Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tusiwache Kuhangaika Kwetu Kujitafutia Utajiri Kuwe ni Chanzo cha Mateso kwa Ummah Wetu

Katika wakati ambapo maadui wa Waislamu wameongeza uadui wao, na Waislamu, kuanzia Masjid al-Aqsa na Syria, mpaka eneo lililokaliwa la Kashmir na Afghanistan, wameongeza kuasi kwao kiungwana, kila afisa wa majeshi yetu ni lazima sasa ajitathmini kwa kina. Ni lazima akubali kuwa kizuizi cha muamko wa Ummah hakiko kwengine ila kwake kwani yeye ni miongoni mwa watu wanaomiliki nusra, nguvu na ulinzi.

Yeye, na wengine kama yeye, ndio wenye uwezo wa kuondoa kizingiti kilichoko sasa, kuutoa Ummah kutoka katika idhilali mbele ya maadui zake, hadi kuwatawala juu yao. Kwa hivyo, ni lazima atafakari ni kitu gani kilichomzuia kusonga mbele kabla na sasa. Huku akifanya hivyo, ni lazima awe na hisia sahihi ya mazingira yaliyo undwa ndani ya jeshi leo kuzuia harakati ya mageuzi na uhuru wa kikweli. Ni lazima atafute muongozo kutoka katika dini ili asibakie kuwa mtazamaji tu wa mgongano baina ya Ummah na wakoloni wavamizi. Hapo ndipo afisa huyu wa jeshi atakapo jitokeza kama mlinzi muaminifu anaye tafuta ushindi mkubwa kwa Ummah.    

Afisa huyu anapaswa kulichukulia joto lililoko sasa na mazingira yanayo zuia kupiga hatua, kuwa si yenye kutokea kibahati mbaya tu. Kutokana na utawala wa kiulimwengu wa mfumo wa kimada wa kirasilimali, kuhangaika kutafuta utajiri wa kimada imekuwa ndio lengo msingi maishani. Kutokana na maslahi duni ya kimada, urafiki huundwa na kuvunjwa, mafungamano hudumishwa na kukatwa, majukumu hutekelezwa na kupuuzwa. Kwa kukosekana Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, utajiri umekuwa ndio kipimo cha mafanikio na hadhi katika jamii. Kuhangaika kwa ajili ya kupata utajiri mkubwa imekuwa ndio jambo kubwa linalo washughulisha, miongoni mwa wenye msemo kwa jumla, na wanajeshi haswa.

Katika kadhia ya Pakistan, inayo miliki jeshi kubwa na lenye nguvu zaidi katika ulimwengu wa Waislamu, tunaona katika vilabu vya gofu na vilabu maalumu mila ya kushindana juu ya mapato ya kidunia. Mazungumzo yametawaliwa na ulinganishaji wa majumba, magari, taasisi za elimu kwa watoto, harusi zilizo pita mipaka, uwekezaji wa kibiashara na kiwango cha uwekaji akiba pesa. Katika mafunzo ya kijeshi ya kigeni, pamoja na miundo yote ya kimawasiliano ya kigeni, wamagharibi wako makini kuhisi na kukuza kasumba ya kimada ndani ya kila afisa, kwani huu ndio ufunguo wa kuwadhibiti. Hivyo basi si ajabu kuwa wengi katika wanajeshi, hususan katika ngazi za juu, wamekusanya utajiri wa kutosha kwa maisha yao yote na hiki kimekuwa ndio kipimo kwa wale walio chini yao. Nyaraka za Panama na kesi za taasisi ya kitaifa ya kuwahisabu walio na mamlaka zinatoa mtazamo wa ukusanyaji mkubwa wa utajiri miongoni mwa watu wenye msemo na walio bahatika. Huku utajiri huu ukidaiwa na wengine kuwa wenye kupatikana kiharamu, na wengine, kuwa wa halali, hakuna hata mmoja anaye weza kukataa kuwa viwango hivi vikubwa ndivyo vilivyo sababisha kuwepo na mazingira ya ufisadi. 

Tunapo tazama zama bora za Ummah wetu, zama za Khilafah na Jihad, tutaona dhihirisho la hali yetu ya sasa. Tuliweza vipi wakati huo kuonja ushindi na nguvu juu ya maadui zetu kwa makarne, na sasa hivi tunashindwa? Kisha, mashindano miongoni mwa majeshi yetu yalikuwa juu ya ufunguzi wa ardhi mpya kwa Uislamu na kuikumbatia shahada. Ummah uliweza kupata ushindi juu ya maadui zake, licha ya idadi yao kubwa ya majeshi na silaha. Kitambo Waislamu waliuchukulia utajiri kuwa kifaa, huku lengo la maisha na kipimo cha mafanikio vikiwa ni kutawala kwa dini yetu. Mpaka hapa, afisa wa jeshi na azingatie kuwa katika utangulizi wa katiba, kama ilivyo tayarishwa na Hizb ut Tahrir kwa Khilafah inayo kuja, elimu ya kijeshi itakuwa na sehemu nzito ya Uislamu.

Kama Hizb ut Tahrir ilivyo tabanni katika kifungu cha 67, "Ni wajib kulipatia jeshi kiwango cha juu zaidi cha elimu ya kijeshi ili kuinua kiwango chao cha kifikra kwa kadri inavyo wezekana. Kila mwanajeshi anapaswa kupewa thaqafa ya Kiislamu itakayo muwezesha kuwa na utambuzi wa Uislamu, angaa kwa kiwango jumla." Leo, Waislamu walio maafisa wa jeshi ni lazima wajitazame ndani yao, kwa kutumia dini yetu kama kipimo, kupambana dhidi ya maslahi na matamanio ya vyeo vyao, ili kujitokeza kuunusuru Ummah katika wakati huu unapo wahitajia mno.

Kwa wanaume wanaotaka kuvunja kizingiti hiki, na wazingatie kwa makini hikma iliyopo katika maonyo ya Mtume wa Allah (saw) kuhusiana na tamaa ya utajiri iliyo pitiliza mipaka. Ka'ab bin 'Iyad anahadithia kutoka kwa Mtume wa Allah (saw) akisema:

«إِنَّ لِكُلِّ أُمَّةٍ فِتْنَةً وَفِتْنَةُ أُمَّتِي الْمَالُ» "Hakika katika kila Ummah kuna fitna na fitna ya Ummah wangu ni mali" [Tirmidhi].

Ibn Ka'ab bin Malik Al-Ansari anahadithia kutoka kwa babake, kuwa Mtume wa Allah (saw) amesema:

«مَا ذِئْبَانِ جَائِعَانِ أُرْسِلاَ فِي غَنَمٍ بِأَفْسَدَ لَهَا مِنْ حِرْصِ الْمَرْءِ عَلَى الْمَالِ وَالشَّرَفِ لِدِينِهِ» "Mbwa mwitu wawili walio miongoni mwa kondoo si waharibifu kwao kushinda mtu aliye na tamaa ya mali na cheo kuliko dini yake.” [Tirmidhi].

Ni vipi basi mtu anaye shuhudia uharibifu huu wa Ummah mbele ya macho yake na fitna juu ya fitna, atanyamazia kimya kutokana tu na kiu ya utajiri? Ikiwa atabakia kufungika katika minyororo ya uchu wa kujitajirisha binafsi, anajinyima fursa ya kutukuzwa milele na milele kesho Akhera kwa kuinusuru dini yetu!

Na wazingatie kuwa uchu wa kupata utajiri ni katika umbile la mwanadamu, ghariza (hisia) yake ya kuhifadhi maisha iko juu. Kihakika, kama tunavyo taka kujihifadhi dhidi ya kitu chengine chochote, tusidharau pia matamanio. Wala tusidharau pia maafa yake ambayo yaweza kusababisha juu ya majukumu ya mja anaye taka radhi za Allah (swt), kama kipaumbele cha maisha yake. Anas b. Malik amepokea katika hadith ya Mtume wa Allah (saw) akisema:

«لَوْ كَانَ لاِبْنِ آدَمَ وَادٍ مِنْ ذَهَبٍ أَحَبَّ أَنَّ لَهُ وَادِيًا آخَرَ وَلَنْ يَمْلأَ فَاهُ إِلاَّ التُّرَابُ وَاللَّهُ يَتُوبُ عَلَى مَنْ تَابَ» "Lau Mwanadamu angekuwa na bonde la dhahabu angependa awe na bonde la pili na hakuna kitakacho jaza mdomo wake isipokuwa mchanga na Allah humsamehe mwenye kutubia" [Muslim].

Zaidi ya hayo, hamu ya kutaka utajiri iko juu hata kwa mtu aliye zeeka na kupanda ngazi za juu katika taasisi ya kijeshi, ingawa mauti ni jambo la kawaida. Anas bin Malik amehadithia kutoka kwa Mtume (saw) akisema:

«يَهْرَمُ ابْنُ آدَمَ وَيَشِبُّ مِنْهُ اثْنَتَانِ الْحِرْصُ عَلَى الْعُمُرِ وَالْحِرْصُ عَلَى الْمَالِ» "Mwanadamu anazeeka lakini vitu viwili havizeeki kwake: tamaa ya umri na tamaa ya mali" [Tirmidhi]

Uislamu, kama ulivyo teremshwa na Muumba (swt) wa mwanadamu pamoja na utajiri, uliitibu hamu hii katika njia bora zaidi. Lau tutajifunza, kutafakari na kubadilika, hatutafungwa na minyororo ya maisha haya mafupi ya dunia, na kuyatupa maisha yetu ya milele ya Akhera.

Kwa hivyo, Uislamu umetukumbusha kuwa utajiri wa kihakika unao tunufaisha sio ule tulio ukusanya na kuwaachia warithi wetu, bali ni ule uliotumiwa kwa ajili ya Allah (swt). Mutarrif amepokea kutoka kwa babake: Nilikuja kwa Mtume wa Allah (swt) alipo kuwa akisoma:

(أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُر) “Utawashughulisheni nyinyi ukusanyaji mali” [Surah at-Takaathur 102:1].

Akasema: «يَقُولُ ابْنُ آدَمَ مَالِي مَالِي» "Anasema mwanadamu: mali yangu, mali yangu". Na yeye (saw) akasema:

«وَهَلْ لَكَ يَا ابْنَ آدَمَ مِنْ مَالِكَ إِلاَّ مَا أَكَلْتَ فَأَفْنَيْتَ أَوْ لَبِسْتَ فَأَبْلَيْتَ أَوْ تَصَدَّقْتَ فَأَمْضَيْتَ» "Je, ewe mwanadamu, una mali yoyote isipokuwa ile ulio kula ikamalizika au ulio vaa ikachakaa au ulio toa sadaqa ukaitanguliza mbele?" [Muslim].

Katika hadith sawa na hii, Abu Huraira (ra) amepokea kutoka kwa Mtume (saw) akisema:

‹‹يَقُولُ الْعَبْدُ مَالِي مَالِي إِنَّمَا لَهُ مِنْ مَالِهِ ثَلاَثٌ مَا أَكَلَ فَأَفْنَى أَوْ لَبِسَ فَأَبْلَى أَوْ أَعْطَى فَاقْتَنَى وَمَا سِوَى ذَلِكَ فَهُوَ ذَاهِبٌ وَتَارِكُهُ لِلنَّاسِ››

"Mja anasema: mali yangu mali yangu, hakika mali yake ni katika mambo matatu tu; alicho kula kikamalizika au alicho vaa kikachakaa au alichotoa akakiweka (kesho akhera) yasiyo kuwa haya ataondoka na kuwaachia watu" [Muslim].

Anas bin Malik (ra) anahadithia kutoka kwa Mtume wa Allah (saw) akisema:

‹‹يَتْبَعُ الْمَيِّتَ ثَلَاثَةٌ، فَيَرْجِعُ اثْنَانِ وَيَبْقَى مَعَهُ وَاحِدٌ: يَتْبَعُهُ أَهْلُهُ وَمَالُهُ وَعَمَلُهُ، فَيَرْجِعُ أَهْلُهُ وَمَالُهُ، وَيَبْقَى عَمَلُه» “Vitu vitatu vinamfuata maiti, viwili vinarudi kimoja kinabakia naye: wanamfuata watu wake, mali yake na amali yake. Watu wake na mali yake vina rudi, amali yake inabakia." [Bukhari].

Maafisa wa ngazi za juu zaidi jeshini na wazingatie kuwe lau watakufa kesho, ni wachache watakaosema kuwa walikufa wakiwa wadogo. Na wajiulize maswali, ni vipi basi kuhusu utajiri ambao kwao walitafuta raha na utilivu? Utajiri huo utamnufaisha nani, isipokuwa warathi wao? Utajiri huo hautakuwa na manufaa kwao, huku wakimkabili Allah (swt) kuulizwa maswali kuhusiana na uwezo wao waliokuwa nao na waliufanyia nini katika zama hizi za idhlali? Na wazingatie basi maneno ya Allah (swt) alipo sema:

يَوْمَ لا يَنْفَعُ مَالٌ وَلا بَنُونَ * إِلاَّ مَنْ أَتَى اللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ

“Siku ambayo haitanufaisha mali wala watoto - Isipokuwa (atanufaika) yule atakayemjia Allah na moyo uliosalimika” [Surah ash-Shura'a 26:88-89]

Maafisa na wazingatie kuwa hamu ya utajiri haipaswi kuishinda ari ya kujitolea katika matendo mema wakati wowote, haswa wakati ambapo matendo mema hayo yana uwezo wa kuleta wimbi la mageuzi kwa Ummah huu kipenzi. Allah (swt) asema:

الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا

“Mali na watoto ni mapambo ya maisha ya dunia. Lakini yaliobakia katika mema ni thawabu bora mbele ya Mola wako na matarajio mema" [Surah Al-Kahf 18:46]

 Ibn 'Abbas (ra) asema:

هي ذكر الله ، قول : لا إله إلا الله ، والله أكبر ، وسبحان الله ، والحمد لله ، وتبارك الله ، ولا حول ولا قوة إلا بالله ، وأستغفر الله ، وصلى الله على رسول الله ، والصيام ، والصلاة ، والحج ، والصدقة ، والعتق ، والجهاد ، والصلة ، وجميع أعمال الحسنات. وهن الباقيات الصالحات ، التي تبقى لأهلها في الجنة ، ما دامت السموات والأرض

“Kumkumbuka Allah ni katika maneno: 'La ilaha illallah, Allahu Akbar, Subhan Allah, Al-Hamdu Lillah, Tabarak Allah, La hawla wa la quwwata illa billah, Astaghfirallah, Sallallahu 'ala Rasul-Allah', na saumu, swala, hajj, sadaqah, kuacha huru mtumwa, Jihad, kuunganisha kizazi, na amali zote nyengine njema. Hizi ndizo amali zitakazo bakia kwa watendaji wake peponi, kwa wale watakao zifanya maadamu mbingu na ardhi zitabakia kuwepo kwake"

Allah (swt) pia ameonya:

وَاعْلَمُواْ أَنَّمَآ أَمْوَلُكُمْ وَأَوْلَـدُكُمْ فِتْنَةٌ وَأَنَّ اللَّهَ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ “Na jueni kuwa hakika mali zenu na watoto wenu ni fitna na mbele ya Allah kuna malipo makubwa.” [Surah Anfaal 8:28]

Na Allah (swt) ameonya:

يأَيُّهَا الَّذِينَ ءَامَنُواْ لاَ تُلْهِكُمْ أَمْوَلُكُمْ وَلاَ أَوْلَـدُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّهِ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْخَـسِرُونَ

“Enyi Mulioamini! Zisiwashughulisheni mali zenu wala watoto wenu katika kumkumbuka Allah. Na atakaye fanya hivyo ni katika walio hasirika.” [Surah Munafiqun 63:9]

Afisa wa jeshi anayetaka kufuata njia ya Maanswari (ra), waliotoa nusra kwa Uislamu hapo awali, aufunge moyoni wake barabara kuwa mafanikio na cheo cha kihakika hayapatikani kupitia utajiri. Abu Huraira (ra) amepokea kutoka kwa Mtume wa Allah (saw) akisema: 

«إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلَى صُوَرِكُمْ وَأَمْوَالِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ وَأَعْمَالِكُمْ» "Hakika Allah haangalii sura zenu na mali zenu lakini ana angalia nyoyo zenu na amali zenu." [Muslim]

Imepokewa kutoka kwa Samurah bin Jundab kwamba Mtume wa Allah (saw) asema:

«الْحَسَبُ الْمَالُ وَالْكَرَمُ التَّقْوَى» “Heshima ni mali na ukarimu ni ucha Mungu.” [Ibn Maajah].

Na ajitakase kutokana na athari fisidifu na kusimama kama mkombozi wa Ummah huu. Na ajitokeze sasa, bila ya kusitasita, akitafuta cheo sawa na cha nduguye wa kijeshi aliye mtangulia katika kutoa nusra kusimamisha Uislamu kama serikali na utawala, naye ni Sa'ad ibn Muadh (ra). Pindi Sa'ad (ra) alipo fariki, mamake alilia na Mtume wa Allah (saw) akamwambia: 

‹‹ليرقأ (لينقطع) دمعك، ويذهب حزنك، فإن ابنك أول من ضحك الله له واهتز له العرش»

“Machozi yako yatasita, na huzuni yako itatoweke,utakapojua hakika mwanao ndiye mtu wa kwanza kumfanya Allah acheke na Arshi yake itingishike.” [At-Tabarani].

Afisa wa jeshi wa zama hizi na ajitolee nafsi yake na mali yake kwa ajili ya Allah (swt) kwa lengo la kupata Jannah katika biashara bora ambayo yapaswa kuonewa wivu! Allah (swt) asema:

إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Hakika Allah amenunua kutoka kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa badali ya pepo* Wanapigana katika njia ya Allah; wanauwa na kuuwawa. Ahadi yake ni ya kweli katika Taurati na Injili na Quran. Na ni nani mkweli zaidi katika utekelezaji ahadi asiye kuwa Allah? Basi pokeeni bishara njema ya biashara yenu mulio ifanya. Na huko ndiko kufaulu kukubwa.” 

[Surah At-Tawba 9:111]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:28

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu