Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 22 Rajab 1444 | Na: HTS 1444 / 32 |
M. Jumatatu, 13 Februari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Ulikutana na Mkurugenzi wa Polisi wa Forodha na Naibu Mkurugenzi wa Polisi huko Wadi Halfa
(Imetafsiriwa)
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ukiongozwa na Ustadh Abdul-Azim Issa- Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, ukifuatana na Ustadh Bilal Ali - Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na Issam Yusuf, na Abdullah Mahjoub, ambao ni waungaji mkono wa hizb, walikutana katika ziara ya kwanza mnamo Jumapili tarehe 12/02/2023 na Brigedia Jenerali Sir Al-Khatam Ahmad Othman - Mkurugenzi wa Polisi wa Forodha wa Wadi Halfa.
Ustadh Abdul-Azim alimueleza Mkurugenzi huyo, baada ya kuutambulisha ujumbe huo, madhumuni ya ziara hiyo kuwa Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ilianzisha kampeni ya kupambana na mihadarati kwenye Shirika la Habari la SUNA mnamo Jumapili tarehe 22/1/2023, na kwamba kampeni hii inajumuisha mihadhara, semina, kalima za hadhara, na mikutano na maafisa wa serikali, kila mmoja kulingana na utaalamu wake, na kampeni hii iliandaliwa katika majimbo mengi ya Sudan.
Mkuu wa ujumbe pia aliweka wazi kwamba umbile la Kiyahudi lina dori ya moja kwa moja katika kuijaza Sudan na dawa za kulevya, ikionyesha hatari ya kuhalalisha mahusiano na umbile hili cha nyakuzi. Alihitimisha risala yake kwa kusema kuwa utatuzi msingi wa tatizo la mihadarati na matatizo mengine yanayoikumba nchi ni kushughulikiwa kwa mujibu wa hukmu za Aqidah (itikadi) tukufu ya Kiislamu, ambayo hutabikishwa na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Mkurugenzi wa Polisi wa Forodha alipongeza hatua za hizb, akiushukuru ujumbe kwa ziara hiyo yenye malengo, na kuitakia mafanikio hizb, na kusema kwamba watashiriki katika kazi yoyote ambayo hizb inafanya, Mwenyezi Mungu akipenda.
Katika ziara ya pili, ujumbe ulikutana na Luteni Kanali Khalid Muhammad Ali - Naibu Mkurugenzi wa Polisi wa eneo la Wadi Halfa. Baada ya kuutambulisha ujumbe huo, Ustadh Abdul-Azim alieleza kile ambacho hizb inafanya ndani ya wigo wa kampeni ya hizb ya kupambana na mihadarati. Abdul-Azim alirudia kile alichosema kwa Mkurugenzi wa Polisi wa Forodha wa Wadi. Kanali aliisifu hizb na mpango wake, na sehemu ya kauli yake ilikuwa: “Kule kwamba hizb inakuja kwetu juu ya suala hili na kutuletea machapisho haya, hii ina maanisha kwamba ni chama kitukufu na ‘sio kidhaifu’”, na alitumai kwamba vyama vyengine vya kisiasa nchini Sudan vitafuata mfano wa Hizb ut Tahrir, akitoa wito wa kufanyika semina kubwa mjini humo. Alisema kwamba angewasiliana na ndugu, mkuu wa polisi, ambaye hakuwepo wakati wa ziara hiyo. Kwa kumalizia, aliushukuru ujumbe huo na kuitakia hizb mafanikio katika kazi yake.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/3079.html#sigProIda34cca927e
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |