Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 10/04/2021

Biden Aagiza Uchunguzi ili Kuiweka Sawa Mahakama ya Upeo ya Amerika

Baada ya kufanikiwa kwa Rais wa zamani wa Amerika Donald Trump katika kuunda Mahakama ya Upeo ya Amerika inayounga mkono Republican ambayo inaweza kuhimili kwa miongo kadhaa, Rais Joe Biden ameunda tume ya wanachama 36 ambayo itatumia miezi sita kuchunguza maoni kama vile kupanua mahakama hiyo au kuweka mipaka ya muda ili kusawazisha ushawishi wa vyama. Lakini yote ambayo yanajadiliwa kihalisi ni kusawazisha ushawishi wa vyama, na sio kuuondoa, ambapo waangalizi makini hawakadirii kuwa inawezekana, licha ya madai ya dhati kwamba nidhamu za kidemokrasia zinafuata idara huru ya mahakama.

Serikali ya Amerika kama serikali zote za Kimagharibi zinazo tawala imejengwa juu ya wazo la ugavi wa mamlaka. Mwanafikra wa Ufaransa wa karne ya 18 Montesquieu alilinganisha serikali za Uingereza na Uthmani, akidai kwamba Waingereza walikuwa bora kwa sababu mamlaka hayakujilimbikiza mikononi mwa mfalme peke yake bali yaligawanywa katika vyombo vingi vya utawala. Waundaji wa katiba ya Amerika, wakikinaishwa na hoja za Montesquieu, walibuni matawi matatu tofauti ya serikali, bunge, baraza la utendaji na mahakama, kama 'uangalizi na mizani' dhidi ya kila mmoja yao. Kwa kweli, hata hivyo, uangalizi huu na mizani hutumika tu kuimarisha kipote cha wachache wenye msemo dhidi ya idadi jumla ya watu, kama vile mfano wa uchama katika Mahakama hii ya Upeo unavyo onyesha. Uwajibikaji halisi kwa kweli unawezekana tu katika hali ya mtawala mmoja aliye tawazishwa mamlaka kamili ambaye anaweza kuwajibika moja kwa moja kwa watu. Lakini katika ugumu wa mamlaka sisizo eleweka zenye kuunganika zinazo patikana katika nidhamu za 'kidemokrasia' kihakika ni kipote cha wachache tu waliotawazwa 'watu wa ndani' ndio ambao wanaweza kuunda matokeo yanayohitajika. Hii ndiyo sababu dhana ya 'serikali tawala' imekuwa muhimu sana kuelezea utendakazi wa serikali za demokrasia za kisasa.

Uislamu unazuia uundaji wa 'serikali' tawala unaotazamwa kwa kuwekeza kwa kipote cha wachache kwa kupitia kumpa mamlaka kamili Khalifa kwa maisha yote, ili aweze kumteua yeyote anayemhitaji kumsaidia katika kutawala. Yeye basi ndio mwenye jukumu peke yake na waziwazi kwa upotovu wowote wa serikali kutokana na Uislamu au kutokana na maslahi ya Ummah. Udhaifu wowote katika kumsahihisha basi ni kwa sababu ya uzembe wa Umma, kama ilivyotokea mara kwa mara huko nyuma, na sio kwa sababu ya kasoro yoyote katika mfumo wa Sharia. Hakika, ni kutokana na mapuuza ndio sababu dola kwa ujumla wake imepotea kwa miaka mia moja iliyopita. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utasimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume (saw) ambayo itaunganisha ardhi za Waislamu, kukomboa maeneo yaliyokaliwa, kuregesha mfumo wa maisha wa Kiislamu, na kubeba nuru ya Uislamu ulimwengu mzima. Ili kuzuia mapuuza yoyote yasitokee tena, Ummah unapaswa kuhimizwa kujihusisha sana na maisha ya kisiasa, na wenye ikhlasi na uwezo lazima wahimizwe kujitolea kuwa wanasiasa wenye nguvu na viongozi wa dola, wakishiriki katika kutawala na kuihesabu dola, wote kama watu binafsi na kupitia kuunda vyama vya siasa ambavyo vinauchukua Uislamu pekee kama mfumo wao.

Misri-Sudan-Ethiopia, Jordan, Uturuki

Huku mazungumzo ya hivi karibuni yakimalizika bila ya matokeo kati ya Misri, Sudan na Ethiopia juu ya Bwawa la Blue Nile linalojengwa na la Ethiopia na kupingwa na Misri na Sudan, Rais wa Misri al-Sisi alitishia "machaguo yote yako wazi". Bwawa hilo kubwa linatarajiwa kuipatia Ethiopia faida kubwa ya kimkakati kupitia kuwa na udhibiti wa usambazaji mkuu wa maji kwa Misri na Sudan, ambazo ziko sehemu ya chini ya mto wa bwawa hilo. Licha ya vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe vinavyolenga Tigray, Ethiopia inaendelea na mipango yake. Waislamu hawatakuwa salama kutokana na vitisho vya kimkakati vya nje hadi watakapo simamisha tena Dola ya Khilafah ambayo, karibu tangu kuanzishwa kwake, itaingia katika safu za dola kuu kwa sababu ya ukubwa wake usio na kifani, idadi ya watu, rasilimali, msimamo na mfumo.

Wiki hii, Mfalme Abdullah wa Jordan alipangua jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wake, akimweka kizuizini kaka yake na wengine kadhaa, ambao baadaye waliachiliwa huru. Jordan inaonekana ni 'ufalme wa kikatiba' ulio na serikali iliyochaguliwa. Lakini wale wanaotamani mabadiliko wanajua kuwa mifumo ya kibunge kwa kweli ni pazia tu za mamlaka halisi ambazo zipo ili kuyalinda na kupinga mabadiliko. Mabadiliko ya kweli katika ulimwengu wa Kiislamu yatatokea wakati wenye ikhlasi ndani ya Ummah watakapoikiuka mifumo iliyopo na badala yake kusimama na kupindua mifumo pamoja na watawala ambao mifumo hii inawalinda.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amejikuta akitendewa vibaya na vyombo vya habari vya Ulaya, wakati huu juu ya mipangilio ya kuketi kwa mkuu wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen, ambaye aliketi kwenye kochi badala ya kiti unawasilishwa kama unyanyasaji mkali wa wanawake katika upande ya Uturuki. Hii ni licha ya ukweli kwamba mambo ya itifaki, kama vile mipangilio ya kuketi, huhakikiwa miezi kadhaa mapema kabla ya mikutano hiyo. Watawala wa Waislamu kama vile Erdogan wanajiona kuwa duni kwa Magharibi na kwa hivyo kila wakati wana hamu kuimarisha 'mahusiano mazuri' na nchi za Magharibi. Lakini badali yake ni udhalilishwaji wao kila wakati. Watawala hawa hivi karibuni watabadilishwa na uongozi wa kweli, wenye ikhlasi, wa kujitolea, wa kimfumo ambao utajipima kwa uaminifu wake kwa Uislamu na utiifu kwa maslahi ya Waislamu; ni uongozi kama huo ndio ambao utakuwa na hadhi halisi, katika ulimwengu huu pamoja na akhera.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu