Jarida la UQAB Toleo 103 - Agosti 2025
- Imepeperushwa katika Jarida la UQAB
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Agosti 2025 M.
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Agosti 2025 M.
Tangu Disemba 8, 2024, Syria imeshuhudia ziara mbalimbali za kidiplomasia katika ngazi mbalimbali. Ziara hizi haziwezi kuelezewa kuwa ziara za kawaida, haswa baada ya kuchunguza historia ya nchi zilizo zuru Damascus na kuelewa uhalisia wake.
Vita vinavyoendelea katika sehemu mbalimbali za dunia—hasa vita kati ya Urusi na Ukraine na mzozo kati ya Iran na umbile la Kiyahudi—vinaonyesha wazi kwamba ulimwengu umeingia katika awamu mpya na tofauti ya vita vya kijeshi na kijasusi. Mtazamo wa kale wa vita, uliopitwa na wakati, unaojengwa juu ya vikosi vikubwa vya askari wachanga, vifaru, na mizinga, unabadilika kwa kasi na kuporomoka. Leo, dola kama vile Marekani, China na Urusi zinatenga bajeti kubwa kwa viwanda vya juu vya kijeshi na zinafafanua upya mbinu mpya za kivita. Vita kwenye mstari wa mbele wa kisasa havikomei tena kwa risasi na bunduki – ni vita vya operesheni za kimahesabu (algorithms), akili ya bandia, droni, mtandao na mawimbi ya satelaiti.
Axios iliripoti kwamba mkutano wa ngazi ya juu ulifanyika jijini Paris kati ya Waziri wa Mambo ya Kimikakati wa ‘Israel’ Ron Dermer na Waziri wa Mambo ya Nje Asaad Al-Shibani, uliopatanishwa na mjumbe maalum wa Marekani nchini Syria, Thomas Barak, mnamo 25/7/2025. Siku chache zilizopita tangu tarehe 12/7/2025 zimeshuhudia kuongezeka kwa machafuko katika Jimbo la Al-Suwayda [Sweida] kusini mwa Syria, ambalo wengi wa wakaazi wake ni Druze. Umbile la Kiyahudi limetangaza kuingilia kati masuala yao sambamba na kuendeleza uvamizi na mashambulizi yake nchini Syria. Lilishambulia pambizoni mwa kasri la rais, na kuishambulia Wizara ya Ulinzi na Majeshi jijini Damascus.
Bunge la Seneti mnamo Alhamisi lilipitisha azimio kwa kauli moja, kulaani tukio la mauaji ya wenza mchana kweupe kwa maagizo ya Jirga kwa jina la kile kinachoitwa “mauaji ya heshima” huko Balochistan. Lilisema mauaji haya ya kinyama hayawezi na hayapaswi kufunikwa na hoja yoyote ya kitamaduni, kikabila, au kimila kwa kisingizio cha kile kinachojulikana kama ghairat au “heshima.” Kwa kweli ni uhalifu ambao umelivunjia heshima taifa. Jaribio lolote la kuhalalisha uhalifu kama huo kwa msingi wa “desturi au heshima” halikubaliki kabisa, kama ilivyo kwa mchakato mzima wa kulaumiwa kwa mwathiriwa.
Jumatatu iliyopita (21 Julai, 2025) alasiri, ndege ya kivita ya Jeshi la Anga la Bangladesh F-7 BGI iligonga jengo katika sehemu ya chini ya Shule ya Milestone na Chuo katika eneo la Uttara katika Mji Mkuu kutokana na hitilafu ya kiufundi. Hii ilisababisha hali ya kusikitisha na ya kuhuzunisha kwa matukio ya kutisha ya watoto walioungua na kukatwa viungo na vijana waliouawa na kujeruhiwa. Sisi katika Hizb ut Tahrir, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) msamaha kwa marehemu hao, na tunawaombea nafuu ya haraka waliojeruhiwa. Na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awajaalie wahasiriwa hadhi ya mashahidi Peponi kwa mujibu wa bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).
Katika hotuba yake baada ya kula kiapo cha kuwa Waziri Mkuu, Kamil Idris alisema: “Kauli mbiu yetu ni matumaini, na dhamira yetu ni kufikia usalama, ustawi, na maisha ya utulivu kwa kila raia wa Sudan!” Katika taarifa yake ya kwanza kwa vyombo vya habari, alitangaza kuwa atatoa muda na juhudi zake kuhakikisha maisha ya heshima kwa kila Msudan.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan inafuraha kuwaalika wanahabari, wanasiasa, na wote walio na hamu na masuala ya Umma kuhudhuria na kushiriki katika kikao kipya cha kisiasa, ambacho kitamwalika Ustadh Muhammad Jami' (Abu Ayman), Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan.
Gaza imeingia katika awamu ya tano njaa (awamu ya janga la njaa), kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa. Huku Waislamu kila mahali wakijaribu kuwanusuru ndugu zao kwa michango na kuanzisha misafara ya kuvunja mzingiro dhidi yao, nchi jirani zinatazama bila harakati yoyote—mbele yao zaidi ni Misri, ambayo ina mpaka na Gaza, lakini inadai kuwa haina usemi katika suala hilo na imeridhia kuchukua dori ya mpatanishi. Hivyo, je, kweli Misri haina uwezo wa kuwanusuru watu wa Gaza?!