Uoanishaji wa Waislamu nchini Denmark Unahusiana na Maadili na Imani, Sio Kazi wala Elimu
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 30 Septemba, Wizara ya Uhamiaji na Uoanishaji ya Denmark ilichapisha ripoti ya hali ya kile kinachojulikana kama kipimo cha uoanishaji. Kipimo hicho cha uoanishaji kilichapishwa mnamo 2012, na kinakusudiwa kuonyesha maendeleo katika uoanishaji wa wahamiaji wasio wa Kimagharibi ndani ya malengo kama vile kazi, elimu na lugha.