Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 511
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Jana, Ijumaa, Agosti 23, 2024, mkutano wa Geneva, ulioanza Agosti 14 kujadili mgogoro wa Sudan, ulihitimishwa kwa kuunda “Muungano wa Umoja wa Kimataifa” ili kumaliza vita nchini Sudan. Kwa mujibu wa Mjumbe Maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Prillo, muungano huo unajumuisha, pamoja na Marekani, Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, IGAD, pamoja na Uswizi, Saudi Arabia, UAE na Misri. Hata hivyo, pamoja na urefu wa majadiliano ya Geneva, matokeo hayana thamani ya halisi katika kusimamisha vita vya kikatili vinavyoendelea nchini Sudan.
Matembezi ya 46 mfululizo yalifanyika tangu kuanza kwa Vita vya Kimbunga cha Al-Aqsa, yakianzia mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu wa Tunis, hadi barabara ya Al-Thawra, ambayo yaliitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kwa watu wa Al-Zaytouna kuwanusurur watu wa Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka, na kichwa chake kilikuwa “Enyi Jeshi la Algeria: Gaza inahitaji Misafara na Vifaru, sio Ujenzi wa Hospitali!”
Ripoti ya habari ya Shirika la Habari la Jordan, Petra, ya tarehe 6 Agosti 2024, ilisema kwamba “Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi iliamua kwamba serikali wala Kampuni ya Kitaifa ya Umeme hazihitajiki kulipa sehemu yoyote ya gharama kwa Kampuni ya Umeme ya Al-Attarat.” Habari hizi za upotoshaji zinakusudiwa kuficha hasara inayotarajiwa ambayo serikali ya Jordan itaipata kutokana na ukweli wa hukumu hiyo, inayosema: “Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi inaamuru kwamba mkataba huo ni halali na hauhusishi ukosefu mkubwa wa haki.”
Barabara za Kenya zilisalia kuwa uwanja wa vita huku maandamano, yaliyochochewa na ongezeko la ushuru lenye utata, yakibadilika na kuwa kilio kikubwa dhidi ya tofauti za kiuchumi zilizokita mizizi na kukosekana kwa uwajibikaji wa serikali. Mstari wa mbele wa vuguvugu hili ni kizazi cha vijana wa Kenya, wanaokataa kunyamazishwa licha ya kukabiliwa na msako mkali wa polisi.
Rais William Ruto amewateua wanachama wanne wa chama kikuu cha upinzani kama sehemu ya baraza jipya la mawaziri huku maandamano yakiendelea kulitikisa taifa hili la kanda ya Afrika Mashariki. Rais alikuwa ameahidi kuteua baraza jipya la mawaziri ili kukabiliana na maandamano ya G-z yaliyoshuhudiwa mwezi mmoja uliopita.
Kufuatia hatua ya serikali za kuwahamisha jamii ya wafugaji wa kimasai katika maeneo ya Mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro, sisi Hizb ut Tahrir Tanzania tunalaani hatua hiyo na hatukubaliani na kitendo hicho kiovu.
Mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 19/8/2024, Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune alitoa wito kwa Misri kufungua mipaka na Ukanda wa Gaza kwa jeshi la Algeria, ili kuwanusuru wakaazi wa Ukanda wa Gaza, na kusema: “Naapa kwamba haraka iwezekanavyo tutapeleka vitengo huko na kujenga upya kile kilichoharibiwa,” na akasema: “Jeshi la Algeria liko tayari kwenda Gaza na sisi tuko tayari, tunasubiri tu Misri itufungulie mipaka yake.”
Mnamo tarehe 09 Agosti, 2024, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu utekaji nyara na upotezaji wa watu unaoendelea nchini. Shirika hilo liliorodhesha takriban watu 83 walioripotiwa kutekwa nyara na kutoweka tangu 2016.