Jumamosi, 04 Rajab 1446 | 2025/01/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kurekebisha Siasa kwa Ajili ya Uhuru Halisi

(Imetafsiriwa)

Mdahalo wa nchi nzima kuhusu Siku ya Uhuru wa Pakistan, 14 Agosti, umepanuka hadi kuhoji muundo wa katiba na siasa zinazotekelezwa. Ni mjadala wa kimsingi, ambao utafafanua mwelekeo wa juhudi za Waislamu wa Pakistan wanaoteseka kwa muda mrefu, kwa ajili ya mabadiliko. Uhuru wa kweli hautapatikana katika mabadiliko ya nyuso pekee, au katika matamshi ya mara kwa mara dhidi ya Wamarekani. Uhuru wa kweli ni uhuru kutokana na usekula wa Kimagharibi, urasilimali wake, Demokrasia yake na mfumo wake wa kisiasa wa kiulimwengu. Uhuru wa kweli unaamuru kujitolea kamilifu kwa Kalima, kama inavyorejelewa, katika msemo maarufu, "Nini maana ya Pakistan? Laa ilaha ilAllah.”

Hivi sasa, siasa nchini Pakistan, kama ilivyo katika Ulimwengu wote wa Kiislamu, inafafanuliwa na hadhara ya Kimagharibi. Ni uchungaji na uwakilishi wa watu katika mambo yao, lakini kwa upande unaogongana na Uislamu, katika mizizi pamoja na matawi yake. Zinatokana na mtazamo wa kisekula, ambapo dini haina dori yoyote. Dini ni jambo la kibinafsi tu na haipaswi kucheza dori katika siasa na utawala. Kwa hivyo katika nchi za Magharibi, Ukristo ni dini ya dola lakini haiathiri katiba, sera na sheria za dola. Katika Ulimwengu wa Kiislamu, Uislamu ni dini ya dola, lakini pia, hauna athari juu ya katiba, sheria na sera.

Ingawa nchi za Magharibi zilipata maendeleo kwa kutabanni siasa za kisekula, Ulimwengu wa Kiislamu haujapata. Siasa za kisekula ni mlango wazi kwa wakoloni kulazimisha matakwa yao kwa Ulimwengu wa Kiislamu. Kipote cha wanasiasa wa ndani wanaziendesha siasa, sheria na katiba ili kutumikia maslahi ya wakoloni. Kwa hivyo, Ulimwengu wa Kiislamu una uongozi wa kisiasa ambao umesalimisha maamuzi yake kwa wageni. Utaendelea kufanya hivyo, kwani hauna kipimo cha Uislamu, kuzuia hilo.

Marekebisho ya siasa katika Ulimwengu wa Kiislamu ni hitaji la wakati huu. Marekebisho kwa Muislamu ni kwa mujibu wa kipimo cha Dini ya Uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ»

Wana wa Israeli wanasiasa wao walikuwa ni mitume wao. Kila alipokufa mtume mmoja, alirithiwa na mtume mwengine. Na hakika yake hakutakuwa na mtume mwengine baada yangu. Watakuwepo makhalifa na watakuwa wengi.” Mtume kisha akaulizwa, فَمَا تَأْمُرُنَا “Watuamrisha nini?” Yeye (saw) akasema,

«فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ فَالْأَوَّلِ أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»

“Mpeni ahadi ya utiifu (Bay’ah) mmoja baada ya mwengine na muwape haki yao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza yale aliyowatawalishia.” [Bukhari na Muslim]

Katika ufafanuzi (sharh) wake wa Hadith hii ya Mtume, Imam An-Nawawi, aeleza, يَتَوَلَّوْنَ أُمُورهمْ كَمَا تَفْعَل الْأُمَرَاء وَالْوُلَاة بِالرَّعِيَّةِ “Wanatawala mambo yao kama wafanyavyo watawala (Umaraa) na magavana (Wulaat) kwa raia.” Kwa hivyo kama ambavyo Mitume (as) waliamua mambo kupitia wahyi, hivyo hivyo watawala na magavana wa Kiislamu. Alieleza zaidi, وَالسِّيَاسَة الْقِيَام عَلَى الشَّيْء بِمَا يُصْلِحهُSiasa: Ni utekelezaji kitu, kupitia kile chenye kukitengeza.” Marekebisho yanatokana na Uislamu pekee, na sio kitu chengine. Kwa hiyo Waislamu wanawakilishwa na Khalifah, ambaye anapewa Ba’yah kwa uteuzi wao. Kisha anakuwa mchungaji wa Waislamu katika mambo yao, lakini kutoka pembe ya Uislamu. Hivyo basi, katiba, sheria na sera zote lazima ziwe kwa mujibu wa Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Hili ndilo linalofunga mlango kwa mkoloni na kupelekea uhuru wa kweli katika maamuzi ya kisiasa.

Hivyo, ni Dola ya Khilafah ndiyo itakayohakikisha uhuru kamili kutokana na utashi wa mkoloni. Ni Khilafah ndiyo itakayounganisha Ulimwengu wa Kiislamu, kuwa dola moja, na kuondoa mipaka ya wakoloni. Khilafah ndiyo itakayozikomboa Ardhi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu, na kupuuza vizuizi vya mfumo wa kisiasa wa kikoloni. Na ni Khilafah ndiyo itakayofungua Dawah kwa ulimwengu mzima, ikiondoa vikwazo vya kimada kupitia Jihad, mpaka, inshaa Allah, ulimwengu mzima utawaliwe na Uislamu.

Ama kivitendo, ni nani atakayeongoza marekebisho haya ya kisiasa ya Ulimwengu wa Kiislamu, Hizb ut Tahrir lazima, kwa uchache, izingatiwe. Hizb ut Tahrir imetoa katiba nzima, yenye ibara 191, inayotoa ruwaza pana ya dola ya Kiislamu ya Khilafah. Zaidi ya hayo, imetabanni maktaba ya vitabu, ambavyo vinatoa ufafanuzi wa kina wa mambo ya utawala na siasa kwa mujibu wa Uislamu, uliotolewa kutoka katika karne nyingi za mijaladi ya vita vya Fiqh ya Kiislamu vilivyo andikwa juu ya mada hiyo. Imewatayarisha kada za Waislamu, wanaume na wanawake, kutoka madh’hab zote, kuanzia Indonesia hadi Morocco, ambao wameelimishwa na kufunzwa katika kutekeleza siasa kutoka katika mtazamo wa Uislamu. Ni kutokana na mtazamo huu kwamba Waislamu wa Pakistan wanahitaji kutathmini upya kaulimbiu maarufu, "Kuna ombwe la uongozi." Pengine, ikiwa itamridhisha Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir itatupeleka kwenye uhuru halisi ambao sote tunaomba Dua kwa ajili yake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu