Jumapili, 15 Muharram 1446 | 2024/07/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uchomaji Moto Quran: Dhihirisho Halisi la Unafiki

(Imetafsiriwa)

Habari:

Serikali ya Denmark, pamoja na Sweden, zinachukua hatua Madhubuti za kupiga marufuku uchomaji Quran mbele ya afisi za balozi.

Maoni :

Kuhusiana na hili ni muhimu kuangazia nukta zifuatazo:

* Kuchomwa kwa Quran ni sehemu ya kampeni pana dhidi ya maadili ya Kiislamu na desturi za Kiislamu kwa miongo kadhaa. Kuchomwa kwa Quran kumeendelea kutokea kwa kushajiishwa na kuungwa mkono na wanasiasa kwa muda wa miaka kadhaa, sio jambo lililojitokeza ghafla.

* Mabadiliko ya msimamo wa kisiasa wa kukomesha uchomaji huo yanasukumwa na hamu ya kudumisha uhusiano mzuri na tawala potovu katika ulimwengu wa Kiislamu, na kuepuka matokeo ya biashara na siasa za kijiografia, sio kwa sababu ya kuzingatia Uislamu au Waislamu.

* Ni ujanja wa kulidogosha suala hili kwa "vitendo vya aibu vya wapumbavu wachache," huku kwa haraka wakiufanyaUislamu na jamii ya Waislamu kuwajibika kwa maovu ya Waislamu binafsi, na kuzitaka jamii za Kiislamu kujitenga nao. Hili ni muhimu sana hasa wakati utamaduni wa uhuru unawezesha "vitendo vya aibu." Sio tu kwamba vitendo vya chuki vinatuzwa kwa sifa, lakini rasilimali nyingi za polisi zinatumiwa kuwalinda wale waliohusika. Licha ya hali hiyo, wanasiasa wanaendelea kuamini kuwa wanaweza kujinasua kutokana na uhusika wowote.

* Uhuru wa kuzungumza kwa miaka mingi umekuwa chombo kinachotumika kuhalalisha vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, ikifuatiwa na juhudi kubwa ya kusisitiza umuhimu wa kutouwekea vikwazo kwa njia yoyote ile. Mabadiliko ya ghafla ya matamshi na misimamo yanaonyesha wazi kwamba huu ulikuwa ulaghai mkubwa kila mara huku wanasiasa wakijificha nyuma yake, huku kwa upande mwingine wakiwanyamazisha Waislamu kupitia utunzi wa sheria kama vile Sheria ya Mhubiri, ambayo inaharamisha maimamu kuzungumza kwa uhuru kwenye mimbari.

* Miitikio kutoka kwa tawala katika ulimwengu wa Kiislamu ni msimamo wa kinafiki vile vile, kwani hawakuweza kujali hata kidogo kuhusu Quran. Madikteta hawa duni wanaipiga vita Quran mchana na usiku na miitikio hii inalenga tu kuizuia kadhia hii kukola moto na kuchochea maasi mapya ya raia.

* Kadhia hii inaangazia kwa uwazi kabisa ukosefu wa ngao ifaayo na uwakilishi wa kweli kwa Waislamu ndani ya dola ya Kiislamu. Nchi za Magharibi hutanguliza maslahi yao badala ya maadili yao, kwani hata tishio dogo la kiuchumi huwasumbua viongozi wao wa kisiasa, na hivyo kusababisha hatua za haraka za kuzuia uchomaji moto wa Qur'an. Dola ijayo ya Kiislamu itaendesha kwa ustadi diplomasia, mazungumzo, vitisho, ushawishi wa kimkakati na nguvu ya udhibiti ili kukomesha maovu haya ya mara kwa mara.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Elias Lamrabet

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu