Al Waqiyah TV: Enyi Watawala katika Nchi za Waislamu ... Je, Hamuoni Aibu?!
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Al Waqiyah TV: Enyi Watawala katika Nchi za Waislamu ... Je, Hamuoni Aibu?!
Al Waqiyah TV: Enyi Watawala katika Nchi za Waislamu ... Je, Hamuoni Aibu?!
Mwaka mzima umepita tangu kuanza kwa Kimbunga cha Al-Aqsa na vita vikali vilivyofuata huko Gaza. Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana, watu wa Gaza wamevumilia mitihani mikubwa, wakiishi katika machungu, mateso, na majanga yasiyohesabika.
Kwa kuzingatia mapambano yanayoendelea, ni wazi kuwa masuluhisho ya sasa yanayoongozwa na Amerika yanashindwa kushughulikia sababu kuu za mzozo huo. Hafla hii itavinjari mwelekeo tofauti-uliojikita katika kanuni na uadilifu wa Kiislamu-ili kutoa njia ya mabadiliko ya kudumu.
Baada ya Swala ya Ijumaa, katika mji mkuu, Tunis, yalifanyika matembezi ya hamsini yaliyoitishwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia, kwa watu wa Zaytouna, kwa ajili ya kuwanusuru watu wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa ulio mateka, na kichwa chake kilikuwa, “Enyi Waislamu, je, mtawaacha watu wa Palestina peke yao na hali Umma una majeshi yenye Nguvu?!”
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia ilifanya mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano huko Ariana katika mji mkuu, Tunis, saa 10:30 asubuhi kwa saa za eneo, wenye kichwa “Uchaguzi ni njia ya Kuendeleza Mfumo wa Kisekula ambao ni Wajib Ubadilishwe kwa Kusimamisha Khilafah”
Al Waqiyah TV: Mihemo ya Walio Imara... Mahojiano ya Moja kwa Moja kutoka Barabara za Gaza!
Takriban watu 40,000 wameuwawa mjini Gaza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku serikali za ulimwengu, zikiwemo nchi za Waislamu zikitazama kama watazamaji pekee wa mauaji haya ya umwagaji damu, bila ya dhamira yoyote ya kisiasa ya kukomesha mauaji hayo. Hakika, tawala nyingi za ardhi za Kiislamu kwa miongo kadhaa zimeimarisha mkono wa uvamizi wa Kiyahudi kupitia mikataba yao ya amani, kuhalalisha mahusiano ya kidiplomasia, na ushirikiano wa kiuchumi na umbile hili la mauaji ya halaiki.
Wanawake wa Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wameelekeza wito kwa wana wa majeshi ya Kiislamu kutekeleza wajibu wao wa Kiislamu katika kuwalinda Waislamu wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) kutokana na uchafu wa umbile la kiyahudi linaokalia kwa mabavu, na kukomboa kila shubiri ya ardhi hii iliyobarikiwa kutoka kwa makucha ya uvamizi huu wa kikatili.
Mgogoro wa Bahari ya China Kusini umeibuka tena kufuatia kuvuja kwa waraka wa kidiplomasia kutoka Jamhuri ya Watu wa China (PRC) kwa Ubalozi wa Malaysia jijini Beijing, wa tarehe 18 Februari. Ujumbe huo ulifichua pingamizi ya China na kuitaka Malaysia kusitisha shughuli za utafiti wa mafuta na gesi huko Beting Raja Jarum na Beting Patinggi Ali, maeneo ya ndani ya Visiwa vya Spratly.
Majeshi ya Waislamu yanapaswa Kuiga Mifano ya Maher al-Jazi na Mashour Haditha al-Jazi.