Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urasilimali na Chakula

Mgogoro wa Chakula ni wa Kutarajiwa katika Mfumo wa Kirasilimali

Sehemu ya 1: Uhalisia wa Mgogoro wa Chakula

(Imetafsiriwa)

“Tunasikitishwa sana na jinsi vita vya Putin nchini Ukraine vimekatiza pakubwa silsila za usambazaji za kimataifa za chakula na kilimo, na tishio vinavyoleta kwa usalama wa chakula duniani. Tunatambua kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa zikitegemea chakula na pembejeo za mbolea kutoka Ukraine na Urusi, huku uchokozi wa Putin ukivuruga biashara hiyo.” (Taarifa ya Pamoja ya Ikulu ya White House ya Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Muungano wa Ulaya Ursula von der Leyen)

Mgogoro wa hivi punde wa chakula, bila ya kushangaza, unalaumiwa Mgogoro wa Ukraine. Dai hili lina kipande cha ukweli kwa- kupanda kwa bei ya mafuta na mbolea na kutatiza silsila za usambazaji wa chakula. Lakini itakuwa ni kusahilisha kupita kiasi kusema kwamba uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ndio uliosababisha ‘mgogoro huu wa chakula usio na kifani’.

Inaanza kuonekana kana kwamba baadhi ya watendaji wabaya wanachukua hatua kimakusudi ili kudhamini janga linalokuja la chakula duniani. Kila hatua ambayo wataalamu wa mikakati wa Utawala wa Biden wamekuwa wakifanya "kudhibiti mfumko wa bei ya kawi" inaharibu usambazaji au kuongeza bei ya gesi asilia, mafuta na makaa ya mawe kwa uchumi wa dunia. Hii ina athari kubwa kwa bei ya mbolea na uzalishaji wa chakula. Hilo lilianza kabla ya Ukraine. Sasa ripoti zinazunguka kwamba watu wa Biden wameingilia kati kuzuia usafirishaji wa reli wa mizigo ya mbolea katika kipindi muhimu zaidi cha upandaji wa masika. Kufikia vuli hii madhara yatakuwa ya kupindukia. (Chanzo: FoodSecurityPortal)

Kwa mara nyingine tena sote tunateseka kutokana na mvutano wa madaraka kati ya Dola za Kibepari. Na kama kawaida, ili kuhalalisha matendo yao dola hizi zinatengeneza simulizi inayosogeza umakini yetu mbali na matatizo ya kimfumo ndani ya Urasilimali na kuyaelekeza kwenye matukio ya mtu binafsi na wahusika wake.

Hatupaswi kupuuza mtindo unaofaa unaojitokeza na uchanganuzi wa hali kama hizi - kuchukua suala la kisiasa na kulilaumu kwa shida zinazotukabili. Inaondoa umakini wetu kutoka kwa shina la sababu na kutuelekeza kwenye tukio mahususi kwa wakati huu ili tuwe na matumaini kwamba mara tu suala hilo litakapotoweka, tatizo pia litaondoka – kamwe halitaondoka. Athari na matokeo yake yanaweza kupungua lakini hadi tu mgogoro mwingine (na daima kutakuwa na mgogoro mwingine) utakaporudisha kichwa chake mbaya.

Mfumo wa Kirasilimali una mapungufu makubwa sana. Daima umekuwa na dosari lakini matukio ya miaka michache iliyopita yameunda hali ambayo tunaweza kuona wazi nyufa zote zilizopo kwenye mfumo huu. Nyufa ambazo wanajaribu kuziziba ili kutuhadaa tufuate mfumo huu - mfumo ambayo kamwe, hauwezi na hautaweza kutupatia mahitaji yetu ya kimsingi, usalama na haki.

Mgogoro wa Kiuchumi ni sehemu ya maumbile ya Mfumo wa Kirasilimali, na vile vile mgogoro wa chakula. Sio kwa sababu hatuna chakula cha kutosha - ulimwengu unacho kingi - ni kwa sababu ya ukosefu wa usimamizi na ufikiaji.

Ni kweli kwamba baadhi ya matatizo haya hayaepukiki, yanatokana na jinsi ulimwengu ulivyounganishwa na maendeleo ya teknolojia.

Sio kwamba kuna uhaba wa vitu hivi ulimwenguni, ni kwamba vingi viko mahali pa makosa, vimehifadhiwa katika bandari za nchi zinazoagiza baada ya Uviko-19 vikilazimisha meli nyingi kutia nanga. Kadiri eneo la meli na kontena linavyopitia mchakato uchungu (wa polepole) wa kuoanisha usambazaji na mahitaji, gharama ya kuhamisha nafaka kati ya masoko makubwa imeongezeka zaidi ya maradufu kutoka viwango vya kabla ya janga hilo la maambukizi. Baadhi wanaregelea kupanda kwa wakati mmoja kwa gharama za chakula na mizigo kama "shangao maradufu" kwa mataifa yanayotegemea uagizaji wa chakula. (Chanzo: CSIS)

Lakini hiyo haimaanishi kwamba mgogoro huu ‘usio na kifani’ haukutarajiwa.

Katika miongo michache iliyopita kuenea kwa uhaba wa chakula kwa wastani au mkali kumeongezeka polepole. Kupungua kwa mapato na kukatizwa kwa silsila za usambazaji, njaa kali na ya muda mrefu iliongezeka kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na migogoro, hali ya kijamii na kiuchumi, hatari za kimaumbile, mabadiliko ya tabianchi na wadudu. Na yote haya yalitangulia janga la COVID na suala la hivi majuzi la Ukraine.

"Kadirio la ongezeko la uhaba wa chakula mwaka wa 2020 lilikuwa sawa na lile la miaka mitano iliyopita kwa pamoja. Takriban mtu mmoja kati ya watatu duniani (bilioni 2.37) hawakuweza kupata chakula cha kutosha mwaka 2020 - hilo ni ongezeko la karibu watu milioni 320 katika mwaka mmoja tu." (Chanzo: FAO)

Ulimwenguni, viwango vya njaa vinasalia kuwa juu sana. Mnamo mwaka wa 2021, vilivuka rekodi zote za awali kama ilivyoripotiwa na Ripoti ya Kiulimwengu kuhusu Migogoro ya Chakula 2022, huku takriban watu milioni 193 wakiwa na uhaba wa chakula—karibu watu milioni 40 zaidi kuliko wakati kiwango cha juu kilichofikiwa mwaka wa 2020. Mizozo na ukosefu wa usalama vinatambuliwa kama misukumo mikuu ya kuongezeka kwa uhaba wa chakula. (Chanzo: Benki ya Dunia)

Mnamo 2020, "takriban watu milioni 323.3 barani Afrika au 29.5% ya watu walikosa chakula au waliishi bila ya kula mwaka huo." (Chanzo: Shirika la Chakula na Kilimo)

"Nchi nane kati ya zinazokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula ziko barani Afrika, na kuathiri zaidi ya Waafrika milioni 81. DRC watu milioni 25.9, Afghanistan milioni 22.8, Nigeria milioni 19.5, Yemen milioni 19, Ethiopia kati ya milioni 14-15, Sudan Kusini milioni 7.7, Somalia milioni 6, Sudan milioni 6, Pakistan milioni 4.7, Haiti milioni 4.5, Niger milioni 4.4 na, mwisho, Kenya milioni 3.4” (Chanzo: Ripoti ya Kimataifa ya Mgogoro wa Chakula 2022)

Ni kweli kwamba suala la ukosefu wa chakula ni gumu sana kwani kuna mambo mengi yanayohusika katika kuwepo kwake.

Na kwa hivyo kutafiti katika mada hii hukutuma chini ya shimo la sungura la habari, uhalali, nadharia na uwezekano. Lakini unapokaa chini na kupekua habari, mambo machache huwa wazi mno, haraka sana.

Mfumo wa Kirasilimali hauangazii kulinda watu- umeundwa ili kuwanyonya. Na kwa hivyo wakati tuna chakula (au tuseme tuna njia za kuhakikisha kuwa kila mtu analishwa), sera ambazo dola za kibepari zimeweka husababisha takriban 8.9% ya idadi ya watu ulimwenguni - watu milioni 690 - kulala tumbo tupu kila usiku.

Mambo haya yanatambulika kuwa ya kudumu katika mfumo wa sasa- ilhali mara kwa mara, kuna ukosefu wa utunzaji, wasiwasi au maandalizi ili kuepuka mamilioni ya watu kufikia hatua ya baa la njaa- au kufa kutokana nayo.

"Kwa kweli kulikuwa na mazao mengi ya ngano katika kukabiliana ufungaji miji wa kuendelea. Hata hivyo, serikali nyingi zilichukua hatua kidogo kujenga au kupanua hifadhi zao za chakula.” Na matokeo yake hawakuwa wamejitayarisha kwa matatizo katika silsila za usambazaji. Hii ni pamoja na ukweli kwamba walikuwa na uzoefu wa awali na matatizo kama hayo (kutokana na natija ya Mapinduzi ya Kiarabu na matokeo yake ya umwagaji damu). Walipata fursa ya kutosha ya kuanzisha maghala mapya ya kitaifa- ambayo ni muhimu kwa sababu maghala yaliyotunzwa vizuri yanaweza kuhifadhi ngano na mahindi, miongoni mwa nyengine, kwa zaidi ya miaka 10. Watu binafsi wanaweza kupanua maisha haya ya rafu hadi miaka 31 chini ya hali zinazofaa. (Chanzo: Utafiti wa Kimataifa)

Kwa hakika, badala ya kulenga kuwalisha, sera za sasa zinaongeza gharama ya chakula kupitia mfumko wa bei, ambao unaongeza idadi ya watu wanaoanguka chini ya mstari wa umaskini ambao tayari unasikitisha na kuangukia kwenye baa la njaa.

“Duniani, bei za vyakula zimekuwa zikipanda tayari kwa muda na ongezeko hili si tu matokeo ya uhaba wa uzalishaji wa chakula, kama baadhi ya taasisi za Umoja wa Mataifa, nchi zinazouza bidhaa za kilimo nje ya nchi na mashirika ya biashara ya kilimo yalivyodai. Kinyume chake, inahusishwa zaidi na sababu kadhaa kama vile janga la UVIKO-19, kukatika kwa silsila za usambazaji, kurundikana mamlaka katika silsila za usambazaji, kupanda kwa bei ya kawi, kuongezeka kwa dhulma za kijamii na umaskini, pamoja na majanga ya tabianchi, ambayo yanazidishwa na ufadhili wa chakula na kilimo na uvumi.” (Chanzo: Wavuti ya Misaada)

"Kupanda kwa bei za vyakula kuna athari kubwa kwa watu katika nchi za kipato cha chini na cha kati kwa kuwa wanatumia sehemu kubwa ya mapato yao kwa chakula kuliko watu katika nchi zenye kipato cha juu." Katika sehemu fulani za Amerika ya Kusini na Afrika, huenda watu wakatumia hadi asilimia 50 au 60 ya mapato yao kununua chakula. (Chanzo: Benki ya Dunia)

Hali inafanywa kuwa ya kutisha zaidi jinsi kulivyo na uangalizi mdogo au wasiwasi.

"Mapema katika janga la maambukizi la virusi vya korona nchini Amerika, mahitaji yaliyopungua ya oda nyingi za bidhaa za maziwa yaliifanya sekta ya maziwa kumwaga maziwa mabichi, ambayo hayajasafishwa chini ya mifereji ya maji na kuyatupa nje. Wakati huo huo, vichinjio vingi vilifungwa kwa sababu ya mikurupuko ya UVIKO, ambayo ililazimisha mashamba mengi "kupunguza" mifugo yao, yaani kuua wanyama (kwa risasi au gesi ya CO2) na kutupa miili yao. Zaidi ya hayo, mapema katika janga hili la maambukizi, wakulima wa matunda na mboga walilazimishwa kutupa mazao hata ingawa hifadhi za chakula zilikuwa na uhitaji mkubwa wa chakula, kwa sababu serikali ilikataa kutoa msaada wa kifedha kufanya michango hiyo kutokea. Na karibu wakati huo huo, mkulima mmoja aliliambia jarida la ‘The Wall Street’ kwamba kwa kuwepo mvurugiko wa silsila ya usambazaji, badala ya kuyaacha mazao yake yafe shambani, alichagua kuyaharibu.” (Chanzo: GreenMatters

Biashara sio suluhisho - ndio kadhia yenyewe

"Mnamo tarehe 13 Aprili 2022, wakuu wa Benki ya Dunia, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, na Shirika la Biashara Duniani walitoa taarifa ya pamoja wakiitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhaba wa chakula, kuweka biashara wazi na kuzisaidia nchi zilizo hatarini, ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili ili kukidhi mahitaji ya haraka zaidi.” (Chanzo: Benki ya Dunia)

Hatupaswi kulitazama hili na kulipongeza kuwa limefanikiwa. Suluhu hizi si njia ya kuhakikisha kuwa watu kote ulimwenguni wanalishwa- ikiwa hilo litatokea, ni faida tu ya pembeni ambayo itasaidia kuwapa watu furaha.

Suluhu hizi ni njia tu ya kuhakikisha kuwa Mfumo wa Kirasilimali hauporomoki wenyewe - kwani mfumo wa sasa wa uchumi na nguvu ya dolari zinategemea mtiririko wa pesa kila wakati. Hii ni wazi kutokana na ukweli kwamba vikwazo vya biashara vilizidisha mgogoro wa chakula kwa kupandisha bei ya ngano kwa 30%. (Chanzo: Benki ya Dunia)

"Ikiwa nchi nyingi maskini bado zingali hatarini sana, ni kwa sababu usalama wao wa chakula unategemea sana uagizaji wa chakula kutoka nje ambao bei yake inazidi kuwa juu na tete". Taarifa iliyotolewa na Olivier de Schutter, ripota maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula (Chanzo: BMC)

"Nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati huagiza zaidi ya asilimia 90 ya chakula chao,  huku Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ikijivunia bili ya kila mwaka ya dola bilioni 45 ya uagizaji chakula." (CSIS)

Kutokana na hali hiyo, nchi hizi zinalazimika kukabiliana na mifumo ya uzalishaji wa ndani ambayo imekuwa dhaifu katika miongo kadhaa iliyopita na sasa zinategemea sana uagizaji wa chakula kutoka nje, hasa ngano kutoka Ukraine na Urusi, na kuvifanya vita na kupanda kwa bei kuwa sababu kuu ya kuyumbisha.

Takwimu hizi zinafanywa kuwa za kutisha zaidi kwa ukweli kwamba mataifa ya Afrika yana hekta nyingi za ardhi yenye rutuba na ardhi ya kilimo, pamoja na mifumo mingi ya maji. Lakini licha ya hili, mataifa mengi barani Afrika yako mbali zaidi na kuweza kulisha wakaazi wake kupitia uzalishaji wao wenyewe wa chakula kuliko ilivyokuwa miaka ya 1960 na 1970.

Badala ya kutumia rasilimali hizo, wanatumia pesa kuagiza bidhaa kutoka nje na kuzuia uwezo wao wa kukuza uwezo wao wa kuondoa umaskini na uhaba wa chakula uliopo katika bara zima.

"Bili ya kila mwaka ya uagizaji chakula wa Afrika ya dolari bilioni 35, inayokadiriwa kupanda hadi dolari bilioni 110 ifikapo 2025, inadhoofisha uchumi wa Afrika, inapunguza kilimo chake na kusafarisha nje ajira kutoka bara hili." (Chanzo: Utafiti wa Kiulimwengu)

Haya Hayakufungika tu kwa Afrika

Leo, zaidi ya nchi 95 ulimwenguni huagiza chakula zaidi kuliko wanachozalisha. Wauzaji nje wanne wanaoongoza ni Marekani, Canada, Australia na Argentina na wanatoa takriban asilimia 80 ya mauzo ya nafaka kwenye soko la dunia. Lakini ili kuagiza bidhaa kutoka nchi hizi, dunia nzima lazima iwe na mtaji wa kununua chakula hiki. Hili linafanywa kuwa gumu zaidi kwani nchi zinazosafirisha nje zinazidi kuwa na ulinzi na nchi zinazoagiza zinakuwa na matatizo na thamani ya sarafu zao. (Chanzo: APCSS).

Kwa hivyo, mzunguko wa biashara na sera zinazohusika zinakusudiwa kupunguza uwezo wa ulimwengu unaoendelea wa kujitegemea. Endapo mwelekeo wa nchi zilizoendelea ni kuboresha afya na ustawi wa watu katika nchi kama vile Afrika, kwa nini zisizipe pesa za kuendeleza uwezo wao ambao hawajatumika badala ya kuzizika kwenye madeni? Na kushajiisha hali ambapo ni lazima ziagize kutoka nje rasilimali ambazo wangeweza kuzalisha kwa urahisi.

Lakini badala ya kuzisaidia nchi hizi, zilizifanya zitegemee pembejeo kutoka nje. Ziling’ang’ana kiuchumi kudumisha uagizaji huu na wakati mgogoro wa mafuta na mgogoro wa madeni ulipotokea katika miaka ya 1970 na 1980, ilibidi waombe vifurushi vya mkopo kutoka kwa taasisi za fedha za kimataifa. Mikopo hii ilikuja na masharti kwa umbo la sera za marekebisho ya kimuundo, ambayo ilisababisha ukombozi kwa upande mmoja na ubadilishaji wa uzalishaji wa ndani wa kilimo kwa mauzo ya nje kwa upande mwingine. Sera hizi pia zilihusisha kuondoa uingiliaji kati wa umma katika sekta ya kilimo, ikiwa ni pamoja na taasisi zinazoongozwa na serikali kama vile bodi za masoko, ambazo hapo awali zilisaidia wakulima wadogo kupitia mikopo, pembejeo na kuwezesha upatikanaji wa soko. Marekebisho ya kimuundo pia yameshajiisha mrundiko wa biashara na uzalishaji wa kilimo, ambao haujumuishi wakulima wadogo katika biashara na ukuaji. Haya yote yalizua hali ambapo walikuwa tegemezi kwa mikopo...

Na makampuni ya kimataifa yanaifanya hali nzima kuwa ya matatizo zaidi kwa kuzidisha vibaya mgogoro wa chakula na kupandisha bei ya vyakula.

Mara nyingi tunasikia kwamba makampuni ndani ya sekta ya kibinafsi yana ushawishi mkubwa lakini wengi wetu hatuzingatii hii inamaanisha nini.

"Kilimo cha kutumia kemikali ambacho Umoja wa Carbide (shirika la kemikali la Marekani) ilikipigia debe, sasa tunaweza kuona athari (hasi nyingi mno) ... Na bado - iwe inahusisha mbinu mpya za uhandisi wa kijeni au dawa zaidi za wadudu - kuna msukumo usio na mwisho wa mashirika ya teknolojia anuwai ya kilimo ili kuimarisha zaidi mtindo wao wa kilimo kupitia kuharibu mbinu asili za kilimo kwa lengo la kuwaweka wakulima zaidi kwenye vinu vya ushirika vya mbegu na kemikali. (Chanzo: Utafiti wa Kimataifa)

Na wanasaidiwa na katika jaribio lao la kudhibiti silsila za usambazaji, na kupata faida kwa gharama ya maisha ya watu.

"Suluhu" zilizowekwa na mashirika ya kimataifa (kama Benki ya Dunia na WTO) zimejikita katika sera na teknolojia zilezile ambazo zilizua tatizo tangu mwanzo: kuongezeka kwa msaada wa chakula, kupunguza udhibiti wa biashara ya kimataifa ya bidhaa za kilimo, na marekebisho zaidi ya kiteknolojia ya kijeni. Hatua hizi zinaimarisha tu hali halisi ya mashirika kudhibiti chakula cha ulimwengu. (Chanzo: FoodFirst)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu