Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hali ya Kisiasa Nchini Gambia

Tunataraji Hizb inatia maanani kadhia za Waislamu katika Afrika kama inavyotia maanani kadhia nyengine za Waislamu ambazo likizuka jambo tu hutoa toleo baada ya siku moja au mbili…Lakini, kwa mfano, Gambia, haijatoa toleo lolote kuhusu (nchi hiyo) hadi leo, pamoja na kwamba yaliyotokea yameendelea kwa karibu miezi miwili.

Soma zaidi...

Kuziendea Mahakama Katika Dar al-Kufr kwa Ajili ya Kuondosha Ukandamizaji

Lakini kwa kukosekana Khilafah, biladi zote za Waislamu zinatawaliwa na viongozi Matwaghut? Kwa hivyo, ikiwa tunahitaji kutatua mzozo wowote, twaweza kwenda katika mahakama za viongozi hao Matwaghut? Lau, mmoja katika wanafamilia yangu atabakwa, je, inajuzu kwenda kutafuta hukmu mahakamani ambako hukmu itafanywa kupitia Taghut ya kidemokrasia? Hawahukumu kwa shariah

Soma zaidi...

Tunaionya Japan Itahadhari na Matokeo ya Kuiunga mkono Serikali ya Wauaji ya Myanmar katika Mauaji yao ya Halaiki ya Warohingya, kwa kuwa Khilafah ya Uongofu inayokaribia kwa hakika italishughulikia suala hili kwa umakinifu

Japani imeifuata India, kibaraka mwingine wa washambuliaji wa Kimagharibi, kwa kuiunga mkono Serikali ya Myanmar kuhusiana na Mauaji ya halaiki ya Waislamu Warohingya.

Soma zaidi...

Kuhamisha Nidhamu ya Usimamizi wa Usambazaji wa Maji kwa Kampuni binafsi huko Purbachal ni Madhara Makubwa na Usaliti wa Uaminifu

Baada ya kuwapisha njia mabepari wafisadi kupora pesa za umma katika sekta ya umeme, serikali ya Hasina sasa imeamua kukabidhi usimamizi wa usambazaji wa maji katika mji mpya wa Purbachal kwa kampuni binafsi ambayo lengo lake ni kupata faida tu, sio kulinda watumiaji.

Soma zaidi...

Mauaji Dhidi ya Watoto wa Yemen yanaendelea, ilhali Wauaji wanacheza dori ya Waweka Amani

Mnamo 26 Aprili, Umoja wa Mataifa ulipeperusha ripoti kwamba idadi ya waliofariki ndani ya Yemen kutokana na mzozo unaoendelea unatarajiwa kupita 230,000 mwishoni mwa 2019. Utafiti kwa kichwa “Tathmini ya Athari ya Vita Juu ya Maendeleo ndani ya Yemen”,  pia iliripoti kuwa Wayemen 131,000 watakuwa wamefariki kutokana na athari mbaya za vita baina 2015 na 2019 mfano kutokana na njaa, maradhi na kukosekana kwa kliniki za afya. Kwa mujibu wa UN mwishoni mwa mwaka, mapigano yatakuwa yamechukuwa maisha ya watu 102,000.

Soma zaidi...

Ongezeko la Takwimu Sio Jipya Bali Halina Budi kwa Zabuni za Kifedha Kabla ya Kongamano la Wafadhili la Brussels kwa Ajili ya Syria

Vita katili nchi Syria dhidi ya raia vimeingia mwaka wake wa tisa mnamo Machi 15. Zaidi ya watu nusu milioni wamekufa, kwa mujibu wa ripoti za kimataifa, na shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria limenakili vifo 19800 vya watoto tangu 2011. Inakisiwa watoto milioni 8.6 wanahitaji msaada wa dharura, na sasa zaidi ya watoto milioni 6 hawana makao au wanaishi kama wakimbizi, na baadhi ya milioni 2.5 yao hawendi shule. Zaidi ya watoto milioni 3 wako katika hatari ya mabomu ya ardhini, huku takriban asilimia 40 ya wale waliouwawa na mabomu ya ardhini wakiwa ni watoto. 

Soma zaidi...

Janga la Watoto Wachanga Linafichua Hali Mbaya ya Sekta ya Afya Nchini Tunisia na Kudhihirisha Kufeli kwa Serikali Hiyo Katika Kuchunga na Kulinda Watu Wake!

Janga chungu liliitingisha rai jumla nchini Tunisia wiki jana! Watoto wachanga kumi na tano walikufa katika Hospitali ya Wassila Bourguiba kwa mujibu wa takwimu rasmi na idadi inazidi kuongezeka. Mnamo Ijumaa, Machi 15, msemaji wa Afisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Ummah alisema “idadi ya watoto wachanga waliokufa katika Hospitali ya Wassila Bourguiba ilikuwa ni 15.” Janga hilo lilifuatiwa na jengine baya zaidi, kila mojawapo likiifichua dola hiyo kuwa haiangalii watu wake!

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu