Jumapili, 06 Rabi' al-awwal 1444 | 2022/10/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Naibu Kamanda wa Kikosi cha Taliban Atishia Kuichukua Tajikistan

(Imetafsiriwa)

Habari:

Naibu kamanda wa Kikosi cha 217 cha Omari cha Taliban, Mullah Jan Muhammad Hamza, anayejulikana zaidi kama "Mullah Jan", ameitishia Tajikistan kuiteka nchi hiyo ndani ya wiki moja ikiwa Dushanbe haitaacha kuingilia masuala ya ndani ya Afghanistan. Hii inaripotiwa na tovuti 8am.af, ikitoa moja ya vyanzo vyake. Wakati huo huo, Mullah Jan alibainisha kuwa tishio hilo linaweza kufikiwa endapo Urusi haitasimama nyuma ya Tajikistan.

Maoni:

Kumbuka kwamba hapo awali Gulbuddin Hikmatyar, waziri mkuu wa zamani na mwanzilishi wa Chama cha Kiislamu cha Afghanistan, alisema kwamba Tajikistan kupitia "kutoa hifadhi kwa upinzani wa Afghanistan ilitangaza vita na Afghanistan", ikitaka kutoka kwa Dushanbe kutoingilia masuala ya ndani ya Afghanistan.

Tangu kundi la Taliban lilipoingia madarakani nchini Afghanistan hadi leo, Dushanbe imechukua msimamo mkali dhidi ya serikali mpya ya Afghanistan, huku nchi nyengine za eneo hilo zikieleza utayari wao wa kushirikiana na Taliban katika nyanja mbalimbali.

Serikali ya Tajik inataka kuundwa kwa kile kinachoitwa "serikali jumuishi" nchini Afghanistan, huku ikiwaunga mkono wanamgambo wa Massoud Jr. Katika mpango wa utawala wa Rahmon, baadhi ya majaribio yalifanywa kuwasajili wafanyakazi wa kujitolea nchini Tajikistan ili wapelekwe Afghanistan kwa ajili ya vita vya kindugu kwa kisingizio cha kulinda idadi ya watu wanaodaiwa kuwa wasiojiweza wanaozungumza Kitajiki.

Licha ya matamshi ya kivita ya kamanda huyu wa Taliban, kauli hii haiwezi kuwa na mashiko yoyote kwa sababu inakinzana na msimamo rasmi wa Taliban, ambao ni kushirikiana na Jamii ya Kimataifa kwa ajili ya utambuzi wa serikali hii mpya. Wawakilishi wa kundi la Taliban wamekuwa wakisema mara kwa mara kwamba hawataruhusu mashambulizi dhidi ya nchi jirani kutoka eneo la Afghanistan. Jambo ni kuwa utawala wa Tajik haujalishwi sana na uvamizi wa kijeshi kutoka eneo la Afghanistan, bali na mwamko katika eneo hilo la wazo la maisha kulingana na sheria za Uislamu na kuunganishwa eneo moja la kihistoria kwa kuangamizwa mipaka bandia ya kitaifa. Mfano wazi wa uhusiano wa dhati wa watu wa Asia ya Kati na Taliban ni mwitikio kwao wa wakaazi wa Samarkand, ambayo ilitembelewa hivi karibuni na ujumbe wa Afghanistan.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu