Tafsiri Al-Baqarah [Muhkam na Mutashabiha]
- Imepeperushwa katika Tafsiri Al-Baqarah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Jambo muhimu katika sayansi ya Quran linalohusiana na tafsiri ya aya za Mwenyezi Mungu, mbali na maana halisi na ya kimajazi, ni kuwepo kwa yaliyo wazi na yaliyo na utata katika Kitabu. Mwenyezi Mungu (saw) amesema, “Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.”



