Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Haiba ya Kimataifa Inapatikana kupitia Kuwatumikia Maadui wa Uislamu?

(Imetafsiriwa)

Shirika la Anadolu katika makala, "Mamlaka ya Uturuki katika uwanja wa kimataifa yanaongezeka," linatoa mukhtasari wa hotuba ya Rais wa Uturuki Erdogan kwa wawakilishi wa chama tawala cha Haki na Maendeleo.

"Katika miaka ya hivi karibuni, mamlaka ya Uturuki katika uwanja wa kimataifa yamekuwa yakiongezeka kwa kasi. Hayo yamesemwa na Rais Recep Tayyip Erdogan katika mkutano na wawakilishi wa chama tawala cha Haki na Maendeleo jijini Ankara.

Kulingana na rais huyo wa nchi, Uturuki ya leo inatetea kwa uthabiti maslahi yake ya kitaifa kwenye majukwaa yote, ikiwemo UN na NATO.

Kiongozi huyo wa Uturuki alibainisha kuwa nchi hiyo inafanikiwa kufikia matokeo yaliyokusudiwa, huku ikitekeleza diplomasia yenye ufanisi.

Rais Erdogan pia aliongeza kuwa kutokana na sera zinazofuatwa na mamlaka katika miongo miwili iliyopita, Uturuki imekuwa "nchi ya kidemokrasia zaidi na huru, nchi yenye fursa sawa." Chanzo: (Shirila la Anadolu)

Bila shaka, dori ya Uturuki katika kutatua matatizo mengi ya kieneo na kimataifa imeongezeka sana. Hii inaonekana kupitia ushiriki changamfu wa Uturuki katika matukio ya Syria, Libya, Nagorno-Karabakh, Afghanistan, Ukraine na maeneo mengine. Lakini, ushiriki huu ufungwa na dori ya mpatanishi na mtekelezaji pekee, lakini sio kama mtu mwenye kuamua mkakati na kufanya uamuzi.

Je, ni ukuaji upi wa haiba ya Uturuki katika uwanja wa kimataifa anaozungumzia Erdogan, ambaye sera yake ndani ya Uturuki yenyewe imegeuka kuwa mgogoro mwingine mkali? Makadirio ya Chama cha Haki na Maendeleo kinachoongozwa na Erdogan yalishuka hadi kiwango cha chini kiasi kwamba kikalazimika kuunda muungano wa wabunge kwa jina Muungano wa Watu, kikiunganishwa na Harakati ya Kitaifa ya mrengo wa kulia.  Na wakati huo huo, alitangaza baadhi ya harakati za Kiislamu kuwa ni zenye misimamo mikali na za kigaidi na kuanza kuwatesa kikatili, hata wale ambao alipitia mabegani mwao kuingia madarakani.

Mtu yeyote na asishangazwe na maneno ya Erdogan, ambaye, kwa kukurupuka kiujinga, anakadiria, labda, kuwa ndio tumaini la pekee la ulimwengu wa Kiislamu, kwamba wakati wa utawala wake Uturuki imekuwa nchi ya kidemokrasia zaidi. Yote tisa, kumi Uturuki ya kisasa ni jamhuri ya kisekula iliyoundwa juu ya magofu ya Khilafah ya Kiuthmani, iliyovunjwa na mikono ya kibaraka wa Uingereza Mustafa Kemal. Na Erdogan, aliyeingia madarakani chini ya pazia la "mwanasiasa wa Kiislamu na mwanamageuzi", kupitia kukiri kwake mwenyewe, ni mlezi mwaminifu wa vima na maadili ya jamhuri, ambayo ni usekula na utaifa wa Kituruki.

Tangu kuanzishwa kwake hadi leo, sera ya serikali tawala ya Uturuki, pamoja na nchi nyingine za Kiislamu, ambazo mipaka yake, katiba na muundo wao wa kisiasa huamuliwa na wakoloni wa Magharibi, zina majukumu mawili pekee.

Kwanza, kuzuia maendeleo ya Umma wa Kiislamu na kuregea kwake katika mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu, kwa kupotosha na kubadilisha imani na hisia zake za Kiislamu kwa fikra za usekula, uzalendo, utaifa nk.

Jambo la pili ni kutumikia kwa utiifu maslahi ya dola kuu za kirasilimali katika mapambano yao ya ushindani wa kuitawala dunia, kutumia mali na maisha ya Waislamu kama bidhaa ya bei nafuu.

Erdogan bila aibu anajigamba ushiriki wa Uturuki katika shughuli za miundo ya kisiasa inayochukia Uislamu, ikiwemo Umoja wa Mataifa na NATO, akiitaja kuwa ni ulinzi wa maslahi ya taifa. Wakati mashirika haya si chochote zaidi ya zana za kuhifadhi utawala wa mfumo wa kirasilimali katika uwanja wa kimataifa, ukiongozwa na Marekani, iliyoketi kileleni mwa siasa za dunia kufuatia matokeo ya Vita vya Pili vya Dunia. Linapokuja suala la kulinda dini, heshima na maisha ya Waislamu, Erdogan anajifunga tu na kumwaga machozi hadharani na kauli tupu zinazotikisa upepo.

Utawala wa Uturuki, ukiongozwa na Erdogan, umecheza dori muhimu katika kuyanyonga mapinduzi ya Waislamu wa Syria dhidi ya udikteta katili wa kibaraka wa Marekani Assad, kuwashawishi na kuwahonga makamanda wengi wa waasi kwa fedha na ahadi za uongo kwenye meza makongamano tofauti tofauti ya "marafiki wa Syria", nk. Chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa, kando na jeshi la ISAF la Uturuki kushiriki katika uvamizi na miaka ishirini ya kuikalia Afghanistan. Uturuki pia inaendelea kupigia debe uhamisho wa ushawishi wa Ulaya katika koloni za zamani za Afrika na ushawishi wa Urusi katika dola za zama za baada ya Usovieti za Caucasus na Asia ya Kati kwa niaba ya Marekani.

Uturuki haikusimama kando wakati wa uvamizi wa sasa wa Urusi dhidi ya Ukraine, ambayo ilitumika kama sababu ya kuanzishwa kwa vikwazo vikali dhidi ya Urusi ambavyo viligonga kwa uchungu maslahi ya kiuchumi ya nchi za EU, ambazo zinategemea sana usambazaji wa rasilimali za nishati za Urusi. Ikiuza aina za kisasa za silaha kwa Kyiv, Ankara wakati huo huo inaendelea na ushirikiano wa karibu na Moscow, ikiwemo kununua kutoka kwake mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga yenye thamani ya mabilioni ya dolari za Marekani.

Hotuba ya Erdogan inashuhudia kwamba yeye, mithili ya vibaraka wengine walioketishwa na wakoloni wa Kimagharibi juu ya shingo za Umma wa Kiislamu, anapima mafanikio kwa kiwango cha usaliti wa maslahi ya Uislamu na Waislamu kwa ajili ya kutumikia maslahi ya maadui wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, mtu yeyote na asihadaike na uchaji Mungu wa kujifanyisha na hotuba za uwongo za madhalimu waovu walionyakua utawala. Yote tisa, kumi hili halitageuka kuwa chochote kwao, isipokuwa fedheha na adhabu kali itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[بَشِّرِ ٱلْمُنَٰفِقِينَ بِأَنَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا * ٱلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ ٱلْكَٰفِرِينَ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ ٱلْعِزَّةَ فَإِنَّ ٱلْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]

Wabashirie wanaafiki kwamba watapata adhabu chungu, Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [4:138-139].

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliuita Umma wa Muhammad (saw) kuwa ni umma bora uliopo kwa manufaa ya wanadamu wote, akataja kabla ya kumuamini Yeye, wajibu wa Waislamu kuamrisha mema na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa. Kutokana na Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na makhalifa waongofu (ra) inajulikana kuwa njia ya kufanya hivyo ni kuwaunganisha Waislamu chini ya uongozi wa Khalifa mmoja, anayetabikisha sharia, katika sera ya ndani ya dola pamoja na katika kiwango cha mahusiano ya kimataifa.

Kwa kuwa kuwepo kwa jamii katika Uislamu hakupimwi na uchamungu wa watu binafsi kipeke yao na wingi wao, bali kwa ubwana wa ada na kanuni za Sharia ndani yake.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ]

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [3:110].

Mamlaka ya kimataifa bila shaka yataregea kwa Umma wa Kiislamu kwa kuregeshwa kwa dola moja ya Kiislamu katika muundo wa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya utume. Kupitia kuugeuza Uislamu kuwa mfumo wa kisiasa, Umma wa Kiislamu utaregea katika uga wa kimataifa kama raia kamili na nguvu yenye ushawishi mkubwa yenye uwezo wa sio tu kulinda maslahi yake, bali pia kuonyesha njia ya wokovu na maendeleo kwa wanadamu wote. Na itakuwaje vyenginevyo, kwa sababu nguvu na ushawishi wake utatokana na uongozi wa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi Mwenye Nguvu na Mwenye hekima, na sio kutokana na maazimio ovyo na maovu ya pote la wanafiki na wapagani. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَجَعَلَ كَلِمَةَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلسُّفْلَى وَكَلِمَةُ ٱللَّهِ هِىَ ٱلْعُلْيَا وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

na akalifanya neno la walio kufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima.” [9:40].

Uadilifu wa mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa Kiislamu, unaotabikishwa na Khilafah, utaurudisha Umma wa Kiislamu kwenye nguvu zake za zamani. Kama ilivyokuwa hapo awali, neno moja kutoka kwa Khalifa litatosha kukomesha mashambulizi yoyote dhidi ya Waislamu na maadili yao kutoka kwa makafiri. Majeshi ya Mujahidina yatakomboa ardhi za Kiislamu na kuangamiza vizuizi vya vyama vya kitaifa na kieneo vilivyoanzishwa na wakoloni. Wakiungana ndani ya dola moja, chini ya bendera za LA ILAHA ILLA ALLAH MUHAMMAD RASULULLAH, Waislamu wataeneza nuru ya Uislamu kwa watu kote duniani, wakiulingania kupitia diplomasia na jihad yenye ufanisi.

[هُوَ ٱلَّذِى أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِٱلْهُدَى وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِٱللَّهِ شَهِيدًا]

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.” [48:28]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abu Ibrahim Bilal

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu