Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 486
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya kuutafuta mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mkesha huu wa Jumatatu, muandamo wa mwezi mpya kwa mujibu wa matakwa ya Shariah unathibitishwa, na kwa hiyo kesho, Jumatatu ni siku ya kwanza ya mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan kwa mwaka huu wa 1445 H.
Kalima ya Ustadh Ali Al-Bakri wakati wa kisimamo kilichoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Syria siku ya Ijumaa, “Kumbatio, Mamlaka na Nguvu ni zenu basi Nusuruni na wala Msimtelekeze.”
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Machi 2024 M.
Mnamo Februari 16, 2024, uainishaji wa kundi la Houthi kama Kundi Lilioundwa Maalum kwa Ugaidi Ulimwenguni (SDGT) ulianza kutumika. Je, ni faida zipi Marekani inazopata kutokana na uainishaji huu, na ni zipi athari zake kwa kundi la Houthi baada ya miaka kumi tangu kuingia kwao Sana’a?
Katika hali ya kusikitisha ya kujichoma moto kwa watawa wa Kibudha wakati wa Vita vya Vietnam, mwanachama anayehudumu wa Jeshi la Wanahewa la Marekani mnamo Februari 26, 2024, alijichoma moto mbele ya ubalozi wa 'Israel' jijini Washington D.C., akitangaza, "Sitakuwa mshiriki tena katika mauaji ya halaiki.”
Mashambulizi ya mabomu ya Lebanon ya wale waliokasirikiwa - Mayahudi - yamekuwa ya mara kwa mara kila siku, na hata kuathiri miji mikubwa kama Sidoni, Tyre, na Nabatieh, baada ya kufungika kwenye vijiji vya mpakani, kuua na kujeruhi watu walio salama katika maeneo hayo na mijini.
Kwa mnasaba wa karne moja ya Miladi (103 H), Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia itafanya Kongamano la kila mwaka la Khilafah chini ya kichwa:
“Khilafah ya Kiislamu... kama Mfumo Mpya wa Kimataifa”