Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 364
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mfumo wa Upendeleo Jumla (GSP) kwa bidhaa za Bangladesh katika soko la Amerika ulisimamishwa mnamo mwaka wa 2013. Mojawapo ya masharti ya kuregesha manufaa ya GSP ilikuwa kukomeshwa kwa ajira ya watoto.
COP26 itazihimiza nchi 195 kutekeleza ahadi walizotoa walipokuwa wakikubaliana juu ya Mkataba wa Paris wakati wa COP21 mwaka 2015.
Jioni ya mnamo Oktoba 29, Odiljon Jalilov, mwanachama wa Hizb ut Tahrir/Sweden, alipatikana na polisi na kuwekwa chini ya ulinzi akisubiri maandalizi ya kuhamishwa hadi Uzbekistan.
Kongamano moja lilifanyika jijini Sana'a tarehe 28/10/2021, lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanazuoni wa Yemen na Mamlaka Kuu ya Wakfu chini ya kichwa "Umoja wa Kiislamu... Fursa na Changamoto".
Pentagon hivi karibuni ilitangaza kwamba shambulizi la droni za Amerika jijini Kabul mnamo tarehe 29 Agosti na kuua raia 10 wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, lilikuwa kosa la kujutia lakini halikuwa utovu wa nidhamu wala ukiukaji wa sheria.
UNICEF ilitangaza kuwa watoto 10,000 wa Yemen ima wameuawa au kulemazwa tangu kuanza kwa vita nchini Yemen mwezi Machi 2015 na kuongezea kuwa vifo vingi zaidi vya watoto na majeruhi havirekodiwi na milioni 11 wanahitaji msaada wa kibinadamu na karibu 400,000 wanaugua utapiamlo mkali huku zaidi yawatoto milioni 2 hawako shuleni.
Greta Thunberg sasa ameondoka kwenye jukwaa baada ya ukosoaji mfupi lakini mkali wa Cop26. "Viongozi hawafanyi lolote,
Awamu ya sita ya kikao cha Kamati ya Katiba, ikiwa na sehemu zake mbili, mwakilishi wa serikali ya kihalifu na mwakilishi wa ule unaoitwa upinzani, ilianza Jumatatu, 18 Oktoba 2021, huu ni mkutano wa sita baada ya mikutano mitano kufeli.
Ni furasa kwetu sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan kuwaalika ndugu zetu wataalam wa habari, wanasiasa, wasomi na wanamaoni kuhudhuria na kushiriki katika Kikao cha Kadhia za Umma cha kila mwezi,