Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali

Watu wa Al-Fatra, Mayahudi na Wakristo

Kwa: Sheikh Asim Al-Jabari

Swali:

Baada ya kutumilizwa bwana wetu Muhammad, Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, je wale waliobakia katika dini ya Kiyahudi au Kikristo watahesabiwa miongoni mwa watu wa Peponi? Na nini hatima ya wale ambao hawakupokea ujumbe wa Muhammad na kuabudu masanamu au viumbe vyengine? Ikibainishwa katika jibu tofauti zilizotajwa.

Tupe faida, Mwenyezi Mungu akubariki

Jibu:

Assalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh,

Ni kana kwamba unauliza kuhusu watu wa Al-Fatra... na chukua haya hapa yafuatayo:

1- Kwa kuanzia ni lazima itiliwe mkazo kuwa Mayahudi na Wakristo ni makafiri na kadhalika washirikina, na kila anaye abudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu wote hao wote ni makafiri, Muislamu ni anaye itakidi Dini ya Uislamu aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad rehma na amani zimshukie na kafiri ni anayefuata dini isiyokuwa Uislamu na huyo sio muumini na sio Muislamu. Amesema Mwenyezi Mungu: [إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللّهِ الإِسْلاَمُ] “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu.” [Aal-i-Imran: 19]. Na akasema Mwenyezi Mungu: [وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِيناً فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ] “Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake.” [Aal-i-Imran: 85]. Asiyekuwa Muislamu ni kafiri, na akifa atakaa milele Motoni, wanakuwa sawa katika hayo Wapagani, Mayahudi, Mabudha, Wakristo na Wakomunisti, wote ni makafiri na wote si Waislamu na sio waumini, na watadumu Motoni Siku ya Kiyama. Aya za Qur'an zimewakufurisha kila asiyefuata Uislamu na kuwazingatia wasiokuwa Waislamu kuwa ni makafiri bila ya tofauti baina ya kafiri na mwengine. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Wakristo: [لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَآلُواْ إِنَّ اللّهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ] “Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu!” [Al-Ma’ida: 72]. Na akasema: [لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُواْ إِنَّ اللّهَ ثَالِثُ ثَلاَثَةٍ] “Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu.” [Al-Ma’ida: 73]. Na kasema kuhusu watu wa kitabu nao ni Mayahudi na Manaswara: [يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللّهِ] “Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu? [Aal-i-Imran: 70]. Na kasema wako sawa katika ukafiri washirikina na watu wa kitabu: ﴿مايَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُواْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلاَ الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ﴾ “Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi.” [Al-Baqara: 105]. Na kasema: ﴿لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّى تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ﴾ “Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana” [Al-Bayyina: 1]. Na akasema: ﴿إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ﴾ “Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo.” [Al-Bayyina: 6]. Na Mtume, rehema na amani zimshukie, alipowafukuza Mayahudi wa Banu al-Nadhir, kauli ya Mwenyezi Mungu iliteremshwa: ﴿هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِنْ دِيَارِهِمْ لأوَّلِ الْحَشْر﴾ِ “Yeye ndiye aliye watoa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu katika nyumba zao wakati wa uhamisho wa kwanza.” [Al-Hashr: 2]

2- Hapo awali mnamo tarehe 18 Ramadhan 1439 H sawia na 06/03/2018 M, tulijibu swali kuhusu watu wa Al-Fatra, na kutokana na jibu lililotajwa hapo juu lilikuwa kama ifuatavyo:

[Hii yamaanisha kuwa watu waliokuwa baina ya ujumbe wa Mtume (saw) na baina ya utume wa Mitume kabla yake (yaani watu wa Al-Fatra) wataokoka kwa sababu hawakufikishiwa ujumbe. Hii ni ikiwa walikuwa washirikina au hawakufuata ujumbe. Ama Watu wa Kitabu (Ahl al-Kitab) walifuata ujumbe kisha wakaupotosha, wamemfuata Mtume, basi walifikishiwa ujumbe, kisha wakaupotosha, na kwa hivyo hawazingatiwi katika watu wa Al-Fatra..., Na kadhalika makafiri wa Magharibi hawazingatiwi kuwa watu wa Al-Fatra, Kwani Uislamu umewafikia, basi vipi kuhusu makafiri wanaoishi miongoni mwa Waislamu? Kwa hiyo watu wa Al-Fatra ni wale ambao hawakufikiwa na Daawah, na wengine wote si katika watu wa Al-Fatra.] Mwisho.

Ni wazi kutokana na jibu hili kwamba Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Manasara walioipotosha dini ya Mitume wao hawazingatiwi kuwa watu wa Al-Fatra na hawajaokoka hata kabla ya utume wa Mtume (saw), basi vipi baada ya utume wake na kutambua kwao ujumbe wake?

3- Kuhusiana na Mayahudi na Manaswara waliobakia katika dini yao baada ya utume wa Mtume (saw) kama ilivyo elezwa katika swali hilo, ilitajwa Hadith ilio wazi kuhusu wao kutoka katika Hadith ya Mtume (saw) ambayo Muslim ameiingiza katika Sahih yake kutoka kwa Abu Hurairah kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye amesema: وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَا يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الْأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلَا نَصْرَانِيٌّ ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَّا كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ» “Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad imo mikononi mwake Hatonisikia yoyote kutoka katika Umma huu iwe Myahudi, wala Mkristo, kisha akafa, na hakuamini kile nilichotumwa nacho isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni

Na ni wazi katika hii hadith tukufu kwamba ambaye hakumfuta Muhammad (saw) katika Mayahudi na Manaswara baada ya kutumilizwa kwake basi hatokuwa miongoni mwa wenye kuokoka bali atakuwa katika watu wa Motoni.

4- Ama yale yaliyokuja katika swali lako kuhusu wanao abudu masanamu na wanao abudu viumbe vyengine ambao hawakupata ujumbe wa Mtume Muhammad (saw), tunaona haiwezekani kuwa duniani kutakuwa na wale ambao hawakufikiwa na ujumbe wa Uislamu. Kwanza dunia imekuwa karibu kama kijiji kidogo na kinachotokea mashariki yake kinajulikana kwa watu wa Magharibi katika muda mfupi kulingana na maendeleo makubwa katika mawasiliano ... Uislamu ni gumzo la watu kila mahali, na nchi kubwa na nchi za washirika wao wanapiga vita Uislamu kwa jina la “ugaidi.” Viongozi na wanasiasa wake wanautaja Uislamu katika maneno yao kila siku, na vipindi vinarusha habari kuhusu Uislamu na Mtume wa Uislamu, amani iwe juu yake ... Kisha Waislamu wameenea katika Ulimwengu wote wanawasiliana na wasiokuwa Waislamu... Mabudha, Mabaniani na Makalasinga wanaujua Uislamu na wanawajua Waislamu... Na wanao abudu masanamu katika Afrika wanawajua Waislamu... Kwa hiyo, kama tulivyotaja hapo juu, tunaona hilo haliwezekani katika duniani kwamba kuna wale ambao hawajasikia Uislamu na ambao hawajafikiwa na wito wa Uislamu...

Lakini endapo tutadhania kuwa wapo ambao hawajafikiwa na wito wa Uislamu katika zama zetu, miongoni mwa waabudu wa masanamu au waabudu wa viumbe vyengine ambao hawafuati ujumbe wa mtume miongoni mwa manabii, basi hawa wanachukua hukmu ya watu wa Al-Fatra na wala hawaadhibiwi kwa kutoufuata ujumbe wa Muhammad (saw), kwa sababu hawaujui wala hawausikii wala Mtume, amani iwe juu yake.” Na hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema: [وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّى نَبْعَثَ رَسُولاً]Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume [Al-Isra: 15]. Na kwa kusema kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu: [... لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ] “…ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume” [An-Nisa: 165]. Lakini mimi nakariri kuwa ni vigumu kuwepo na mtu ambaye hajafikiwa na ujumbe wa Uislamu. Na pamoja na hayo, ikiwa ni kwa njia ya kudhania kuwa yupo, basi atakuwa ni katika watu wa Al-Fatra.

Hili ndilo ninaloliona katika jambo hili na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi, Mwingi wa hekima.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

16 Shawwal 1443 H

16/05/2022 M

Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu