Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 352
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kuokoa adhabu isiyo ya haki kwa kuulingania Uislamu pamoja na Hizb ut Tahrir, Hafizov Asgat aliongezewa miaka mengine 10 gerezani hadi kufikia miaka 19.
Haki za Waislamu hazirejeshwi kupitia unyenyekevu, ulegezaji msimamo, diplomasia na mapatano.
Mnamo Alhamisi, 22 Julai 2021 Waziri wa Kigeni wa Israel Yair Lapid alitangaza kwamba Israel imejiunga na Muungano wa Afrika (AU) kama dola mtazamaji.
Katika wiki za hivi karibuni, serikali ya Denmark imekabiliwa na upinzani wa kisiasa na kukashifiwa kitaifa na kimataifa kwa mipango yake ya kuwahamisha wakimbizi hadi vituo vya hifadhi nchini Rwanda.
Mfululizo wa matukio ya machafuko ulianza mnamo Jumanne jioni, 10/08/2021, baada ya kuuawa kwa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 wakati wa vita katika wilaya ya Altindağ ya Ankara, ikifuatiwa na kurusha mawe katika nyumba za wahamiaji kutoka Syria na uporaji maduka yao.
Hamid ur Rahman Sharifi, mbebaji ulinganizi wa Hizb ut Tahrir, aliuwawa shahidi mnamo 8 Agosti kwa shambulizi la makombora lililotokana na mzozo mkali katika mkoa wa Kunduz.
Kwa mujibu wa huduma ya habari ya Idara Kuu ya Mambo ya Ndani ya jimbo la Chuy, mwanaharakati mmoja katika Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir, mzaliwa wa mkoa wa Jalal Abad, katika wilaya ya Alamüdün ya jimbo la Chuy, alikamatwa.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Syria iliandaa kisimamo katika mji wa Azaz viungani mwa Aleppo Kaskazini baada ya swala ya Ijumaa kwa anwani "Daraa Yawaomba Nusra Wenye Ikhlasi na Yaondoa Barakoa kutoka kwa Wanyonge!"
Kwa mujibu wa na ripoti ya shirika la habari la Associated Press mnamo Ijumaa, katika mapigano ya kasi isiyo dhibitika kwenye ngome yao ya kusini mujahidina wa Afghanistan waliichukua miji mikuu mingine minne ya mikoa ikiwapa udhibiti wa nusu ya miji mikuu ya mikoa ya Afghanistan na theluthi mbili za nchi hiyo,