Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ni Mauwaji Nchini India

(Imetafsiriwa)

Ninaandika kutoka mji mkuu wa India, Delhi ilhali nikiendelea kupata nafuu ya ugonjwa wa Uviko-19. Ni ngumu kuelezea kile tunachokishuhudia ndani ya India. Ugonjwa umeenea hewani na vifo vimetapaka kila mahali.

Kwa wiki sasa India inaweka rekodi mpya ya kiulimwengu kila siku kwa ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na Uviko-19. Zaidi ya visa vipya takribani 400,000 vimeripotiwa mara kwa mara, huku idadi isiyo rasmi ikitarajiwa kuwa kubwa zaidi.

Jijini Delhi, Uviko-19 imegusa karibu kila kaya. Ndugu zangu watatu katika familia yangu hivi sasa wamekutwa na Uviko-19 pamoja na jamaa wa karibu wakiwa katika hali mbaya wakipumua kwa msaada wa oksijeni. Wiki moja tu iliyopita Mama yangu mlezi alikutwa na Uviko na siku chache baadaye viwango vyake vya upumuwaji vilianza kushuka. Aliweza kuwekewa vifaa vya upumuwaji takribani kwa muda wa masaa sita huku akitaabika. Kwa sasa ni mahututi na amelazwa hospitalini.

Kila wakati simu inalia au taarifa yoyote itaingia, tunaogopa kama kutakuwa na taarifa yoyote kutoka kwa jamaa, marafiki, au tunaofahamiana nao juu ya mtu aliyetutoka na hiyo ndio hali kwa mamilioni ya watu hapa. Sote tunahuzunika! Facebook, WhatsApp, Twitter zote zimekuwa vyombo visivyo rasmi vya msaada kuhusu Uviko-19. Watu wanaomba kupitia mitandao ya kijamii kupata msaada.

Ukubwa wa uharibifu ungeliweza kufahamika kwa ukweli kwamba watu matajiri pamoja na wale waliokaribu na utawala wamekuwa wakitoa ujumbe wa SOS kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya msaada. Wanafanikiwa kupata msaada lakini hilo sio linalohitajiwa na mamilioni ya watu. Wengi hapa wanaomba mitungi ya oksijeni na vitanda hospitalini  kwani wengi wanakufa mitaani na katika milango ya hospitali kwa kushindwa kupumua. Mapambano hayaishii katika kupata vitanda na vifaa vya upumuaji hospitalini, hali ni mbaya sana hapa hata hospitali kubwa zinatuma ujumbe wa SOS kwa serikali ili waweze kuwaongezea vifaa vya usambazaji wa oksijeni. Katika kipindi cha wiki moja, zaidi ya wagonjwa 60 katika hospitali tatu kubwa binafsi hapa Delhi wamekufa kwa sababu ya kuishiwa na oksijeni. Mnamo tarehe 4 Mei, hospitali 41 hapa Delhi zimetuma ujumbe wa SOS kwa serikali. Hii ndio hali ya mji mkuu wa taifa la India. Kinachotokea katika miji midogo ni mbaya zaidi.

Katika hospitali nyingi, watu wanalazimika kusaini fomu na kukubaliana kwamba endapo mgonjwa atakufa kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni haitakuwa dhima ya hospitali au serikali. Hospitali nyengine zimewaagiza wagonjwa kutafuta vifaa vyao wenyewe vya upumuaji. Idadi rasmi ya vifo kwa siku ni takribani 4,000 lakini kutokana na waandishi wa habari na watu wanaofanya kazi hospitalini wanasema idadi halisi ya vifo vya kila siku ni zaidi ya 40,000, mara kumi zaidi ya kile kinachoripotiwa na serikali.

Maiti zimejaa; maeneo ya kuchomea maiti yameisha. Mazishi sasa yanafanyika katika mbuga. Miti inayotumiwa katika kuchomea maiti inapungua kwani kuna maiti nyingi zaidi kuliko idadi ya kuni kwenye vituo vya kuchoma maiti. Idara ya misitu imelazimika kutoa idhini maalumu ya kukata miti kwa ajili ya kuchomea maiti. Watu wanakufa bila ya kupata matibabu yoyote na kwa sababu ya ukosefu wa kitu cha msingi kama oksijeni, hii ni dhahiri shahiri kuwa serikali inafadhili mauwaji. Ni kama vile sadaka ya mauwaji imetuangukia kwetu watu wa India.

Watu Bilioni walisukumwa kwenye Maangamizi

Mnamo tarehe 24 Machi 2020, Waziri Mkuu Narendra Modi alitangaza masharti magumu ya ufungaji miji ulimwenguni ambayo ilidumu kwa miezi kadhaa na taarifa ya masaa manne tu na huku serikali ikikosa mpango wa namna gani itakabiliana na ufungaji wa ghafla wa uchumi. Ufungaji miji huu usiotarajiwa ulisababisha machafuko baina ya mamia ya mamilioni ya watu, haswa kwa wale wenye vipato vya chini, walipoteza kazi zao ndani ya usiku mmoja na kuachwa wamekwama barabarani bila chakula au njia yoyote ya kuwasaidia kurudi vijijini kwao. Hii ilisababisha uhamaji mkubwa wa wafanyakazi-wahamiaji huku mamia ya watu wakifa njiani na maelfu kufa kwa njaa. Huu ni mtazamo tu wa demokrasia kwa upana wake ulimwenguni ambayo imewaangusha vibaya watu wake kwa kiwango cha juu.

Wimbi la kwanza lilifichua kwamba miundombinu yetu ya huduma ya afya imesambaratika, madaktari walikuwa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa PPE na barakoa. ili kushughulikia Uviko miundombinu maalumu ilijengwa na, mamilioni ya pesa zilikusanywa kwa jina la mfuko wa ‘PM CARES’. Mwaka mmoja baadaye hakukuwa na utayari wa kukabiliana na Uviko unaoweza kuonekana mahali popote. Watu wanaomba vitanda vya hospitali, dawa na hata oksijeni!

Wimbi la kwanza liliathiri vibaya India (India ilikuwa nchi ya tatu iliyoathiriwa vibaya) na kisha ikapungua. Licha ya  maonyo ya mara kwa mara kutoka kwa wataalam kuhusu wimbi la pili, mnamo Januari 2021 katika Kongamano la Uchumi Duniani (WEF), Waziri Mkuu Modi alitangaza ushindi dhidi ya virusi vya korona. kupambana na UVIKO haikuwa shida kubwa kwa serikali, na ni dhahiri kabisa kuwa ukweli ni kwamba hawakufanya chochote kwa mwaka mzima kujiandaa na wimbi la pili. Mwanzoni mwa Machi 2020, baraza la wanasayansi, lilionya serikali juu ya aina mpya ya kirusi cha korona, lakini serikali haikusikiliza na ikawaacha watu zaidi ya bilioni 1.3 kwa huruma ya kinga zao za mwili kujilinda dhidi ya ugonjwa hatari wa kuambukiza.

Katika demokrasia, wasiwasi mkubwa kwa chama chochote cha siasa ni kuingia madarakani. Katika jamii yenye ujamaa sana nchini India, chama tawala kinajua kwamba wataendelea kushinda chaguzi maadamu wataendelea kushinikiza ajenda yao ya Ubaniani. Kwa hivyo, hata katikati ya wimbi la pili, wakati kesi za Uviko-19 zilikuwa zikiongezeka, na kufikia zaidi ya watu 200,000, Waziri Mkuu mlaghai alikuwa akifanya shughuli nyingi za mikutano ya uchaguzi na mamia na maelfu ya watu ambao hawakuvaa barakoa huku waliohudhuria wakikosa kuweka umbali wa kijamii. Jijini Kolkata, mji mkuu wa Bengal Magharibi ambapo mikutano ya uchaguzi ilifanyika, kila mtu  aliyepimwa, alikuwa ameambukizwa UVIKO. Bengal Magharibi inatarajiwa kuwa eneo jipya kinara kwa Uviko.

Hata baada ya ongezeko kubwa la visa vya Uviko, Kumbh Mela (Mkusanyiko wa kidini ya kibaniani) uliweza kuandaliwa mnamo Aprili ambapo mamilioni ya watu walikusanyika pamoja kuoga katika mto Ganges. Wengi wa warioregea kutoka Kumbh walipata maambukizi ya Uviko. Mkutano wa Kumbh Mela na mikutano ya uchaguzi ilithibitika kuwa hafla kubwa zilizoweza kueneza Korona, hii ni tofauti na kile kilichotokea katika Tablighi Jamaat (ambao walidhalilishwa na kuandamwa kwa miezi), chombo kikuu cha habari hakija weza hata kukosoa mikutano mikubwa ya uchaguzi na melas katikati ya wimbi la pili.

Nchi Kuu Zaidi ya Kidemokrasia Duniani ni Mdanganyifu Mkuu Zaidi Ulimwenguni

Mnamo 2020 kuanzia tarehe 13 hadi 15 Machi, kabla ya kutangazwa kufunga miji, Tablighi Jamaat walifanya kongamano jijini New Delhi. Baadhi ya wanachama wa Tablighi Jamaat walikutwa na Uviko, kwa zaidi ya mwezi vyombo vikuu vya habari viliendesha kampeni dhidi ya Waislamu na kuziita “wasambazaji wakubwa wa korona au mabomu ya korona,” hashtagi kama “jihad ya korona”(kuashiria kuwa Waislamu walikuwa wakisambaza virusi vya korona kwa makusudi) iliweza kushika kasi katika mtandao wa Twitter. Ripoti za Kwanza za Tukio (FIR) ziliwekwa dhidi ya wanachama wa Tablighi Jamaat na baadhi yao walifungwa kwa miezi. Jamii yote ya Waislamu ilichafuliwa. Wachuuzi masikini wa Kiislamu walinyanyaswa na walikabiliwa na migomo ya kiuchumi ambapo walikataliwa hata kuingia katika maeneo ambayo sio ya Waislamu. Serikali ya kitaifa yenye msimamo wa Ubaniani na sehemu kubwa ya vyombo vya habari vinavyo wafanyia kazi vilipata uchochoro na wakawalaumu Waislamu kwa kuenea kwa virusi wakati wa wimbi la kwanza. Ilikuwa ni hatia kupitia ushirika.

Ingawa hakuna mtu aliyewahi kufikiria ukubwa wa maafa ya wimbi la pili lililoleta, lakini Waislamu wa India hawakushangazwa na kitendo cha Modi kushindwa kushughulikia janga hilo. Alichaguliwa tu kwa sababu ya siasa zake kufarakanisha watu. Waislamu kutoka India, ambao wamekaa hapa kwa miongo kadhaa wanajua maisha yao hayana thamani hapa. Mwaka jana tu tulishuhudia sheria mpya za uraia dhidi ya Waislamu na Waislamu kutoka kote nchini waliingia mitaani ili kuipinga. Hii ilisababisha mauwaji ya halaiki dhidi ya Waislamu mashariki mwa Delhi huku umati wa vikundi vya Mabaniani walioungwa mkono na polisi wakiwaua Waislamu mchana kweupe. Vijana wa Kiislamu wakiwemo wanafunzi na wanaharakati walibandikiwa tuhuma za uwongo za kuleta ghasia na bado wangali wamefungwa magerezani.

Waislamu wanasongwa kwa viwango visivyo vya kawaida, sahau juu ya wahusika kufikishwa mahakamani, mauwaji na mateso ya Waislamu sio tu nchini India bali huwakuta mahali pengine popote ulimwenguni huadhimishwa hapa na sehemu kubwa ya jamii. Mfano wa hivi karibuni wa hili ni hashtagi “India inasimama na Israeli” ilishika kasi wakati Wazayuni waliposhambulia Masjid al-Aqsa.

Sasa, huku maiti za wapendwa wao zikirundikana, kwa sababu ya wimbi la pili lenye uharibifu, kuna hasira na kuchanganyikiwa kati ya Mabaniani jumla dhidi ya serikali, lakini athari ya hii itabakia kuonekana kama chuki jumla kwa Waislamu kwa sababu ya siasa za jamii husafisha kila kitu katika nchi hii.

Jitihada za kumaliza wimbi la pili tayari zimeanza. Kwenye chumba cha vita dhidi ya Uviko chenye zaidi ya watu 200, Mbunge wa BJP Tejaswi Surya aliwachagua wafanyakazi 17 wa Kiislamu na kuwatuhumu kwa kuendesha kashfa ya kuzuia kitanda.

Huku nchi nzima ikiwa na huzuni na inajitahidi kupata nafasi ya kuteketeza miili ya waliokufa, ujenzi wa bunge jipya, Central Vista, (mradi wa dolari bilioni 2) umeanza na imetangazwa kama huduma muhimu na serikali ya Modi.

Ni dhahiri kabisa kuwa katika demokrasia, viongozi hufanya kazi kukaa madarakani kwa faida zao binafsi. Katika nchi hii kubwa zaidi ya kidemokrasia ulimwenguni, serikali ina uwezo wa kuficha makosa yake makubwa kupitia propaganda ambazo zimejengwa juu ya kudhalilisha watu wachache. Demokrasia, kusoma kati ya mistari, ni nidhamu ambayo hupelekea ukandamizaji watu wake wachache.

Hakuna ubishi sasa kwamba serikali ya kitaifa ya Kibaniani imeisukuma India katika maafa ya virusi, lakini hali hapa ingekuwa karibu sawa na chama kingine chochote cha kisiasa kilichoko madarakani; zote ni pande tofauti za sarafu moja, mfumo huo huo uliooza, ambao unashibisha maslahi ya kibinafsi kupitia kunyonya damu ya raia hata ikiwa watalazimika kuchochea chuki elfu na masimulizi ya udanganyifu ili kuipata.

Katika demokrasia kubwa zaidi ulimwenguni watu wanaomba mitaani kupata haki zao za kimsingi za maisha na huduma za afya. Mfumo wa watu unawabana watu wake wenyewe hadi kufikia kufa. Hatuwezi kupumua!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Yameena Hassan*

* Yameena Hassan yuko jijini Delhi, India na ameshuhudia moja kwa moja mapambano ya nchi na COVID

#Covid19    #Korona        كورونا#

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu