Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari: 05/10/2022

Vichwa vya Habari:

• ‘Fursa’ ya Nord Stream

• Korea Kaskazini Yarushia Japan Kombora

• Kiongozi Mkuu wa Iran Awatuhumu Wafadhili wa Kigeni

Maelezo:

‘Fursa’ ya Nord Stream

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada kwamba mashambulizi dhidi ya mabomba ya gesi asilia ya Nord Stream yanayounganisha Urusi na Ujerumani yanatoa "fursa kubwa" ya kukomesha utegemezi wa Ulaya kwa nishati ya Urusi. Kwa miaka mingi, Marekani ilifanya kazi kwa bidii kupinga Nord Stream 2 kwa kuweka vikwazo lakini ikashindwa kusimamisha ujenzi wake. Mradi huo ulisitishwa na Ujerumani mnamo Februari 22 baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kuamuru wanajeshi kuingia Donbas, agizo ambalo lilitangulia uvamizi wa Februari 24. Marekani imekataa madai kwamba ilihusika na shambulizi la Nord Stream, na vyombo vya habari vya Magharibi vinadokeza kwamba Urusi ilihusika ingawa mabomba hayo yanamilikiwa zaidi na Gazprom, kampuni ya gesi ya serikali ya Urusi. Kwa muda mrefu Marekani ilipinga mabomba ya Nord Stream kwani inafanya Ulaya kutegemea gesi ya Urusi na kwa maoni kama vile ya Anthony Blinken, ingeonekana waziwazi kidole cha lawama kinanyoshewa Marekani kwa kuhujumu bomba hilo.

Korea Kaskazini Yarushia Japan Kombora

Korea Kaskazini ilirusha kombora la masafa ya kati ambalo liliruka maili 2,850, likiwa na kasi ya juu katika eneo la kaskazini mwa Japan takriban Machi 17. Kombora hilo lilitua katika Bahari ya Pasifiki baada ya kuruka kwa takriban dakika 22. Kama matokeo ya jaribio hilo, mamlaka ya Japan ilitoa onyo la kujihami kwa kisiwa cha Hokkaido. Wataalamu wanaamini kuwa kombora hilo lilikuwa aina ya Hwasong-12, aina ile ile ya kombora lililoruka juu ya Japan mwaka wa 2017. Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan walizungumza kwa njia ya simu na kulaani jaribio hilo kwa "matamshi makali zaidi," na kulitaja kuwa hatari kwa Watu wa Japan, na Biden akaimarisha ahadi ya "ironclad" ya Marekani kwa ulinzi wa Japan.

Majaribio hayo ya Korea Kaskazini yanajiri wakati ambapo mazoezi ya pamoja yanafanywa na Marekani, Korea Kusini na Japan, na wakati Makamu wa Rais wa Marekani alipotembelea mpaka ulioimarishwa kati ya Korea mbili.

Korea Kaskazini inaituhumu Marekani na washirika wake kwa kuitishia kwa mazoezi na uimarishaji ulinzi.

Kiongozi Mkuu wa Iran Awatuhumu Wafadhili wa Kigeni

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alijibu maandamano makubwa zaidi nchini Iran katika miaka mingi, akivunja kimya cha wiki kadhaa kulaani kile alichokiita "machafuko" na kuituhumu S na Israel kwa kupanga maandamano hao.

Akizungumza na kada ya wanafunzi wa polisi jijini Tehran, Khamenei alisema "amehuzunishwa sana" na kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 chini ya ulinzi wa polisi, na kuliita "tukio la kusikitisha." Hata hivyo, alikemea maandamano hayo kama njama ya kigeni ya kuyumbisha Iran, akiakisi maoni ya hapo awali ya mamlaka hiyo.

“Ghasia hizi zilipangwa,” alisema. “Machafuko haya na ukosefu wa usalama viliundwa na Amerika na utawala wa Kizayuni, na wafanyikazi wao.”

Vuguvugu la hivi punde la waandamanaji nchini Iran limesababisha baadhi ya machafuko yaliyoenea katika taifa hilo kwa miaka mingi, yaliibuka kama muitiko kwa kifo cha Amini. Tangu wakati huo yamekua changamoto ya wazi kwa uongozi wa Iran.

Maandamano hayo yameibua malalamiko mengi nchini Iran, ikiwemo ukandamizaji wa kisiasa wa nchi hiyo na uchumi unaodorora. Machafuko yameendelea jijini Tehran na mikoa ya mbali hata baada ya mamlaka kukatiza matumizi ya mtandao wa intaneti na kuifunga mitandao ya kijamii.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu