- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari 27/07/2022
Vichwa vya Habari:
- Bangladesh Yatafuta Mkopo wa IMF
- EU Yakubali Gesi ya Mgao huku kukiwa na Hofu ya Ukatishaji wa Urusi
- Kura ya Maoni ya Tunisia Yaidhinisha Upanuzi wa Mamlaka ya Rais
Maelezo:
Bangladesh Yatafuta Mkopo wa IMF
Bangladesh inatafuta mkopo kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, na kuwa taifa la hivi punde zaidi la Asia Kusini kuomba usaidizi huku mafuta ya bei ghali yakiila akiba ya fedha za kigeni ya eneo hilo.
Serikali ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina imemwandikia mkopeshaji wa kimataifa na ombi lake la dolari bilioni 4.5 kutoka kwa IMF. "IMF iko tayari kuisaidia Bangladesh, na wafanyikazi wake watashirikiana na mamlaka juu ya muundo wa programu," shirika hilo la kimataifa lilisema baada ya wafanyikazi wake kutembelea nchi hiyo. Akiba ya fedha za kigeni nchini Bangladesh ilishuka hadi dolari bilioni 39.79 kufikia Julai 13 kutoka dolari bilioni 45.33 mwaka uliotangulia. Hiyo inatosha kugharamia takriban miezi minne ya uagizaji bidhaa kutoka nje, juu kidogo tu kuliko ile iliyopendekezwa na IMF ya miezi mitatu.
EU Yakubali Gesi ya Mgao huku kukiwa na Hofu ya Ukatishaji wa Urusi
Serikali za Muungano wa Ulaya zimekubali kugawa gesi asilia msimu huu wa baridi ili kujilinda dhidi ya kupunguzwa kwa usambazaji zaidi na Urusi huku Moscow ikifuatilia uvamizi wake nchini Ukraine. Mawaziri wa nishati wa EU waliidhinisha rasimu ya sheria ya Ulaya iliyoundwa kupunguza mahitaji ya gesi kwa 15% kuanzia Agosti hadi Machi. Sheria hiyo inajumuisha hatua za hiari za kitaifa za kupunguza matumizi ya gesi na, ikiwa zitaleta akiba isiyotosha, kichochezi cha hatua za lazima katika kambi hiyo yenye wanachama 27. "Ninajua kuwa uamuzi huo haukuwa rahisi, lakini nadhani, mwisho, kila mtu anaelewa kuwa muhanga huu ni muhimu. Tunapaswa, na tutashirikiana maumivu,” Waziri wa Viwanda wa Czech Jozef Sikela aliwaambia waandishi wa habari baada ya kuongoza mkutano huo jijini Brussels. Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwishoni mwa Februari na nchi za Magharibi kujibu kwa kuweka vikwazo vya kiuchumi, nchi 12 za Muungano wa Ulaya zimekabiliwa na kusitishwa au kupunguzwa kwa usambazaji wao wa gesi wa Urusi. "Ujerumani ilifanya makosa ya kimkakati siku za nyuma kwa utegemezi wake mkubwa kwa gesi ya Urusi na imani kwamba itatiririka kila wakati na kwa bei nafuu," alisema Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck, ambaye pia anawajibika kwa nishati na anahudumu kama makamu wa chansela wa nchi hiyo. Usumbufu katika biashara ya nishati ya Urusi na EU tayari unachochea mfumko wa bei ikirekodi viwango barani Ulaya na kutishia kusababisha mdororo wa kiuchumi kama vile kambi hiyo ilivyokuwa ikipata nafuu kutokana na mdororo uliosababishwa na janga la maambukizi. Upunguzaji wa nishati pia unafufua tofauti za kisiasa za miongo mingi zinazohusisha uratibu wa sera. Huku EU ikipata mamlaka kuu juu ya sera za kifedha, biashara, kutoaminiana na mashamba, ubwana wa kitaifa juu ya masuala ya nishati ungali unatawala pakubwa.
Kura ya Maoni ya Tunisia Yaidhinisha Upanuzi wa Mamlaka ya Rais
Rais wa Tunisia Kais Saied amesherehekea ushindi wa karibu uhakika wa kura ya ndiyo katika kura ya maoni ya katiba mpya ambayo inampa mamlaka makubwa na kuhatarisha kuregeshwa kwa utawala wa kimabavu mahali palipozaliwa mapinduzi ya Kiarabu. Tume ya uchaguzi - inayodhibitiwa na Rais Kais Saied - inasema 95% walipiga kura ya ndiyo katika kura ya maoni ya katiba, ambayo ilisusiwa na makundi ya upinzani. Baada ya matokeo yaliyotarajiwa kutangazwa kwenye televisheni ya taifa, wafuasi wa Saied waliendesha magari kwa misafara katikati ya Tunis, wakipeperusha bendera na kupiga honi zao, huku wengine wakiimba wimbo wa taifa au wakipaza sauti “Tutazitoa muhanga nafsi zetu na damu yetu kwa ajili yako, Saied!” Ni karibu theluthi moja tu ya wapiga kura milioni 9.3 waliojiandikisha kupiga kura walipiga kura, tume ya uchaguzi ya ISIE ya Tunisia ilisema, ikionyesha kujitenga kukubwa kwa watu na mchakato wa kisiasa. Bado, waliojitokeza walikuwa wengi kuliko waangalizi wengi walivyotarajia, na ikiashiria kwamba Saied anaendelea kufurahia umaarufu wa kibinafsi karibu miaka mitatu katika mamlaka yake. Muungano mkuu wa upinzani nchini Tunisia mnamo Jumanne ulikashifu bodi ya uchaguzi kwa kughushi idadi ya waliojitokeza kupiga kura. Ahmed Nejib Chebbi, mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Wokovu ambacho kinajumuisha wapinzani wakuu wa Saied, alisema takwimu "zimeongezwa na haziendani na kile waangalizi walichokiona uwanjani" kote Tunisia. Mahali pa kuzaliwa kwa Mapinduzi ya Kiarabu panafanywa kama nembo ya demokrasia, lakini baada ya muongo mmoja demokrasia nchini Tunisia hakika imeleta serikali tepetevu na mivutano ya ndani kwa ndani.