Umma wa Muhammad Umeachwa Unazama kwenye Mafuriko ya Matope na Takataka Bila ya Khilafah
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Gazeti la ‘The Guardian’ liliripoti kuwa baadhi ya maeneo ya Gaza yanakabiliwa na mafuriko makubwa wakati wa msimu huu wa baridi baada ya usiku wa mvua kubwa na upepo mkali. Maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na kambi za wakimbizi za Jabalia. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya 85% ya raia wa Gaza sasa wamekimbia makaazi yao; wengi wao ni wanawake na watoto.