Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uturuki Imetawaliwa na Mfumo wa Mafia kwa Miaka 100

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Chama cha AK imejikita katika mkutano wa Biden-Erdogan utakaofanyika Brussels, ambao Rais Erdogan amekuwa akiungojea kwa miezi kadhaa kwa matumaini makubwa. Kwa sababu mkutano huu utaonyesha picha ya wazi ikiwa Erdogan atabakia madarakani kwa muhula mwingine au la. Erdogan anashangaa juu ya hili kuliko Umma wa Uturuki, na analijua vizuri. Sera ya utawala wa Biden kukandamiza China, sera yake ya kuidhibiti Urusi na utaratibu mpya utakaoamua katika maswala muhimu ya Mashariki ya Kati ni ya muhimu sana kwa Uturuki. Kwa sababu serikali ya Chama cha AK na Erdogan wanaweza kutoa ujasiri maadamu wataendelea na sera hizi mpya na mabadiliko katika tabia ya utawala wa Biden. Vinginevyo, ikiwa utawala wa Biden hauwezi kuona nguvu ya kutosha kutoka kwa Erdogan naye Erdogan hawezi kutoa imani hii kwa utawala wa Amerika, serikali ya Chama cha AK na Erdogan zitakuwa na wakati mgumu mbeleni katika uhusiano wao na utawala wa Amerika hadi kufikia uchaguzi wa 2023.

Wakati hali ni hii kwa upande wa uhusiano wa Amerika na Uturuki, kwa upande mwingine, kuna ajenda nyingine katika siasa za ndani Uturuki ambazo zina muumiza kichwa Erdogan. Kama mnavyojua, ajenda ya Uturuki ilikuwa imetikisika kwa mwezi uliopita na taarifa iliyofichuliwa na Sedat Peker, kiongozi wa kikundi cha uhalifu, kuhusu uhusiano wa serikali na Kikundi cha Mafia. Sedat Peker anatoa taarifa ambazo zinawalenga Waziri wa Mambo ya Ndani Suleyman Soylu, Waziri Mkuu wa zamani Binali Yildirim, Waziri wa zamani wa fedha na pia mkwewe Erdogan Berat Albayrak na baadhi ya manaibu wa Chama cha AK kwenye video zake zilizotumwa kutoka Imarati. Madai mengi yanatolewa, kutoka biashara ya dawa za kulevya hadi utapeli wa pesa, kutoka biashara ya mafuta na silaha huko Syria hadi katika zabuni kubwa za kimagendo nchini Uturuki. Kwa kufanya hivyo, Peker pia alifichua uhusiano mchafu wa zamani na wa sasa wa serikali na Mafia nchini Uturuki. Ukiangalia majina yaliyolengwa na Sedat Peker katika taarifa zake, inaweza kueleweka wazi kuwa mlengwa halisi ni Erdogan. Kwa kuzingatia ukweli kwamba Peker alikuwa akishtakiwa katika kesi za Ergenekon katika miaka iliyopita na kwamba ana viashiria vya uwanaharakati mpya, inaweza kusemwa kuwa inaaminiwa kuwa Uingereza hutumia matakwa haya ya kibinafsi ya Peker. Kushindwa kwa serikali ya Chama cha AK kupambana na janga hilo na mzozo wa uchumi, kutokuwa na uhakika katika uhusiano wa Uturuki na Amerika, na kupungua kwa uwezo wa kupiga kura wa miungano ya watu kunaonekana kutia hamasa vyama vinavyounga mkono Uingereza. Mnamo Juni, baada tu ya matokeo ya mkutano wa Erdogan-Biden, tunaweza kutathmini wapi mchakato huo ufafikia, ni uharibifu kiasi gani serikali ya Chama cha AK na Erdogan watapata katika hili.

Kuhusu uchafu wa zamani wa uhusiano baina ya serikali na mafia; kwa kweli, hakuna kilicho badilika tangu jana. Kwa kweli, historia ya zamani ya jamhuri ya Uturuki ni chafu sana na uhusiano wa serikali na mafia hivi kwamba haijalishi kwa serikali mpya kujionesha kuwa safi, bila kujali ni kiasi gani inasema kwamba imeiondoa nchi kutoka kwa amri ya mafia na “operesheni mikono safi”, haijalishi kwa namna gani, kwa namna fulani pia inaunda utaratibu wake mchafu wa Mafia. Kwa mfano, wakati Chama cha AK kilipoingia serikalini, moja ya sera yake mashuhuri zaidi ilikuwa “kuindoa Uturuki kutoka miaka ya 1990 na kufanya kazi ili isirudi miaka hiyo ya nyuma”.Shukrani kwa ushirikiano wake na kikundi cha Gulen, alifanya operesheni kwa vikundi vyote vya mafia vya miaka ya 90. Hata hivyo, Erdogan na Gulen wameweka vikundi vyao wenyewe ambapo mafia wa zamani wametoka. Tofauti pekee kati yao ni kwamba kipindi cha zamani vikundi vya mafia vilikuwa na sura ya vikundi vya uhalifu wa wazi na watu majangili, wakati kipindi kipya cha mafia kilifanya kazi na tabia na njia tofauti. Baada ya mapigano kati ya Erdogan na Gulen yaliyoanza mnamo 2013 na jaribio la mapinduzi mnamo Julai 15, mafia wa Gulen, ambao wametapakaa katika maeneo yote ya serikali, waliondolewa, na mwanya huu ulijaribiwa kuchukuliwa na vikundi vya kimafia na wahalifu wa miaka ya 90. Kwa maneno mengine, uhusiano wa serikali na mafia umekuwepo na kuendelea kuwepo nchini Uturuki. Kwa sababu shida hii inasababishwa na mfumo wa kibepari wa kisekula ambao Uturuki inakaa juu yake.

Jamuhuri ya Uturuki sio nchi ya sheria, Uturuki ni nchi ambayo jina lake limekuwa likinasibishwa na mauwaji yasiopatiwa ufumbuzi, mauwaji ya kisiasa na matukio ya kinyume na sheria tokea zamani hadi sasa. Na inafanya kazi hizi na vikundi vya mafia vyenye uhusiano navyo. imefanya hivyo hapo zamani, inafanya leo, na itaendelea kufanya hivyo kesho. Serikali hubadilika, vyama hubadilika, hata mfumo wa serikali hubadilika, lakini utaratibu huu mchafu, utaratibu huu wa kimafia haubadiliki. Ili kumaliza utaratibu huu mchafu, ni lazima kusafisha kabisa. Usafishaji ambao hautaacha mabaki ya mfumo huu wa kisekula. Njia pekee ya kuondoa utaratibu huu uliooza, njia pekee ya kuokoa nchi hii kutoka kwa mafia, vikundi vya uhalifu na ugaidi, ni kuunda mfumo sahihi. Mfumo huo ni mfumo wa Kiislamu, na dola itakayotekeleza mfumo wa Kiislamu ni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Afisi Kuu Ya Habari Hizb Ut Tahrir na  

Mahmut Kar

Mkuu Wa Afisi Ya Habari Hizb Ut Tahrir Wilaya Ya Uturuki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu