Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wale ambao hawako upande wa Haki wanakuwa ni Walinzi wa Batili

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais Erdogan, katika taarifa yake baada ya kikao cha baraza la mawaziri, alisema: “Mashaka juu ya utawala wa Uturuki ni mjadala uliomalizika kwa kuishangilia Jamhuri mnamo Oktoba 29, 1923. Hakuna mtu yeyote katika nchi hii ambaye ana tatizo na jamhuri au mwanzilishi wa taifa.” (Mashirika ya Habari, 16.01.2024)

Maoni:

Jaribio la kuleta maridhiano ya wema na uovu, haki na batili, uadilifu na dhulma ni juhudi tasa sawa na kumtumikia shetani. Katika mfumo wa kidemokrasia usio maadili, ambapo njia yoyote inachukuliwa kuwa halali kwa maslahi ya kisiasa, viongozi hutumia mfumo huo kikamilifu.

Uislamu uliutumikia ulimwengu kwa karne kumi na tatu, ukizileta jamii kutoka gizani hadi kwenye nuru. Hukmu za Kiislamu, mdhamini wa amani na usalama, ziliondolewa kwa ghafla mnamo Machi 3, 1924, na wasaliti waliokuwa wakishirikiana na makafiri. Katika nafasi yake, jamhuri, kinyume kabisa na dhati ya jamii, ilipandikizwa. Rais Erdogan, akijaribu kuushawishi umma kwa kauli mbiu za “Jamhuri iwe na maisha marefu”, anajihusisha kwa khiyari katika kosa kubwa ambalo hata milima ingeogopa. Muumini wa kweli wa Mwenyezi Mungu na maisha ya akhera hapaswi kushirikiana na mifumo hii iliyotungwa na wanadamu.

Utawala wa jamhuri ulioingizwa nchini kutoka nje, ulipandikizwa kupitia kufanya makubaliano na nchi za Magharibi na kuleta uharibifu kwa Uislamu na Waislamu, ni wa kigeni na haukubaliki. Ingawa Waislamu wamechagua viongozi kama Erdogan, kauli zake za uwongo hazitasikika miongoni mwa Waislamu. Viongozi ambao hawaungi mkono haki hutenda kama walinzi wa serikali za batili. Enzi ndefu  ya karne ya ukandamizaji sio sura iliyofungwa kwetu; itaendelea kujadiliwa mpaka mfumo halali wa Khilafah utawale. Hili ni hitajio la kithiolojia na kifikra. Je, suala hili litafungwa vipi wakati ubwana umekabidhiwa wanadamu badala ya Mwenyezi Mungu, aliyeumba mbingu na ardhi, kama ilivyoelezwa katika mamia ya aya?

Mifumo dhaifu iliyotekelezwa katika ulimwengu wa Kiislamu kwa karne moja haipo kwa ajili ya kulinda maisha, utu na dini ya Waislamu bali kuendeleza ubabe wa makafiri waliopandikiza tawala hizi, kama inavyoshuhudiwa katika matukio ya hivi karibuni ya Gaza. Ewe Erdogan! Umetumia kadhia ya Palestina kwa miaka mingi kupata kura kutoka kwa Waislamu. Leo, licha ya kuwa na uwezo, unaweza kuvumilia kutazama uonevu huu ukitokea. Hata hivyo, unataka kufunga mjadala kuhusu tawala za uovu zilizoanzishwa na vibaraka wa Uingereza! Kadhia ya Gaza peke yake imetuonyesha udharura wa kuzibadilisha tawala hizi wa Khilafah.

Tutaendelea kufichua ubatili, uongo, na undumakuwili wa mifumo yote ya wanadamu kila mahali hadi pale Khilafah itakaposimamishwa ili kutabikisha sheria za Mwenyezi Mungu (swt). Tutawalingania Waislamu kukataa masuluhisho yanayokengeuka kutoka katika imani zao mpaka Mola wetu Mlezi aturuzuku kwa mujibu wa amri yake iliyoidhinishwa. Mjadala huu wote utamalizika kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, InshaAllah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu