Katika wakati ambapo vyama tawala vinajiandaa kushindana katika uchaguzi na ngawira zake zilizopangwa kufanyika Novemba 11 mwaka huu, vikosi maalum, vifaru, na magari ya kivita, alfajiri ya Ijumaa, 22/08/2025, vilizingira Hoteli ya Lalezar katikati ya Sulaymaniyah na kuivamia, ili kutekeleza operesheni ya kumkamata mkuu wa Chama cha Jabhat Ash-Sha’ab, Lahur Sheikh Jangi. Baada ya mapigano makali ya silaha yaliyodumu kwa masaa mengi kati ya Vikosi vya Kupambana na Ugaidi na Vikosi Maalum (Commandos) na “Asayish,” vikosi vya usalama vilivyounganishwa na Muungano wa Uzalendo wa Kurdistan upande mmoja, na walinzi wa Sheikh Jangi upande mwengine, yalimalizika kwa kukamatwa kwa Lahur na kaka yake Pulad, na kusababisha vifo na majeraha.