Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 502
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Khilafah itakomesha sera ya ubinafsishaji iliyowekwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, IMF, ambayo imesababisha uharibifu wa sekta ya nishati, mafuta na gesi, na badala yake itatabikisha hukmu ya umilikaji wa umma katika Uislamu, kuhusiana na nishati na madini.
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni taasisi ya kikoloni ikitoka kwa mkataba wa bretton woods, inatumika kuanzisha ukiritimba wa dola ya marekani katika biashara ya kimataifa.
Kwa kutenga asilimia 52 ya bajeti yote kwa malipo ya riba pekee, maslahi ya wananchi, serikali na usalama yako hatarini.
Hakika watawala wa Pakistan, pamoja na watawala wa nchi nyengine za Kiislamu, ni vibaraka wa duni wa ukoloni, na barakoa zao sasa tayari zimeshapomoka kikamilifu.
Hakika Khilafah itaziunganisha nchi za Kiislamu kuwa Dola moja kwa njia ya Kimsingi!!
Kalima yenye kichwa “Jueni kwamba katika Mapinduzi yenu munaelekea Njia Panda!” Imetolewa na Ustadh Abdo Al-Dalli (Abu Al-Mundhir), Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Syria.
Dkt. Abdur Rafay kuhadithia maelezo yanayoatua moyo kutoka Rafah na kuhutubia suluhisho la Palestina.
Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka zake za dhati kwa Umma wa Kiislamu, wenye kulemewa na majeraha na kustahamili shinikizo la moja kwa moja na lisilo la moja kwa moja la kikoloni. Kwa mnasaba huu, tunawataja makhsusi watu wetu wenye subira mjini Gaza Hashim na kwa jumla katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, tukimuomba Mwenyezi Mungu azifanye siku za Idd hii kuwa chanzo cha utulivu wa nyoyo zao.