Alhamisi, 05 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina): Watu wa Palestina Wanauita Umma na Majeshi yake Kuinusuru Gaza na Jenin!

Chini ya anwani, “Enyi Majeshi ya Waislamu ... Ni Nani Atakayenusuru Rafah, Jenin, na Palestina yote ikiwa Nyinyi Hamtazinusuru?!”, umati mkubwa wa watu wa Palestina ulishiriki katika mji wa Al-Bireh matembezi yaliyoitishwa na Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina mnamo siku ya Ijumaa, 16 Dhu al-Qa'dah 1445 H sawia na 24 Mei 2024 M, wakiyataka majeshi ya Waislamu na vikosi vya silaha kuisuluhisha Palestina na watu wake kutokana na uhalifu wanaotendewa na umbile la Kiyahudi.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Mkutano wa Waandishi Habari mjini Port Sudan “Suluhisho Linatoka Ndani”

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan ilifanya mkutano na waandishi wa habari uliofaulu wenye kichwa: “Mgogoro wa Sudan...Suluhisho Linatoka Ndani,” mnamo siku ya Alhamisi, 8 Dhul-Qa'adah 1445 H sawia na 16 Mei 2024 M, katika ukumbi wa mikutano, katika Hoteli ya Al-Basiri Plaza mjini Port Sudan.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina): Qalqilya... Mkutano mkubwa wa Hadhara wa Kuinusuru Gaza na Rafah!

Alasiri ya leo Jumamosi tarehe 18/05/2024, umati mkubwa wa watu kutoka eneo la mkoa huu na maeneo ya jirani walikusanyika katikati ya mji wa Qalqilya, kuitikia wito wa Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina), ambao iliuelekeza kwa watu kuinusuru Gaza na Rafah, kukusanyika katika kisimamo cha halaiki chini ya kichwa, “Enyi Waislamu: Rafah baada ya Gaza Inalilia msaada, basi ifikieni,”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi “Musiitelekeze Rafah kama Mulivyoitelekeza Gaza!”

Matembezi ya 31 mfululizo, tangu kuanza kwa vita vya Kimbunga cha Al-Aqsa, yalianza mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu wa Tunis, ambayo yaliitishwa na Hizb ut-Tahrir/Wilayah Tunisia, kwa watu wa Al-Zaytouna, na kichwa chake kilikuwa“Musiitelekeze Rafah kama Mulivyoitelekeza Gaza!”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Uholanzi: Matembezi ya Amsterdam “Komesheni Mauaji ya Halaiki Mjini Gaza”

Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa maandamano katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kuinusuru Gaza, yenye kauli mbiu “Komesheni Mauaji ya Halaiki Mjini Gaza.” Maandamano hayo yalizunguka mitaa ya Amsterdam, yakisindikizwa na nyimbo za vijana wakitaka kunusuriwa kwa Gaza na kuhamasishwa kwa majeshi ya Waislamu.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Amali Kubwa “Imetosha… Umewadia Wakati wa Vitendo sio Maneno!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miezi saba, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 115,000, wanaume na wanawake, hadi sasa, Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Uturuki inaandaa amali kubwa za halaiki katika maeneo 17 tofauti tofauti nchini Uturuki.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu