Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 14/09/2022

Vichwa vya habari:

Uraia wa Waislamu wa Uingereza Wadunishwa hadi Hadhi ya ‘Daraja la Pili’, asema mwanafikra

Urusi Yashindwa kwa Kishindo Nchini Ukraine

Azerbaijan Yaanzisha Mashambulizi Mapana dhidi ya Armenia

Maelezo:

Uraia wa Waislamu wa Uingereza Wadunishwa hadi Hadhi ya ‘Daraja la Pili’, asema mwanafikra

Hadhi ya Uraia wa Waislamu wa Uingereza imedunishwa hadi “daraja- la pili” ikiwa ni matokeo ya muendelezo wa udunishaji hadhi ya uraia wa watu, hayo yalidaiwa na mwanafikra mmoja. Taasisi ya Mahusiano ya Jinsia ‘The Institute of Race Relations (IRR)’ imesema malengo ya nguvu hizo hayawajumuishi Waislamu, raia wengi kutoka kusini mwa Asia wamekumbana na ubaguzi na hali ngumu katika uraia wao. Ripoti ya IRR ilichapishwa ikilenga kutoa ufafanuzi juu ya utata wa kesi ya ´Shamima Begum, ambaye alisafirishwa kwa magendo kupelekwa kwa kundi la ISIS akiwa na miaka15, wakati ambapo sheria za uraia na mipaka – zinazoruhusu uraia wa mtu kuondolewa bila hata kupewa taarifa kwa mtu huyo, zinatoka katika vitabu vyenye misingi ya imani fulani. Frances Webber, makamu mwenyekiti wa IRR ambaye pia ndio mwandishi wa ripoti hiyo, ameandika: “Ujumbe ulitumwa na sheria kuhusu zuio la uraia tangu mwaka 2002 na kutabikishwa kwake ikiwa ni dhidi ya Waislamu wa Uingerza wanaotokea kusini mwa Asia ni kuwa, bila kujali hati zao za kusafiria, watu hawa sio na kamwe hawawezi kuwa raia ‘wa kweli’ ukilinganisha na ‘wanati’. Wakati Raia ‘mwanati’ wa Uingereza, ambaye hana uwezo wa kuwa na uraia wa nchi yoyote nyengine, anaweza kufanya uhalifu mkubwa zaidi pasi na kuvuruga haki zake za kubakia Muingereza, hakuna yeyote katika raia wanaokadiriwa milioni 6 wa Uingereza wenye uraia mwingine anaweza kujihisi hali ya kujiamini kutokana na maumbile ya kudumu ya Uraia wao.” Ripoti hiyo inaonyesha sababu ya mtu kuondolewa uraia wake ikiwa ni pamoja na “kueleweka vibaya na kutofahamika” na kuonya hatari ya maana hizi kutumiwa vibaya kisiasa, huku Webber akitolea mfano kesi ya Begum.

Urusi Yashindwa kwa Kishindo Nchini Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametangaza wiki hii kwamba vikosi vya Ukraine vimechukua udhibiti wa zaidi ya kilomita mraba 1,000 (ambazo ni sawa na maili 621) za eneo kutoka Urusi. Vyombo vya habari vya Magharibi vimeipa kipaumbele habari hiyo kuhusu operesheni ya kushtukiza ya kuiokomboa Kharkiv kutoka mikononi mwa Urusi. Baada ya kutangaza kwa wiki nzima kuhusu operesheni ya mji wa kusini wa Kherson, majeshi ya Ukraine yaliwashtukiza Warusi, na hivyo kupelekea majenerali wa Urusi kuamua kuondoa vikosi vyao kutoka kusini mwa Kharkiv, ambapo walizidiwa kiidadi ya 8 kwa 1 huku majeshi ya Ukraine yakishambulia. Waliobakia katika wanajeshi wa Urusi na wanamgambo walikimbia hadi Urusi na kuacha nyuma nyenzo muhimu za kivita kwa wanajeshi wa Ukraine. Huku ni kushindwa kifedheha kwa Urusi iliyo anzisha harakati mbovu za kivita ambapo badala ya kuchukua maeneo zaidi sasa yenyewe ndio inapoteza maeneo.

Azerbaijan Yaanzisha Mashambulizi Mapana dhidi ya Armenia

Azerbaijan imefanya mashambulizi makubwa dhidi ya sehemu muhimu nchini Armenia, hali ambayo haikutarajiwa ikiwa ni matokeo ya mzozo wa muda mrefu kuhusu mpaka wa Armenia. Wizara ya ulinzi ya Armenia imeripoti mashambulizi, yaliyoanza usiku wa kuamkia tarehe 13, yakilenga maeneo muhimu ya miji ya kusini mwa mpaka wa Armenia na Azerbaijan. Wizara ya ulinzi ya Azerbaijan imesema imejibu “mashambulizi ya ndani” kufuatia “vitendo vikubwa vya kichokozi.” Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, katika taarifa yake ya bunge asubuhi, alisema wanajeshi 49 wa Armenian wamefariki katika mashambulizi hayo.  "Tunatakiwa kufahamu kwamba, kwa bahati mbaya idadi hii itaendelea," alisema. Tangu kuanza kwa vita vya Ukraine, kumekuwa na ishara kwamba Azerbaijan imeupima uwezo na utayari wa Urusi wa kutunza amani katika ukanda huo. Kuongezeka kwa mzozo huu ni baada ya Urusi kurudi nyuma kufuatia mashambulizi ya Ukraine. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi amesema kwamba Urusi imepokea ombi la Armenia la kutaka msaada lakini haijasema aina ya msaada itakayoisaidia. Urusi ni mwangalizi wa mkataba wa kusitisha mapigano kati ya pande hizo mbili uliosainiwa mwaka 2020 na walinda amani karibu 2,000 waliopo Nagorno-Karabakh, mpaka wa Azerbaijan ambao vikosi vya  Armenia vilishinda katika vita vya mwanzo kati ya pande hizo miaka ya tisiini. Muda wa tukio hili umekuja pale ambapo Urusi inapata taabu dhidi ya Ukraine.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu