- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa
Amiri wa Hizb ut Tahrir
Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook
Jibu la Swali
Je, Anahutubiwa (Khitwab) Nani katika Aya Hii
[یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوۤا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ یَنصُرۡكُمۡ]
"Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni" [Muhammad: 7]
Kwa: Mohamed Ali Bouazizi
(Imetafsiriwa)
Swali:
Assalam Alaykum
Mwenyezi Mungu awaongoze watu wote katika yale yenye kheri kwa Uislamu na Waislamu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوۤا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ یَنصُرۡكُمۡ]
"…Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni" [Muhammad: 7]
Je, hotuba hii inaelekezwa kwa umma pekee, yaani je, Mwenyezi Mungu ataunusuru Umma wakati ambao Uislamu unatabikishwa ndani yake? Kwa maana nyengine, Nusra inapotolewa kwa kikundi (kutla) kinachofanya kazi ya kurudisha maisha ya Kiislamu na Khalifa kuanza kutekeleza Uislamu, ndio Nusra ya Mwenyezi Mungu huanza?
Au je, hotuba katika Aya hii pia inahusu kundi linayofanya kazi ya kurudisha maisha ya Kiislamu na Mwenyezi Mungu kuwanusuru ni kwa kuitikia mwito watu wa Nusra (Ahlu nusra), kama Seerah ilivyoeleza kuwa Mwenyezi Mungu alipotaka kumnusuru mja wake (Muhammad, amani iwe juu yake) alipeleka kwake kundi la Aws na Khazraj?
Jibu:
Waalaykum salam Warahmatullahi Wabarakaatuh
Aya hiyo tukufu ni:
[یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوۤا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ یَنصُرۡكُمۡ وَیُثَبِّتۡ أَقۡدَامَكُمۡ (٧) وَٱلَّذِینَ كَفَرُوا۟ فَتَعۡسࣰا لَّهُمۡ وَأَضَلَّ أَعۡمَـٰلَهُمۡ (٨) ذَ ٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَرِهُوا۟ مَاۤ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأَحۡبَطَ أَعۡمَـٰلَهُمۡ (٩)]
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu * Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao * Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.” [Muhammad: 7-9]
Hotuba hiyo ni ya jumla (walio amini) ni kwa Waumini na sio kwa wapiganaji peke yake, yaani inajumuisha kupigana na mengine yasiokuwa ya kupigana pia yanahusu jeshi katika vita na vilevile kwa kundi linalobeba Dawah. Hotuba hii haiidhinishi kiwazi juu ya vita mfano wa Aya:
[وَقَـٰتِلُوهُمۡ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتۡنَةࣱ وَیَكُونَ ٱلدِّینُ لِلَّهِۖ فَإِنِ ٱنتَهَوۡا۟ فَلَا عُدۡوَ ٰنَ إِلَّا عَلَى ٱلظَّـٰلِمِینَ]
“Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu.” [Al-Baqara: 193]
[قَـٰتِلُوهُمۡ یُعَذِّبۡهُمُ ٱللَّهُ بِأَیۡدِیكُمۡ وَیُخۡزِهِمۡ وَیَنصُرۡكُمۡ عَلَیۡهِمۡ وَیَشۡفِ صُدُورَ قَوۡمࣲ مُّؤۡمِنِینَ]
“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.” [At-Tawba: 14]
Hotuba katika Aya tukufu ndio mada ya swali sio andiko (naswi) kuhusu kupigana vita pekee ambayo haikusanyi mengineyo bali ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu (swt):
[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَٱلَّذِینَ ءَامَنُوا۟ فِی ٱلۡحَیَوٰةِ ٱلدُّنۡیَا وَیَوۡمَ یَقُومُ ٱلۡأَشۡهَـٰدُ]
"Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi" [Ghaafir: 51]. Mwenyezi Mungu (swt) hawanusuru mitume wake pekee, bali kadhalika (na walioamini),
[وَٱلَّذِینَ ءَامَنُوا]
Na nusra sio tu siku watakaposimama mashahidi:
[وَیَوۡمَ یَقُومُ ٱلۡأَشۡهَـٰدُ]
Yaani Akhera pekee wapate radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo ya Firdawsi, bali kadhalika katika uhai wa duniani kwa izza na tamkini:
[فِی ٱلۡحَیَوٰةِ ٱلدُّنۡیَا]
Inaweza kusemwa kwamba neno ushindi na uthabitishaji wa nyayo linaonyesha ushindi katika vita, na hii ni kweli, lakini pia halikatai ushindi wa mbebaji Daawah kwa kufikia lengo lake, yaani, kushinda katika ulimwengu huu na Akhera, kama tulivyoeleza hapo juu kwa ujumla wa hotuba, hivyo yote haya ni ushindi (Nusra), yaani ni kufuzu. Pia, kuimarika kwa nyayo kunaweza kuwa kwa kuegemea kwenye kauli ya haki, kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu:
[یُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِینَ ءَامَنُوا۟ بِٱلۡقَوۡلِ ٱلثَّابِتِ فِی ٱلۡحَیَوٰةِ ٱلدُّنۡیَا وَفِی ٱلۡـَٔاخِرَةِ]
“Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Akhera.”
- Imekuja katika tafsiri ya Ibn Kathir juu ya Aya:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ (7) وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ (8) ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ]
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao * Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.” [Muhammad: 7-9]
Mwenyezi Mungu amesema:
[یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوۤا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ یَنصُرۡكُمۡ]
"…Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni" [Muhammad: 7]
Kama kauli yake:
[وَلَيَنْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ]
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye.” [Al-Hajj: 40]
Kwani malipo ni kwa mujibu wa vitendo, Ndio maana akasema:
[وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
“Na ataithibitisha miguu yenu” [Muhammad: 7] kama ilivyokuja katika Hadith:
«مَنْ بَلَّغَ ذَا سُلْطَانٍ حَاجَةَ مَنْ لَا يَسْتَطِيعُ إِبْلَاغَهَا، ثَبَّتَ اللَّهُ قَدَمَهُ عَلَى الصِّرَاطِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»...
“Mwenye kumfikishia haja Sultani yule ambaye hawezi kumfikishia, Mwenyezi Mungu atazithibitisha nyayo zake katika Swirati Siku ya Kiama…”
[یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوۤا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ یَنصُرۡكُمۡ]
"Enyi Mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni" [Muhammad: 7] yaani Dini ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (atakunusuruni) dhidi ya adui yenu:
[یَنصُرۡكُمۡ]
Na ataifanya imara miguu yenu:
[وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
Na kukufungulieni katika sehemu za vita au kwenye malengo ya Uislamu]. Kuthibitishwa huwa katika vita na huwa katika Daawah kwa Uislamu.
- Na ikaja katika tafsiri ya Al-Qurtubi katika tafsiri ya Aya tukufu:
[یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوۤا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ یَنصُرۡكُمۡ]
"…Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni" [Muhammad: 7] Yaani mkiiunga mkono Dini ya Mwenyezi Mungu atakunusuruni dhidi ya makafiri. Mfano wake:
[وَلَيَنْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ]
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye.” [Al-Hajj: 40]
Katrib akasema: Mkimsaidia Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atakunusuruni, na maana yake ni moja.
[وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
“Na ataithibitisha miguu yenu” [Muhammad: 7].
Yaani, wakati wa kupigana. Husemwa kuhusu Uislamu. Husemwa katika Swirati. Na husemwa: Maana yake ni kuzithibitisha nyoyo kwa usalama...
Na kuthibitisha miguu: ni uwakilishi wa yakini na ukosefu wa udhaifu katika hali ya yule ambaye miguu yake imesimama juu ya ardhi na haikuteleza, kwa sabab utelezaji ni udhaifu unaomfanya mtu kuanguka, na kwa hiyo inawakilisha kushindwa, kukata tamaa na kukosa. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[فَتَزِلَّ قَدَمُۢ بَعۡدَ ثُبُوتِهَا]
“…Usije mguu ukateleza baada ya kuthibiti kwake” [An-Nahl: 94]
Hitimisho ni kwamba Aya tukufu, ijapokuwa inaashiria ushindi katika vita na utulivu wa miguu katika vita, lakini haikanushi ushindi wa Dini ya Mwenyezi Mungu katika kubeba Daawah yake na uthabiti wake juu ya haki, ili miguu isiteleze, na kisha mbebaji Daawah asiogope lawama ya mwenye kulaumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Natumaini kwamba hii inatosha na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi na Mwingi wa Hekima.
Ndugu Yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
25 Rajab Al-Khair 1443 H
26/02/2022 M
Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook.
#أقيموا_الخلافة #الخلافة_101
#ReturnTheKhilafah #YenidenHilafet #TurudisheniKhilafah