Hotuba ya Pili Katika Kongamano: ‘Vijana Waislamu …Waanzilishi wa Mabadiliko Msingi’
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Thaqafa ya watu wowote huwakilisha uti wa mgongo wa uwepo wao na kudumu kwao. Juu ya thaqafa, hadhara yake hujengwa, dhamira na malengo yake hufafanuliwa, mpangilio wa maisha yao huwa wa kipekee kwake, watu wake huyeyushwa ndani ya chungu kimoja ili watafautishwe kupitia hiyo na mataifa na watu wengine.