Jumatatu, 06 Rajab 1446 | 2025/01/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mwaka wa Kwanza wa Utawala wa Taliban

(Imetafsiriwa)

Baada ya miaka 19 na miezi 9 na kwa gharama ya zaidi ya dolari trilioni 2, serikali inayoungwa mkono na Marekani nchini Afghanistan ilianguka baada ya Taliban kuuzingira mji mkuu, Kabul mnamo Agosti 2021. Kuanguka huko kulikuwa kwa haraka na kwa kushangaza, na kuhitimisha kushindwa kwa aibu kwa Marekani, kubaya zaidi tangu kuanguka kwa Saigon. Ulimwengu ulitazama huku Talban wakirudi madarakani baada ya mapumziko ya miongo miwili. Madai yalianza mara moja kwamba mfumo mkali wa utawala wa kiimla ungewanyang'anya watu wa Afghanistan haki zote na utawala wa kikatili wa Taliban wa miaka ya tisiini umeregea. Taliban ilirithi mkorogo baada ya uvamizi wa miongo miwili wa Amerika kumalizika. Lakini licha ya mafanikio kadhaa katika mwaka wao wa kwanza madarakani, changamoto katika nchi hiyo yenye milima zinaongezeka kwa kasi.

Taliban walitakiwa, kwa hakika kwa usiku mmoja, kubadilika kutoka kuwa waasi wa muda mrefu hadi kwenye maisha yao mapya kama maafisa wa serikali. Taliban ilitangaza serikali mpya ya mpito mnamo 7 Septemba 2021 ikitangaza nchi hiyo kuwa ni ‘Imarati ya Kiislamu’. Kiongozi Mkuu, ‘Amir al Mumineen’ (Kamanda wa waumini) Mullah Haibatullah Akhundzada, hakuchukua dori rasmi ndani ya serikali ya mpito lakini anasalia kuwa mamlaka kuu ya harakati hiyo juu ya masuala ya kisiasa na kijeshi. Serikali ya mpito ilijumuisha kaimu Waziri Mkuu na manaibu wawili wa Waziri Mkuu. Mohammad Hassan Akhund, ambaye alikuwa karibu na mwanzilishi wa harakati hiyo, alitangazwa kama kaimu Waziri Mkuu. Manaibu wake wawili walikuwa mwanzilishi mwenza wa Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar, aliyeongoza tume ya kisiasa ya Taliban na Abdul Salam Hanafi ambaye alikuwa mjumbe wa tume ya kisiasa ya Taliban iliyojadiliana katika mazungumzo ya amani ya Qatar na makubaliano ya amani yaliyofuata na Marekani. Serikali pana ya Taliban ilijumuisha wanaume waliokuwa kwenye orodha ya magaidi wa Marekani na orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Sirajuddin Haqqani, mtoto wa Jalaludeen Haqqani mkuu wa zamani wa mtandao wa Haqqani, akawa waziri wa mambo ya ndani. Muundo wa serikali nchini Afghanistan unafanana sana na serikali ya hapo awali iliyoungwa mkono na mataifa ya kigeni. Hakujawa na maelezo yoyote au mpangilio wa kanuni au falsafa ya utawala wa Kiislamu au jinsi Taliban inavyopanga mpito hadi utawala wa Kiislamu.

Huku Taliban ikimakinika madarakani, hakukuwa na mauaji ya kimadhehebu au ya kikabila kama nchi za Magharibi zilivyodai. Utabiri wa mauaji ya watu wengi kutoka Magharibi uligeuka kuwa makosa kabisa. Wizara ya Habari ya Afghanistan ilithibitisha 'Imarati ya Kiislamu' ilitangaza msamaha wa jumla kwa wapinzani wake wote, wakubwa kwa wadogo. Hawa ni pamoja na wale waliobeba silaha, Daesh au wanachama wa vuguvugu la upinzani la Panjshir. Serikali ya Taliban ilialika kila mtu kwenye maisha ya amani chini ya kivuli cha 'mfumo wa Kiislamu'. Wizara hiyo ilieleza jinsi idadi kubwa ya wapinzani walivyojisalimisha na tume ya kuwasiliana na Waafghani kuanzishwa, kwa mwaliko ambao mawaziri muhimu na wabunge wa utawala uliopita wanaregea katika nchi yao kwa kuiamini ‘Imarati ya Kiislamu’. Mwaka mmoja baadaye, Afghanistan inahisi kuwa salama na isiyo na vurugu kuliko ilivyokuwa katika miongo kadhaa. Graeme Smith, mshauri mkuu wa Mpango wa Asia wa Kundi la Kimataifa la Migogoro, alibainisha kuwa awamu hii ya utawala wa Taliban "...pengine inaorodheshwa kama kipindi cha amani zaidi cha miezi sita ambacho Afghanistan imefurahia katika miongo minne."

Taliban imerithi uchumi uliojengwa kwa karata ambao unangojea kuporomoka.

Kabla ya Taliban kuchukua utawala Agosti 2021, mgogoro mkubwa wa kibinadamu tayari ulikuwepo nchini Afghanistan, kutokana na mzozo wa miongo miwili. Mfumo rasmi wa benki uliokuwepo uondoka kwa kuondoka Marekani na hii ilimaanisha biashara za Afghanistan na serikali zilishindwa kuhamisha fedha. Kufungiwa na kisha kukamatwa kwa fedha za benki kuu ya Afghanistan na Marekani kulidhuru zaidi uchumi wa Afghanistan. Tangazo kwamba nusu ya fedha hizi zitatumika kwa kesi za wahasiriwa wa 9/11 lilisababisha Taliban kudai kwamba dola za Kimagharibi zimeisaliti harakati hiyo, kuvunja ahadi zilizotolewa hapo awali, na kutoa matakwa zaidi bila ya kutoa chochote kikubwa kama badali. Hisia ya usaliti inaonekana kuimarisha mabishano miongoni mwa viongozi wa Taliban kupitia kutabanni msimamo mkali na kuregelea baadhi ya ahadi zao wenyewe.

Uongozi wa Taliban umekuwa katika machungu ya kueneza ujumbe tofauti kabisa ili kuepuka janga lile lile lililotokea miaka 20 iliyopita. Wamejitahidi kuamuru vikosi vyao vya ardhini kufanya kazi kwa kujizuia na kuwashawishi Waafghan wote juu ya nia yao nzuri. Viongozi wa Taliban mara moja walitangaza msamaha wa jumla kwa mtu yeyote ambaye alifanya kazi kwa utawala uliopita na pia wakawataka maafisa wa serikali na waandishi wa habari, wakiwemo wanawake, kuregea kazini, na hata kuyafikia makundi ya wachache ili kupunguza wasiwasi wao.

Lakini Magharibi haijashawishika na vyombo vyake vya habari na maafisa wameingia katika wingi wa kuwachora Taliban kwa sura hasi. Ahadi ambazo Taliban wametoa kuhusu haki za raia wa Afghanistan, makabila madogo ya kidini, wanawake, na watu wa tabaka la kati wasomi kwa jumla zimekuwa za utata na mara nyingi zinakinzana. Kuna mgawanyiko wa wazi ndani ya vuguvugu la Taliban kati ya wale wanaopinga kufanya makubaliano yoyote na wale wanaotaka kupata uhalali wa kimataifa. Taliban baada ya mwaka mmoja wa utawala wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama, kiuchumi na kijamii. Haya yote yanafanyika huku Marekani na washirika wake wakiendelea kuishinikiza Taliban juu ya masuala haya kwa matumaini kwamba Taliban italegeza misimamo na kukubaliana na matakwa ya Magharibi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu