Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Vichwa vya Habari 14/12/2022

Taharuki umezuka tena huko Kosovo kaskazini huku mamia ya Waserbia wakiweka vizuizi vya barabarani kwa kutumia mashini nzito katika vivuko viwili vya mpaka na Serbia, na kuzuia magari. Haya yanajiri kutokana na mvutano wa hivi majuzi wakati Kosovo ilipoamuru madereva kusalimisha nambari zao za leseni zilizotolewa na Serbia na badala yake kuweka nambari za Kosovo.

Soma zaidi...

Vichwa vya Habari 07/12/2022

Indonesia imepitisha kanuni mpya ya jinai yenye ubishani inayojumuisha kupiga marufuku kuishi kinyumba na ngono nje ya ndoa, katika mabadiliko ambayo wakosoaji wanashindana yanaweza kuhujumu uhuru katika taifa hilo la Asia ya Kusini. Sheria hizo mpya zinahusu watu wa Indonesia na wageni na pia zinaregesha marufuku ya kumtusi rais, taasisi za serikali au mfumo wa kitaifa wa Indonesia unaojulikana kama Pancasila.

Soma zaidi...

Vichwa vya Habari 6/12/2022

Vita nchini Ukraine vimefichua udanganyifu mkubwa katika udhibiti mpya wa hifadhi za silaha baada ya Vita Baridi, na kuacha baadhi ya nchi zikijitahidi kukabiliana na mahitaji ya ulinzi. Ujerumani imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kudumisha dhamira yake ya ulinzi kwa NATO huku ikiipa Ukraine silaha zinazohitajika ili kukabiliana na Urusi.

Soma zaidi...

Vichwa vya Habari: 30/11/2022

Maandamano ya umma nchini China yanayohusiana na vizuizi vya serikali vya Covid-19 yamegonga vyombo vya habari vya kimataifa kufuatia moto mbaya wa ghorofa moja huko Urumqi, Xinjiang ambao uliua watu kumi. Maandamano yalizuka katika miji kote China kulingana na video zilizochapishwa kwenye Weibo na Twitter za China. Raia kote China walilaumu vifo hivyo kutokana na kushindwa kwa huduma za zimamoto na uokoaji kufikia jengo hilo kwa sababu ya vizuizi vya COVID-19.

Soma zaidi...

Vichwa vya Habari 23/11/2022

China imefunga moja ya mikataba mikubwa zaidi ya gesi asilia majimaji (LNG) pamoja na Qatar yenye thamani ya dolari bilioni 60, Shirika la Habari la Qatar lilitangaza. Mkataba huo wa kihistoria na nchi yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani unatazamiwa kuimarisha usalama wa kawi wa Beijing kwa miongo kadhaa na ni mapinduzi makubwa kwa China huku nchi zikikimbilia kufunga mikataba ya kawi kutokana na uhaba unaosababishwa na vita vya Urusi na Ukraine.

Soma zaidi...

Vichwa vya Habari 16/11/22

Urusi ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Ukraine, siku chache tu baada ya kujiondoa kidhalilifu kutoka kwa mji wa Kherson. Kombora moja lilitua katika mpaka wa Ukraine nchini Poland na kuua watu wawili. Kombora hilo lilitua karibu na Przewodow, chini ya maili tano kutoka mpaka wa Ukraine na takriban maili 40 kaskazini mwa Lviv, Ukraine.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu