Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mgogoro wa Amerika Katika Demokrasia Unamtupia Biden Changamoto Nyingi

Baada ya mashambulizi ya fujo kwenye Makao ya Serikali ya Amerika (US Capitol Hill), wito wa mashtaka kwa Trump na kutaka ajiuzulu umepamba moto kote katika jamii ya Wamarekani. Kampuni za teknolojia kama Twitter na Facebook zimemfungia Trump kutuma maudhui, huku Msemaji wa Baraza la Wawakilishi la Amerika Nancy Pelosi akitaka Trump kunyang'anywa alama za siri za uzinduaji wa nyuklia wa taifa na kumzuia kuanzisha vita. [1] Trump amejaribu kujiepusha na lawama kwa kuwashutumu waandamanaji, lakini wakosoaji wamepuuzia mwenendo wake wa uchekeshaji akiwa anajaribu kujikinga na adhabu kutokana na mapinduzi baridi.

Matukio ya wiki iliyopita si tu yamemomonyoa taswira ya Amerika nje na sifa ya demokrasia yake, lakini pia ndani kuna maswali ya kina yanabakia kuhusu uungaji mkono wa wanachama wa republican wa juhudi zake za ovyo za kushikilia utawala. Wakati wa mchakato rasmi wa uhakiki wa uchaguzi katika Bunge la Congress, wanachama 121 wa republican wamekataa kura zilizohisabiwa katika jimbo la Arizona, na 138 walikataa matokeo ya Pennsylvania. [2] Mchakato wa uhakiki ulichafuliwa kwa fujo zilizotekelezwa na waungaji mkono wa Trump, zilizoacha vifo vya watu 5. Picha za televisheni zikiangaza kote duniani zimeimarisha taswira ya Amerika ya kuwa ni dola ya kinyonyaji ya kirasilimali (banana republic) ambapo Trump mtu duni na kichaa anajaribu kwa papatiko kukwamia utawala.

Jambo jengine la kushangaza lilikuwa ni kuamiliwa vyema kwa waandamanaji wa Trump na askari polisi. Kama waandamanaji wangekuwa ni wanaharakati wa ‘maisha ya weusi yanathamani’ (black lives matter) au Waislamu wanaolalamikia kuhusu haki zao za kiraia, kuna shaka ndogo ya kuwa idara za utekelezaji wa sheria zisingewashambulia kwa risasi. Badala yake, waungaji mkono wa Trump wameachiwa njia nyeupe kusababisha ghasia na vurumai katika mahala ambapo maamuzi muhimu ya kiutawala hufanyika. Washirika wanaotegemea ulinzi wa Amerika wanapaswa kushughulishwa sana na nchi ambayo hutumia $718.69 bilioni kwa mwaka katika ulinzi, lakini imepoteza mji wake wa utawala kwa masaa kadhaa. [3]

Matukio ya wiki chache zilizopita pia yanatoa mwanga juu ya changamoto nyingi utakazokabiliana nazo utawala wa Biden katika jamii ya Wamarekani iliyogawanyika pakubwa na kuwafikia washirika wake walio na shaka. Watu milioni 74 wamempigia kura Trump—hesabu kubwa zaidi ya pili katika historia ya uchaguzi wa uraisi—ni Biden tu aliyevuna kura zaidi kufikia milioni 81. Trump amehakikisha kukubalika kwa kiwango cha asilimia 87 miongoni mwa wapiga kura wa republican na asilimia 6 miongoni mwa wana-democrat. [4] Zaidi ya hayo, asilimia 85 ya wana republican wanaamini kuwa uchaguzi uliibiwa na Biden hakuwa halali. [5] Hii ni mara ya mwanzo katika historia ya Amerika kuwa takriban asilimia 50 ya wapiga kura wako dhidi ya raisi mpya.

Chama cha Republican hivi sasa rasmi kimekuwa chama cha Trump. Yeye na waungaji mkono wake watakuwa na ushawishi muhimu juu ya siasa za Amerika siku za usoni. Pia itamaanisha kuwa wanasiasa wa Republican watalazimika kuendelea kuchukua madoido ya Trump na sera ili kupata kusimamisha wagombea, na kuhifadhi kiwango muwafaka cha ushawishi wa kifedha ili kushinda. Hii ndio sababu kwa nini wana-Republican wengi wameungana na Trump kubisha matokeo ya uchaguzi. Kwa muda wote hii itapelekea kuwa na jamii ya Amerika iliogawanyika zaidi—umbo la utu wa Jekyll na Hyde (tabia mbili ndani ya umbo moja).

Licha ya kuwa na wingi katika Congress na wingi wa kiufundi katika Senate (kwa sasa limegawika nusu kwa nusu na kura za Makamu wa Raisi zinaipa Democrats wingi mdogo), Biden atakutana na ugumu kupitisha ajenda za mageuzi yake muhimu ya ndani kuwa sheria. Sheria nyingi katika Congress kwa kweli huhitaji kura 60 katikaSenate kwa sababu ya miongozo ya kiutaratibu. Zaidi ya hayo, miswada ya upatanishi lazima ifuate mjumuiko wa masharti magumu yanayojulikana kama “Byrd Rule.” [6] Hii ina maana kuwa Biden atakumbana na ugumu kutekeleza mageuzi ya kimuundo kuhusiana na ahadi zake muhimu katika afya, elimu na ahadi nyengine. Kibaya zaidi, hatua yoyote dhidi ya malengo adhimu ya Republican itapelekea mapambano ya kimahakama katika Mahakama Kuu ambapo majaji wahafidhina wamewazidi wapenda maendeleo kwa 6 kwa 3. Au uwezekano mkubwa kwa Biden kukumbana na maandamano makubwa ya mitaani (Trump ameshafungua milango) ambapo itazorotesha hatua zozote kuelekea kwenye mageuzi ya kimuundo.

Kwa upande wa kimataifa, washirika na wadau wengine wa kimataifa huenda wakasita kuingia kwenye mikataba mipya. Matazamio ya Raisi mfano wa Trump baada ya miaka minne mbele kuweza kugeuza chochote ambacho Biden amejifunga nacho. Haya kwa hakika ndiyo aliyofanya Trump juu ya mafanikio adhimu ya kimataifa ya Obama. Kujitoa kwa Trump kutoka katika makubaliano ya JCPOA na kujitolea kudhibiti jitihada za Iran za mpango wa Nyuklia, na kuutupilia mbali Mkataba wa Paris juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa imewafanya washirika wengi kutilia shaka udumishaji wa dhamana wa Amerika juu ya makubaliano ya pande nyingi. [7,8] Endapo Biden ataingia kwenye mizozo ya nyumbani, na hamasa zikahama kuelekea kwenye Chama cha Republican, hamu ya washirika ya kuingia kwenye mipango ya muda mrefu pamoja na Raisi wa kipindi kimoja wa Democrats itapungua.

Kwa kweli, hali ya sasa ya mambo nchini Amerika imekaribisha makala nyingi mno juu ya mporomoko wa Amerika. Mwanzoni, wenye imani juu ya mporomoko wamehusisha kifo cha Amerika na matukio muhimu ya kihistoria kama kufaulu kwa chombo cha angani cha Urusi (Sputnik 1), mgogoro wa mafuta katika miaka ya 70, kuinuka kwa Japan na EU, vita vya Afghanistan na Iraq, na Mdororo Mkuu wa kiuchumi wa 2008. [9] Kuongezea mporomoko huu kuna wimbi jengine lililoletwa na janga la Covid-19 na mapinduzi baridi ya Trump. Ima kuporomoka kwa Amerika kuko karibu ama la, jambo moja ni hakika, kuwa Amerika sio tena dola kuu kama lilivyokuwa. Dunia inashuhudia kifo cha kasi cha siasa za Amerika, demokrasia na ukubwa wa kiulimwengu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:                                                                                                                                                  

   [وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ]

“Na kila ummah una muda wake. Utapofika muda wao basi hawatakawia hata saa moja, wala hawatatangulia.” (TMQ: 7:34)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Abdul Majeed Bhatti

Marejeo

[1] NPR, (2021). “Pelosi Asks Military To Limit Trump's Nuclear Authority. Here's How That System Works” [online] NPR. Available at: https://www.npr.org/sections/congress-electoral-college-tally-live-updates/2021/01/08/955043654/pelosi-asks-military-to-limit-trumps-nuclear-authority-heres-how-that-system-wor [Accessed 10 Jan. 2021].

[2] CBS News, (2021). “House rejects objection to Pennsylvania vote count” [online] CBS News. Available at: https://www.cbsnews.com/live-updates/electoral-college-vote-count-biden-victory/ [Accessed 10 Jan. 2021].

[3] Statista, (2019). “U.S. military spending from 2000 to 2019” [online] Statista. Available at: https://www.statista.com/statistics/272473/us-military-spending-from-2000-to-2012/ [Accessed 10 Jan. 2021].

[4] Gallup, (2020). “Presidential Approval Ratings -- Donald Trump” [online] Gallup. Available at: https://news.gallup.com/poll/203198/presidential-approval-ratings-donald-trump.aspx [Accessed 10 Jan. 2021].

[5] Eurasia Group, (2021). “Top Risks 2021” [online] Eurasia Group. Available at: https://www.eurasiagroup.net/issues/top-risks-2021 [Accessed 10 Jan. 2021].

[6] New York Times, (2021). “With New Majority, Here’s What Democrats Can (and Can’t) Do on Health Care” [online] New York Times. Available at: https://www.nytimes.com/2021/01/07/upshot/biden-democrats-heath-plans.html [Accessed 10 Jan. 2021].

[7] Reuters, (2018). “Instant View: U.S. withdraws from Iran deal” [online] Reuters. Available at: https://www.reuters.com/article/us-iran-nuclear-instantview-idUSKBN1I92UA [Accessed 10 Jan. 2021].

[8] BBC, (2020). “Climate change: US formally withdraws from Paris agreement” [online] BBC. Available at: https://www.bbc.com/news/science-environment-54797743 [Accessed 10 Jan. 2021].

[9] Common Dreams, (2020). “America’s Destructive Denialisms” [online] Common Dreams. Available at: https://www.commondreams.org/views/2020/12/18/americas-destructive-denialisms [Accessed 10 Jan. 2021].   

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 21 Januari 2021 15:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu