ut Tahrir nchini Denmark ilituma ujumbe kwa ubalozi wa Pakistan jijini Copenhagen kutaka kuachiliwa huru mara moja kwa mhandisi aliyetekwa nyara kiholela na kihalifu, Naveed Butt, kwa kutaka kwake kuanza tena kwa maisha ya Kiislamu na kwa kubeba kwake ulinganizi kwa njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Jumatatu, 10 Dhu al-Qa'adah 1442 H sawia na 21 Juni 2021 M

Bonyeza Hapa kwa Malezo Kamili

Hizb ut Tahrir Uingereza:

Ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan Kutaka wa Kuachiliwa Huru kwa Naveed Butt!

Zaidi ya miaka tisa imepita tangu serikali nchini Pakistan imteke nyara mhandisi Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan, na tangu alipotekwa nyara haijulikani alipo!

Katika suala hili, Hizb ut Tahrir nchini Uingereza ilituma ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan jijini London kutaka kuachiliwa huru mara moja kwa mhandisi aliyetekwa nyara kiholela na kihalifu, Naveed Butt, kwa kutaka kwake kurudisha maisha kamili ya Kiislamu na kubeba kwake da'wah kwa kufuata njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Jumamosi, 17 Shawwal 1442 H sawia na 29 Mei 2021 M

Bonyeza Hapa kwa Malezo Kamili

Tufani ya Twitter

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) tutaandaa Tufani ya Twitter kwa kutumia alama ishara

#FreeNaveedButt

Mnamo Siku ya Jumamosi 8 Mei 2021 M

Saa 8pm kwa saa za mji wa Madina Al-Munawwara / 10pm kwa saa za Pakistan.

Tunawaomba Waislamu wote wenye Ikhlasi kupaaza sauti zao kwa ajili ya kuachiliwa huru ndugu yetu Naveed Butt Mwenyezi Mungu amwachishe kutoka kutekwa kwake na mateka wote wa Waislamu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwamba juhudi zenu ziwe katika mizani ya mema yenu

2021 05 08 Naveed Butt Twitter Storm EN

Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan

Katika Kipindi cha Mwezi Uliobarikiwa wa Ramadhan, Wito wa Kuachiliwa Huru Naveed Butt, Mtetezi Halisi wa Khilafah, Aliyetekwa Nyara Tangu Mnamo 11 Mei 2012

20 Ramadhan 1442 H - 02 Mei 2021 M

Bonyeza Hapa

Naveed logo FaceBook

Old Camp en Copy

Mkusanyiko wa Picha

 

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu