Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Je, Uislamu wa Kisiasa Umeshindwa katika Vuguvugu la Waarabu?

Januari 2021 imeshuhudia muongo mmoja wa maadhimisho ya Vuguvugu la Waarabu. Wakati madikteta wa muda mrefu wakiondolewa madarakani, pia tulishuhudia kuibuka kwa serikali mpya katika nchi kama Tunisia na Misri.

Katika mataifa yote mawili vyama vya Ikhwan al-Muslimina na Ennahdah vilishinda chaguzi na hivyo kufanya mwanzo wa zama mpya katika Mashariki ya Kati. Lakini baada ya muongo mmoja, vyama vyote haviko tena madarakani, katika jaribio lao kupata uhalali vyama vyote vilicheza na maneno matupu kwenye Uislamu mara tu walipopata madaraka na kupoteza mapenzi ya watu waliowaunga mkono katika kukaa madarakani.

Vyama vyote Ikhwan al-Muslimina na Ennahda vimeibuka washindi katika nchi zenye mfumo uliozungukwa ambapo watawala wamekuwa katika utawala kwa miongo kadhaa. Nchini Misri jeshi halisalimishi utawala, lakini limemuondoa aliyekuwa Jemedari wake Mkuu wa Anga aliye na miaka 82, lakini likabakisha udhibiti juu ya maslahi yake yote. Nchini Tunisia, Zine El-Abidine Ben Ali aliziimarisha idara za usalama wa ndani pamoja na chama chake na aliwakandamiza kikatili wapinzani wake wote wa kisiasa, wakiwemo pia wale anaotafautiana nao na kuupamba Uislamu kwa sura ya nje. Lakini katika nchi zote mbili, hakukuwa na safisha safisha iliofanyika licha ya Ikhwan al-Muslimina na Ennahdah kuwekwa kwenye madaraka na watu. Hosni Mubarak na Ben Ali walitumia idara za usalama wa ndani na ukandamizaji kubakia kwenye utawala, lakini katika nchi zote watu wametaka mifumo hiyo ipinduliwe. Lakini vyama vyote Ikhwan al-Muslimina na Ennahdah walitaka siasa za wastani, utekelezaji kivitendo na haja ya kutoihofisha jamii ya kimataifa. Watu walitaka mabadiliko halisi, Ikhwan al-Muslimina na Ennahdah walishikilia kubakisha hali kama ilivyo. Vyama vyote vikageuka kuwa si vyama vya kimapinduzi.

Ikhwan al-Muslimina na Ennahdah vililingania utawala wa Kiislamu na hivyo watu wakawapigia kura kushika madaraka. Lakini licha ya kuwa na uungaji mkono wa ummah vyama vyote viliendelea kufuata maafikiano na matokeo yake vimeendelea kuridhia kwa matumaini ya kupata uhalali. Ennahdah iliacha kufuata Shari’ah kuwa ndio chanzo cha uwekaji wake wa sheria katika katiba mpya na kutangaza kuwa inataka kubakisha mfumo wa kisekula wa taifa. Kiongozi wa Ennahdah, Rachid Ghannouchi, alisisitiza kuhusiana na usimamishaji wa Khilafah: “Bila shaka, sisi ni watu wa dola ya kitaifa. Tunahitaji dola kwa ajili ya mageuzi ya Watunisia, kwa ajili ya Dola ya Tunisia. Ama kwa suala la Khilafah, hili halina uhalisia. Suala la uhalisia leo hii ni kuwa sisi ni Dola ya Watunisia inayohitaji mageuzi, kwa hivyo itakuwa ni Dola kwa ajili ya Watu wa Tunisia, na sio dhidi yao.” Hivyo hivyo, Chama cha Ikhwan al-Muslimina kimekwenda mbali zaidi katika kuionyesha siasa yake ya wastani. Katika kufukuzia kupendezesha kile kinachoitwa rai za kimataifa, wameachana na msimamo wote wa kujifunga na serikali ya Kiislamu. Ilipokuja suala la kutumia misingi ya Kiislamu, wakataja vizingiti vya kikatiba na haja ya kutowaweka kando walio wachache. Lilipokuja suala la kutumia uchumi wa Kiislamu, wameelezea haja ya kuepuka kuwaogofya wawekezaji wa kimataifa na watalii. Moja kati ya jambo la mwanzo la Raisi Mohammed Morsi akiwa raisi wa Misri, lilikuwa ni kutuma taarifa rasmi ya kujifunga kwa Misri na mkataba wa amani na “Israel”! Miito yake ya mwanzo ya Uislamu iliondolewa kabisa kutoka matamshi ya Morsi mara aliposhika madaraka.

 

Vyama vyote, cha Ikhwan al-Muslimina na Ennahdah mara waliposhika madaraka, ilikuwa wazi kwamba hawakuwa na programu za kisiasa. Wote hao walipochukua madaraka, walizirithi nchi zilizoathirika na matatizo makubwa ya kiuchumi. Hata hivyo, vyama vyote vilikosa sera na havikuwa na muongozo wa kukabiliana na changamoto hizi. Tunisia ina ufinyu wa kiasili, ni nchi ndogo, yenye wakaazi milioni 11 na Pato ghafi la ndani GDP la $50 bilioni – dogo kuliko lile la mji wa Nigeria wa Lagos. Lakini umuhimu wa eneo la mwambatope la Tunisia katika bonde la Ghadames, linalokisiwa kuwa na ujazo wa futi trilioni 23 ambazo ni rasilimali ya gesi ya mwambatope inayorejesheka na mapipa bilioni 1.5 ya rasilimali ya mafuta ya mwambatope inayorejesheka inaendelea kutelekezwa. Serikali ya Ikhwan al-Muslimina ilifanya vibaya zaidi nchini Misri. Serikali ya Muhammed Morsi ilileta mfadhaiko mkubwa na kukosekana udhabiti nchini kutokana na utoaji wao wa maamuzi. Misimamo ya kisera ilichukuliwa na kisha kugeuzwa moja kwa moja kutokana na upinzani. Katika nchi zote hali ya kiuchumi na kijamii ilikuwa mbaya kutokana na kukosa kustawisha sera na baadhi ya wakati kukosa uwezo wa maamuzi ya papo kwa papo. Uhalisia ni kuwa, ikiangaliwa nyuma katika kipindi cha Ikhwan al-Muslimina na Ennahdah walipokuwa kwenye utawala, hawakuwa na misingi yoyote mbali ya kufanya mapatano na kuachana na miongozo ya Kiislamu. 

Katika nchi zote mbili Tunisia na Misri, Ikhwan al-Muslimina na Ennahdah vilikabiliana na mbinyo mkubwa kutoka kwa madikteta wa muda mrefu na idara za ujasusi. Vilikuja madarakani baada ya kuwashinda wapinzani wao waliojiimarisha na kuota mizizi. Wapinzani waliojinufaisha kutokana na uungwaji mkono kutoka kwa madikteta wa kisekula.

Nchini Misri, Ikhwan al-Muslimina muda wote ikiongoza katika hali ya udhalili na kushindwa kuwanyamazisha wapinzani licha ya kuwa na uungwaji mkono wa watu wengi. Wapinzani wa kisekula, maafisa wa zama za Mubarak, na tabaka teule la wafanya biashara hawakukubali kabisa ushindi wa kura wa Ikhwan al-Muslimina, dai lao kubwa lilibakia kuwa Morsi lazima ang'atuke. Matokeo ya kutowashughulikia vyema wapinzani, Ikhwan al-Muslimina ikaendelea kukumbana na upinzani wa kuendelea. Matokeo yake, watu muhimu katika wapinzani waliendeleza maandamano ya mara kwa mara kuudhoofisha utawala wa Morsi. Jaribio la Ennahda kukabiliana na upinzani Tunisia lilikuwa ni kupitia kuridhisha (wapinzani) na mapatano. Wakitaraji kuwa hili litawatuliza na kuimarisha nafasi yao. Lakini Ennahda ilipoteza uaminifu pamoja na waungaji wake mkono wengi kutokana na hili.

Waislamu walipata mamlaka katika Vuguvugu la Kiarabu katika baadhi ya nchi, lakini Uislamu haukupata, na katika fursa ya mwanzo utawala wa Kiislamu uliachwa ili kuwaridhisha wasekula kwa matumaini ya kupata uhalali. Wakati wengi ndani ya Tunisia na Misri wakitamani mabadiliko ya kweli, kwa muongo mmoja na zaidi matumaini haya yamebaki kuwa ni ndoto huku vyama walivyoviunga mkono vikikataa kuwapa kile walichokiahidi muda mrefu na ambacho watu walikipigia kura.

Kwa hivyo, haishangazi kuwa vyama vyote hivi, Ikhwan al-Muslimina na Ennahda havipo tena kwenye serikali. Utawala wa Kiislamu haukushindwa katika Vuguvugu la Waarabu, (bali) haukutekelezwa kabisa na watetezi wake kutokana na vipimo vyao vya muda mfupi, vipimo vya miamala yao, na vipimo vyao vya kisiasa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 25 Januari 2021 13:08

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu